Monday, December 16, 2013

SEMINA YA SIRI YA KUWA MILLIONEA YA SHIGONGO,SUGU MASANJA MKANDAMIZAJI NA MWANG,AMBI YAFANA SANA JIJINI MWANZA.



Mwanza, Jana ktk viwanja vya CCM KIRUMBA, Ilifanyika Bonge la Semina Kubwa ya Ujasiriamali kwa wananchi wa mwanza, ambapo semina hiyo ilikuwa nawazungumzaji wakuu. Mr SHIGONGO ERIC, EMANUEL MGAYA(MASANJA MKANDAMIZAJI) JOSEPH MBILINYI .(SUGU) Ambaye ni mbunge wa jiji la mwanza. pia semina hiyo ilisindikizwa na Bonge la  burudani  kutoka kwa wasanii mashuhuri hapa nchini wakiwemo, FIDQ, H-BABA, YOUNG KILLER, MARTHA MWAIPAJA NA MH: SUGU Alitoa bonge ya burudani.

Semina hiyo ijulikanayo kama STREET UNIVERSITY, Inayomilikiwa na Shigongo na Mwang,ambi imeleta mabadiliko makubwa sana kwa vijana wa mwanza ambapo wamejua siri kubwa ya mafnikio katika ujasiiamali. semina ilianza tarehe 13/12/2013-15/12/2013. 

Mzungumzaji mkuu alikuwa Mr SHIGONGO ERICK ambaye alieleza historia ya maisha yake tangu alikotoka mpaka kufikia mafanikio yake. yeye ni mzalwa wa hapa mwanza na kasoma shule ya msingi  hapahapa mwanza, pia alikulia ktk familia masikini sana lakini juhuudi zake ndizo zilizopelekea kuanikiwa kwake leo hii. kipaji alichonach kikubwa ni uandishi, lakin hajawahi kusoma chuo chochote cha uandishi, hivyo alitumia ndoto yake na kipacji alichopew na mungu kufikia mafanikio hayo. ktk mazungumzo yake alitaja mambo kumi ya kufnikiwa ktk maisha na baaadhi ya mambo hayo ni:

1.Choka na mahali ulipo na kamwe usiridhike hata kidogo
2. kuwa na ndoto na kuwa na hasira ya mafanikio
3.Kuwa na mipango na njia za kufikia kutekeleza mipango yako ili kufikia lengo lako
4. kufanya utekelezaji wa wazo na mipango yako (implementation) pia uwe na viungo vya mafanikio kama wazo fedha, watu nk
5. Nidhamu ktk fedha. nk    na mengine mengi zaid tafuta Cd yake ina mambo mengi ya msingi.

Mzungumzaji wa pili Mr JAMES MWANG,AMBI yeye alifundisha vtu vingi sana baadhi ya vitu hivyo ni:
MAMBO MAKUU MANNE YA KUFAULU MAISHA.
1.Ndoto
2.Imani
3.Malengo
4.Bidii      

Pia alizungumzia MAMBO MAKUU 4 YA MUHIMU KTK KUJENGA BIASHARA IMARA.
1.Uongozi na menejimenti ya Biashara
2.Bidhaa au huduma ni lazima iwe na kiwango
3.Ujuzi wa masoko na mauzo
4.Huduma bora kwa wateja( customer service) na mabo mengine mengi.

 Mzungumzajia wa Tatu EMMANUEL MGAYA(MASANJA) yeye alifundisha kupitia Historia ya maisha yake aliyopitia ambayo yalikuwa magumu sana, lakini juhudi zake na kufanya kazi kwa bidii bila kukata tamaa ndiko kumempa mafanikio makubwa aliyonayo sasa, ambapo anamiliki magari , Nyumba bora na kali sana ya Ghorofa pale jijin Dar, pia Ni Mkurugenzi na Mmiliki wa Kampuni ya ulinzi ijulikanayo kama OK security company. zaidi aliwataka watu kukomaaa na kuokata tamaa ili kutimiza ndoto zao.

Mzungumzaji wa Nne ni Mh. JOSEPH MBILINYI (SUGU) mbunge wa mbeya mjini yeye alizungumzia zaidi kwamab kila kiyu kinawezekana ili mradi tu umeamua na kutokata tamaaa, aliwafundisha watu ia kupitia historia ya maisha yake kutoka mwanamziki hadi kuwa Mheshimiwa lajini mziki bado anaupiga kama kawa na amesema kamwe hawezi kuacha mziki kwani ni sehemu ya maisha yake. Kwa kweli ilikuwa ni ya aina yake na ya kihistori .

 Mimi binafsi imenigusa sana na kuamsha fikra zaidi za kuwa na mawzo na ndoto kubwa ili kuzitimiza. ewe kijana Mtanzania fursa ni nyingi sana hapa nchini tengeneza dhana na uwezo wa kujiajaili mwenyew na kuajili wengine na zaidi kutotegemea ajira za kuajiriwa hili litaipunguzia mzigo serikali kuwa na watu na vijana wengi ambao wamesom lakin wako mtaani. Himahima vijana Mlimaliza elimu ya juu jiungeni ktk vikundi mbalambali ili muweze kukopesheka na muweze kuendeleza biashara zenu enyewe.

 Tunawashukuru sana kwa kuja na wazo hli la STREET UNIVERSITY. ambalo naamini litakuwa suluhisho kubwa la ukosefu wa ajira hapa nchini. Mungu wabariki watu hao Mungu ibariki Tanzania Mungu wabariki vijana Wa Kitanzania ili Tuweze kufikia na kutimiza ndoto zetu.

Imeandaliwa na :
AMAN E. MBWAGA
Mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuo kikuu cha Mt Agustino Mwanza (2013)
(BA in PUBLIC RELATIONS & MARKETING) 
CONTACTS. Email: prof.mbwaga@gmail.com
Twiter:@amanmbwaga
Mobile; +255765058711


PICHA NA MATUKIO YALIYOJILI KATIKA SEMINA HIYO PALE CCM KIRUMBA.

Erick Sigongo akitoa semina





Aman Mbwaga akiwa na Erick Shigongo Mtunzi maarufu wa vitabu nchin Tanzania
wananchi wa mwanza

Aman Mbwaga akiwa na Mr James Mwang,ambi mkufunzi wa semina.


Mh SUGU akitoa semina

Hapa sugu Kaamua kuchana mistari






Wafnayakazi wa tigo wakisikliza semina kwa makini



Aman Mbwaga akiwa na Masanja Mkandanizaji huku semina ikiendeea.

H.Baba akitoa vitu vyake jukwaani

Aman mbwaga akiwa na Msanii wa Muziki H.BABA


Msanii Young KILER Akiwaburudisha wananhi wa Mwanza
FIDQ nae akifanya vitu nvake jukwaani






ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YANGU MUNGU AKUBARIKI NA KARIBU TENA.

No comments:

Post a Comment