Tuesday, October 30, 2018

TFS Sao Hill na Kampuni ya “Follow The Honey Tanzania” Kuanzisha Utalii wa Nyuki.

Na Amani Mbwaga, Mafinga.


Furaha kubwa katika Ziwa Ngwazi linalopatikana katika Shamba la Miti Sao Hill 
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shamba la Miti Sao Hill, iko katika mpango kabambe wa kuanzisha Utalii wa Nyuki kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya nyuki safari kutoka Marekani na kampuni ya Follow the Honey Tanzania.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Follow The Honey Tanzania Bwana Kaizerege Camara ambae aliambata na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Kampuni Tanzu ya Nyuki Safari kutoka Marekani na Follow the Honey Tanzania Bi Marry Canning katika Shamba la Miti Sao Hill liliopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa .

Ziara hiyo ilifanyika jana na  kujionea shughuli mbalimbali za ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa asali ya SaoHill Honey wamefurahishwa na jinsi shamba lilivyo na vivutio vingi hali itakayochangia kuchochea utalii wa nyuki Tanzania.

“Tumegundua kwamba Tfs ni Zaidi ya Misitu baada ya kujionea fursa zilizopo katika shamba la Miti Sao Hil ikiwemo Miti iliyopandwa, Miti ya Asili, vyanzo vya maji, ziwa aina mbalimbali za maua, kwa hiyo ni jambo la kujivunia kuona kwamba taasisi hii inafursa kubwa sana ya kuweza kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia asali na baadhi ya vivutio vilivyopo katika shamba hilo” alisema Bwana Camara.

Wameona  ufugaji wa nyuki ambao umefikia kwa kiwango kikubwa sana hadi kufikia ufugaji wa kibiashara na kuahidi kushirikiana na serikali ili kuhakikisha asali inayozalishwa Tanzania katika Shamba la Miti Sao Hill inapata masoko katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo marekani na hatimae kuitangaza nchi na kuingiza pato la Taifa.

Aidha wawekezaji hao wameahidi kuandaa Makala (Documentary) kwa kushirikiana na wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) itakayoonesha vivutio vya kipekee vilivyopo katika shamba la miti Saohill ili itumike kwenye Shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwenye video za ndege zake na ulimwenguni kote  kuonesha Utalii wa nyuki na kuitangaza asali ya Sao Hill  Honey Tanzania.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herberth Haule kwa maslahi ya umma ameahidi kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo kuhakikisha kwamba shamba la miti Sao hill linakuwa zaidi ya Miti ambapo itaongeza fursa kwa Watanzania ikiwemo ajira, kipato lakini pia kuchangia uchumi wa Taifa.

Aidha Afisa Nyuki wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Said Aboubakar ameishukuru kampuni hiyo na kusema kwamba kampuni hiyo imekuja wakati muafaka na kwa nia njema ya kukuza utalii wa nyuki nchini Tanzania hususani katika Shamba la miti Saohill hivyo ameona kuna fursa nyingi zinaweza kutumika kupitia Safari nyuki ambayo itaunganisha masoko ya asali yenye ubora kutoka Tanzania na kuuza nnje ya nchi na hatimae kujipatia fedha za kigeni.

Shamba la Miti Sao Hill lina ukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya upandaji miti na hifadhi ya mazingira, kati ya eneo hilo kiasi cha hekta 86,003 ni kwa ajili ya upandaji miti kibiashara, hekta 48,200 kwa ajili ya utunzaji  wa mazingira na vyanzo vya maji na kekta 1,700 ni kwa ajili ya makazi na uwekezaji.


HABARI PICHA


Bi Marry Canning Akisaini Kitabu Cha wageni Katika Ofisi ya Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill

Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herbert Haule

Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania Bi Marry Canning 
Majadiliano na Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Yakiendelea


Picha ya Pamoja


Banda la Uuzaji wa Asali ya Sao Hill Honey



Happy mmoja wa waandaaji wa Asali ya Sao-hill kabla haijaenda Sokoni akionesha jinsi inavyopakiwa.


Bi Mary Canning akiwa na Afisa Nyuki wa Shamba la Miti  Sao Hill Bwana Said Aboubakar












Moja ya Mzinga wa nyuki wa asili uliokuwa ukitumika  katika Shamba la Miti Sao Hill kwa ajili ya ufugaji wa nyuki















Mr Camara wa kwanza kushoto akiwa na Bi Marry na Kulia ni Bwana Side Aboubakar wakiangalia jinsi utomvu unavyovunwa Katika Shamba la Miti Sao-Hill ikiwani moja ya kivutio cha watalii.


Mr Camara Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania






Baadhi ya miche iliyoandaliwa katika shamba la miti Sao Hill tayari kwa kupandwa katika msimu huu wa upandaji miti


Baadhi ya Msitu wa Miti ya Sao Hll Katika Muonekano









Furaha kubwa katika ziwa Ngozi linalopatikana ndani ya Shamba la Miti Sao Hill ni moja ya kivutio kikubwa cha utalii














Afisa Nyuki Shamba la Miti Sao Hill  Bwana Side Aboubakar Akiwaonesha  viongozi waandamizi wa Kampuni ya Follow the honey Tanzania  (Hawapo pichani) baadhi ya mizinga ya Nyuki liyopo katika shamba la miti Sao Hill

Picha zote na Amani Mbwaga
Kwa Maoni au ushauri Wasiliana nasi;
Simu: +255 656 632 566
E-mail:prof.mbwaga @gmail.com