Na Amani Mbwaga, Mafinga
Waziri wa ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi amezitaka taasisi mbalimbali kuajili vijana wanaomaliza mafunzo ya Jkt kwani wanauzalendo wa kutosha na wanamoyo wa kufanya kazi kwa nguvu zote.
Ameyasema hayo baada ya kuombwa na Mbunge wa Mufindi Kusini Mhe Menradi Kigola alipoiomba wizara kuwapatia ajira vijana wanaomaliza mafunzo ya JKT Kujitolea kwani wanarudishwa nyumbani hali ambayo inatia wasiwasi kwamba vijana hao wanaweza kujiingiza katika vitendo viovu kwa sababu wanamafunzo ya kutosha jeshini halafu wanakosa ajira na kurudishwa mitaani.
Akijibu hoja hiyo ya Mbunge Dkt Mwinyi amewaomba kuwaelimisha vijana kwamba JKT Haiajiri bali wanafanya mchakato wa kupeleka mafunzo yaStadi za Kazi VETA ili waweze kujiajiri wenyewe.
Aidha Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe Cosato Chumi ameipongeza JKT Kwa kuwa na Uhusiano mzuri na wananchi na pia kwa ustadi mkubwa na weledi katika ujenzi wa ofisi za Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo mpaka sasa wako mbele ukilinganisha na mkataba kwa hiyo wanaspidi ya kutosha.
Dkt Mwinyi ameendelea na ziara yake katika Kikosi cha Jeshi Mafinga kukagua miradi mbalimbali inayoendeshwa na kikosi hicho kilichopo Mafinga Mjini Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
HABARI PICHA
No comments:
Post a Comment