Na Amani Mbwaga,
Mufindi
Hayo yamesemwa jana
wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya Jeshi la akiba (Mgambo) yaliyofanyika katika kata ya Mninga
Tarafa ya Kasanga wilayani Mufindi Mkoani Iringa ambapo mgeni rasmi wa hafla
hiyo alikuwa ni Mkuu wa Wilaya na Mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama (W) Mufindi Mhe. Jamhuri William.
Katika hotuba yake
Mhe William alisema mafunzo ya Jeshi
la akiba ni mafunzo ambayo yako rasmi
kabisa katika utendaji kazi wa serikali na yapo kwenye katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977.
Ndio maana kwa
kutambua umuhimu wa Jeshi la akiba serikali imeanzisha maalumu Kamandi ya Jeshi
la Akiba ambalo ni rasmi katika miongozo na usimamizi wa Jeshi la Ulinzi wa
Wananchi JWTZ.
Kwa hiyo sio mafunzo
ambayo ni lele mama, bali ni mafunzo ambayo yamezingatia sera kanuni, taratibu
na miongozo yote inayohusiana na ulinzi wa Taifa la Tanzania.
“Vijana mimi kama
mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na usalama Wilaya Mufindi nawapongeza sana na
nawatia shime endeleeni na uzalendo huo na Mungu atawabariki katika utumishi
wenu” Alisema.
Serikali wilayani
mufindi imedhamiria katika shughuli zote za kiserikali itawatumia askari hao wa
Jeshi la Akiba pamoja na askari wengine katika shughuli zote za kitaifa.
“Hivyo natoa wito
Makampuni mbalimbali yanayotaka kufanya kazi Mufindi na wanahitaji walinzi basi
wasihangaike wala kuangalia pembeni wahakikishe wanachukua vijana hawa kwa
sababu tayari wameiva na wana uzalendo mkubwa katika kulitumikia Taifa.
Akitoa taarifa ya
mafunzo Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya
Mufindi Meja RN Mwasakyene alisema mafunzo hayo yalianza tangu trehe 02 Julai
2018 wakiwa jumla ya wanafunzi 220, Wanawake wakiwa idadi 45 na Wanaume idadi 175.
“Mpaka leo hii
tunawahitimu 217 wanaume wakiwa idadi 173 na wanawake 44 sababu za wengine
kushindwa kuendelea ni utovu wa nidhamu na hasa utoro wa muda mrefu” alisema
Meja Mwasakyene.
Aidha masomo
yaliyofundishwa ni utimamu wa mwili, ujanja wa porini, uhandisi, mbinu za
kivita, usomaji wa ramani, mabomu ya mkono na baadhi ya silaha.
Akisoma Risala ya
utii kwa mgeni rasmi mmoja wa wahitimu alisema walisoma pia masomo ya uraia
ikiwemo zimamoto , uhamiaji, kuzuia na
kupambana na rushwa na hatimae usalama wa raia.
Vijana hao wakati wa
mafunzo yao walishiriki pia katika kufanya huduma za kijamii ikiwemo kuchimba
mshimo ya vyoo katika shule ya msingi Lugoda iliyopo kata ya Mninga.
Aidha wameomba
mikataba ya ulinzi katika sekta binafsi au serikalini itolewe pale wanapopata
fursa ya kuajiliwa wanataka wajue mikataba hiyo lakini pia na mkuu wa wilaya
awe anaifahamu kwani ndio mtetezi wao mkuu, wanaamini atawasaidia.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi na Diwani wa kata ya Mninga Mhe
Fsto Mgina amewapongeza wahitimu hao wa Jeshi la akiba kwa kumaliza mafunzo yao
salama na kusema wao kama viongozi wa serikali wanafarijika sana kuona vijana
wanamaliza mafunzo hayo kwani watakuwa chachu ya maendeleo.
Baadhi ya wahitimu
wa mafunzo hayo ya jeshi la akiba walipata wasaa wa kueleza furaha yao akiwemo
Mhitimu Vivian Kihombo Msichana mashuhuri aliekuwa paredi kamanda amesema “Mimi
nilichojifunza katika mfunzo haya ni kuwa mzalendo aidha nawahamasisha vijana
wenzangu waje kufanya mafunzo haya na kamwe wasiogope”
Nae Mhitimu Zaire
Januari Mdeta alisema “ Mimi nimepata faida ya kuwa timamu kimwili, na
kiakili lakini pia naipenda nchi yangu
ndio maana nimjifunza uanajeshi ili niweze kutetea raia na mali zao na niko
tayari hata kufa kwa ajili ya wengine kupona na kutetea taifa langu”.
Hafla hiyo
iliambatana na maonesho ya gwaride, singe, kwaya na shairi.
HABARI PICHA
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William akipokea Salamu ya Heshima |
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William Akitoa Hotuba |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi na Diwani wa Kata ya Mninga Mhe.Festo Mgina akitoa salamu za kata yake. |
Wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la Akiba Mufindi |
Mshauri wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Mufindi Meja RN Mwasakyeni akitoa Taarifa ya Mafunzo |
Paredi ikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa Mwendo wa pole Ikiongozwa na Paredi Kamana Vivian Kihombo |
Paredi ikipita mbele ya Mgeni Rasmi kwa mwendo wa Haraka |
Msoma Risala akikabidhi kwa Mgeni Rasmi DC Mufindi |
Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mufindi |
Kikundi cha Singe |
Kikundi cha Kwaya |
Pichani Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Mufindi (Katikati) akiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Mufindi |
Mgeni Rasmi DC Mufindi Katikati akiwa na Wakufunzi wa Jeshi la Akiba Wilaya ya Mufindi |
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William Katikati akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Paredi ya Wahitimu wa Jeshi la Akiba Mufindi |
Mgeni Rasmi DC Mufindi akiwa katika Picha ya Pamoja na Washindi waliopewa zawadi kwa kufanya vizuri zaidi katika mafunzo yao |
Ugeni ukiondoka kutoka Uwanjani (Picha zote na Amani Mbwaga) |
No comments:
Post a Comment