Na Amanni Mbwaga,
Mafinga.
Waziri Jenista Mhagama akipokea zawadi ya Asali ya nyuki wasiouma |
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu Mhe Jenista Joakim
Mhagama Ameongelea Mkakati wa Kuboresha Ajira kwa Vijana Kupitia Mradi wa
Kitalu nyumba (Green House) Kwa Kila Halmashauri.
Ameyasema hayo
alipofanya ziara yake katika Halmashauri za Wilaya ya Mufindi “tumefanya
Utafiti tumeona kiwango cha upungufu wa ajira kinazidi kupungua, sasa hivi tumefikia
kiwango cha asilimia 10.3” alisema Mhe Mhagama.
Serikali imefanya
utafiti wa nguvu kazi iliyopo na kugundua asilimia 56 ya nguvu kazi yote ni
vijana, na wengi wao waliomaliza darasa la saba na kidato cha nne hawana ujuzi
kabisa hivyo kazi kubwa ya wizara ni kutoa mafunzo ya ujuzi kwa vijana ili
watoke kwenye asilimia 79.9 angalau ifikie asilimia 54.
Mhe Mhagama
ameziagiza Halmashauri kote nchini kutafuta vijana 100 watakaopata mafunzo kwa
muda wote katika kitalu nyumba (Green house) na huu utakuwa mpango endelevu kwa
kila mwaka ili kufikia vijana 500 kwa kila Halmashauri.
Kunatakiwa kuwe na kitalu
nyumba (Green House) 500 mpaka 1000 zinazomilikiwa
na vijana katika kila halmashauri, ambapo kunakua na uhakika wa soko,
uzalishaji ambao unatija kwa vijana ili kujenga uchumi na hatimae kuchangia
pato la halmashauri na Taifa kwa ujumla.
“Mkoa wa Iringa ni moja
kati ya Mikoa 7 tu ambayo tulitoa taarifa kwa mikoa yote Tanzania bara lakini
ni mikoa 7 ndio iliyoweza kuonesha uthubutu wa utekelezaji ikiwemo mkoa wenu wa
Iringa hivyo nina wapongeza sana” alisema Mhe Mhagama.
Wilaya zote ambazo
ziko katika mkoa wa Iringa zitanufaika na miradi hiyo mikoa mingine ni Ruvuma,
Mwanza, Kagera, Simiyu, Manyara, Lindi na baadae kufikia mikoa yote Tanzania
bara.
Mhe Waziri amehakikisha
kwamba mwezi huu wa 10 mwishoni ni lazima utekelezaji wa miradi hiyo uanze
kuonekana.
Ukweli ni kwamba ifikapo
tarehe 30 oktoba kama kuna Halmashauri haijatekeleza vigezo vilivyowekwa ambapo
ni mkataba baina ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Halmashauri, basi mradi
utahamishwa na kupelekwa halmashauri zingine za jirani ili ziwe na faida ya
miradi miwili na kuendelea.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William amemuhakakikishia Mhe Waziri kusimamia
ipasavyo mradi huo katika halmashauri zake za wilaya ya mufindi ili zisije
zikanyang’anywa miradi hiyo kwa kushindwa kufikia vigezo, na amewaagiza
wakurugenzi wote kuhakikisha wanasimamia ukamilishaji wa vigezo ili miradi iwe
endelevu na ameapa kama mradi utahama basi na mkurugenzi wa halmashauri hiyo
ajiandae kufungasha vilago vyake.
HABARI PICHA
Waziri Jenista Mhagama akiwasili katika ofisi za Mkuu wa Wilaya Mufindi na Kupokelewa na Mwenyeji wake Mhe Jamhuri William ambae ndie Mkuu wa Wilaya hiyo |
Waziri Jenista Mhagama akisalimiana na Mwenyekiti wa Ccm Wilaya ya Mufindi Ndugu Daud Yassin |
Waziri Jenista Mhagama akisalimiana na Mwakilishi kutoka Ofisi ya Katibu Tawala (RAS) Mkoa wa Iringa |
Waziri Jenista Mhagama akisalimiana na Afisa Uhamiaji wa Wilaya Mufindi |
Waziri Jenista Mhagama akisalimiana na Kamanda wa Zimamoto Wilaya ya Mufindi |
Waziri Jenista Mhagama akisalimiana na Afisa Usalama wa Taifa Wilaya ya Mufindi |
Waziri Jenista Mhagama akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bwana Isaya Mbenje |
Mkuu wa wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William (Kulia) akitoa taarifa ya Wilaya ya Mufindi kwa Mhe Waziri Jenista Mhagama |
Afisa Kilimo wilaya ya Mufindi Bwana Lubuva akitoa maelezo utekelezaji wa mradi wa Kitalu nyumba kwa waziri Jenista Mhagama |
Waziri Jenista Mhagama akifurahia zawadi ya Asali ya nyuki wasiouma kutoka kwa wajasiriamali wadogo ambapo kwa niaba yao Mkuu wa Wilaya Mufindi alikabidhi zawadi hiyo |
Waziri Jenista Mhagama tayari kuendelea na Safari yake Jijini Dodoma Picha zote na Amani Mbwaga Kwa Maoni au Ushauri Wasiliana nasi Mob: +255 656 632 566 E-mail:prof.mbwaga@gmail.com |
No comments:
Post a Comment