Sunday, September 9, 2018

Rc Hapi Ataka Kiwanda Kuzalisha Karatasi Nyeupe Mufindi.

Rc Hapi wa Pili Kulia akikagua Kiwanda cha Karatasi Mgololo wakati wa ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa iliyofanyika katika Tarafa ya Kasnga Kata ya Makungu Wilayani Mufindi, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William

NaAmani Mbwaga, Mufindi
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ali hapi amekitaka kiwanda kinachazolisha karatasi cha MPM-Mgololo Mufindi  kilichopo wilayani Mufindi Mkoani Iringa kuanza kuzalisha karatasi nyeupe zitakazotumika kutengenezea vitabu madaftari na karatasi za ofsini.

Ameyasema hayo mapema leo hii wakati akikagua uzalishaji wa karatasi katika kiwanda cha MPM - Mgololo Kilichoanzishwa na Hayati baba wa Taifa Mwalimu Jk Nyerere ikiwa ni siku yake ya  kwanza kufika baada ya uzinduzi wa kampeni ya tarafa kwa tarafa Wilayani Mufindi yenye lengo la kurudisha nidhamu kwa watumishi wa umma.

“Nimekuja kuona ni kitu gani ambacho Baba wa Taifa alituachia sisi na hasa wanaIringa  na wajibu wetu ni nini katika rasilimali hii iliyobinafsishwa kwa mashariti nafuu kwamba wale waliokabidhiwa wanafanya kazi kwa makubaliano na mashariti yaliyotolewa kwa wakati huo” Alisema Mhe Hapi

Alibainisha kuwa faraja yake ni kwamba kiwanda kinafanya kazi na ndio kiwanda kikubwa kuliko vyote Tanzania kinachoshughulika na karatasi, kiwanda hiki hutoa huduma za jamii, ajira, huchangia pato la Taifa na Mkoa wa Iringa kwa ujumla.

Kuna aina kuu mbili za karatasi zilizokuwa zinazalishwa wakati wa Baba wa Taifa, kwanza ni karatasi ngumu hizi hutumika kutengenezea mifuko ya Cement na ile mifuko rafiki wa Mazingira.

Aina ya pili ni karatasi nyeupe za Madaftari, vitabu na zinazotumika maofsini hivyo ni kwanini kiwanda hakizalishi karatasi nyeupe alihoji Mhe Hapi huku akisema nchi yetu inahitaji karatasi za kutosha Necta inahitaji na kwingine kwingi kwa kufanya hivyo pato la Taifa litaongezeka, na ajira kwa Watanzania.

Aliongeza pia kwamba zaidi ya asilimia 90 ya mashine zinazofanya kazi zilinunuliwa na Mwalimu Nyerere.

“Hii ni mali ya watanzania, hizi ni juhudi na historia iliyotukuka kwa viongozi wetu kazi kubwa ni sisi viongozi tuliopo sasa tunaomsaidia Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni namna gani tunapanga kuhakikisha tunamsaidia ili viwanda viwe na tija iliyokusudiwa na Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere, alisema Mhe Hapi.

Kiwanda cha karatasi Mgololo kilijengwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu JK Nyerere katika miaka ya 1980.

Thamani ya Kiwanda ilikuwa ni dola 360 ambazo kwa thamani ya sasa ni tkribani Trilioni 1 na zaidi.

Aidha Mhe Hapi katika ziara yake alikagua pia mradi wa ujenzi wa kituo cha Afya kilichofadhiliwa na kiwanda cha karatasi Mufindi kilichopo Mgololo, Mabara ya Mgololo Sekondari yenye ghorofa moja iliyojengwa kwa zaidi ya milioni 400 fedha za kitanzania na Mwisho kufanya Mkutano wa hadhara katika Tarafa ya Kasanga kata ya Makungu ambapo amezungumza na wananchi na kusikiliza kero zao ikiwemo kuzitatua kupitia Mahakama ya Wananchi ya Iringa Mpya.


HABARI PICHA ZIARA NZIMA RC HAPI.

RC Hapi akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Karatasi Mgololo



Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William akimkaribisha RC Hapi kuzungumza na Watendaji wa Kiwanda cha Karatasi Mgololo

Kuelekea kwenye Mitambo ya Uzalishaji  Karatasi katikati ni Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi



Moja ya hatua Katika Uzalishaji wa Karatasi




RC Hapi akiangalia vipande vipande vya miti vilivyoandaliwa kwa ajili ya Uzalishaji wa Karatasi







RC Hapi Katikati  akipata Maelezo kutoka kwa Injinia Chogo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Karatasi Mgololo


RC Hapi akijionea baadhi ya Bidhaa zinazotengezwa kiwandani hapo.








Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William Aliyesimama akimweleza Rc Hapi namna Kiwanda kilivyochangia huduma kwa jamii

Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Karatasi Mgololo

RC Hapi akinesha bidhaa ya Kifungashio inayotengenezwa Uganda kutokana na Malighafi kutoka Tanzania Mgololo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa



Rc Hapi akiwa katika Picha ya Pamoja na Uongozi wa Kiwanda  na iongozi wengine


RC Hapi akipokeaTaarifa ya Ujenzi wa Kliniki ya Mama na Mtoto Katika Zahanati ya Mgololo iliyofadhiliwa na Kiwanda cha Karatasi Mgololo





Maabara za Shuleya Sekondari Mgololo zilizojengwa kwwa Msaada kutoka Kiwanda cha Karatasi Mgololo

RC Hapi akiingia katika uwanja wa Mikutano

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina





Mamia ya Wakazi waliohudhuria Mkutano wa Iringa Mpya






Kaimu Mkurugenzi  Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Bwana Isaya Mbenje akijibu baadhi ya hoja






Picha zote na Amani Mbwaga


No comments:

Post a Comment