Friday, December 21, 2018

Sao Hill Forest FC yawasili Jijini Dar es salaam tayari kwa Michezo ya Kirafiki na Kushinda Mechi ya Kwanza.


Na Amani Mbwaga, Dar es salaam.

Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shamba la Miti Sao Hill, kupitia timu yake ya mpira wa miguu imewasili vyema jijini Dar es salaam Jana usiku ikitokea Mafinga Wilayani   Mufindi Mkoani Iringa.

Kiongozi wa Msafara na Mwenyekiti wa Misitu Sports Bonanza ambae pia ni Afisa Nyuki wa Shamba la miti Sao hill Bwana Said Aboubakar amesema timu imewasili vyema na iko tayari kwa michezo mbalimbali ya kirafiki ambayo imeanza mapema leo hii ambapo iliikutanisha      Sao Hill Forest FC Vs Juhudi FC katika uwanja wa Kinesi muda wa saa 10:00 Jioni ambapo Sao Hill Forest imeibuka mshindi wa Magoli 02 kwa 0, Magoli yote yalifungwa na mchezaji mahiri Barnaba Mlomo Dk ya 19 na Dk 39.

Aidha kesho tarehe 22 Desemba 2018 saa 10:30 jioni mchezo wa kirafiki utaendele baina ya  KMC B Vs Sao hill Forest Fc katika Uwanja wa Shule ya Sheria (School Of Law) Dsm kuanzia saa 10:30 jioni.

Tarehe 23 Disemba 2018 saa 2 :00 asubuhi itakuwa ni Udsm FC Vs Sao Hill Forest  Fc Uwanja wa Taifa (Shamba la Bibi),  tarehe 24 Disemba 2018 saa 10:30 jioni ni Azam B Vs Sao Hill Forest FC Katika Uwanja wa Chamazi na Tarehe 25 Disemba 2018 ni Simba Sports Club B FC  Vs Sao Hill Forest FC uwanja wa Kinesi saa 2:00 Asubuhi.

Ziara hii ya kimichezo ni matokeo ya Michezo ya Misitu spots bonanza iliyozikutanisha timu takribani 32 kutoka katika zaidi ya vijiji 60 vinavyolizunguka shamba la miti Saohill ambapo miongoni mwao walichaguliwa takribani wachezaji 23 ambao wameunda timu ya misitu iliyoko chini ya wakala wa huduma za misitu Tanzania (TFS) Shamba la miti Sao Hill.

Aidha lengo kuu ni kurudisha shukrani kwa jamii inayozungukwa na shamba yaan (Corporate Social Responsibility) na kupitia michezo hii kunawasaidia vijana kujipatia ajira, kuvumbua vipaji vyao na kuviendeleza sanjari na kulitangaza shamba.

Shamba hili lilianzishwa mwaka 1939, na ndilo kubwa kati ya mashamba 23 ya taifa lina ukubwa wa hekta 135, 903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya upandaji miti na hifadhi ya mazingira, kati ya eneo hilo kiasi cha hekta 86,003 ni kwa ajili ya upandaji miti kibiashara, hekta 48,200 kwa ajili ya utunzaji  wa mazingira na vyanzo vya maji pamoja na ufugaji wa nyuki na hekta 1,700 ni kwa ajili ya makazi na uwekezaji, aidha shamba hili huchangia sana katika Pato la Taifa.

HABARI PICHA


Sao Hill Forest FC

Juhudi FC
Sao Hill Forest FC Wakiwa katika Picha ya Pamoja na Juhudi FC Katika mechi ya Kirafiki Uwanja wa Kinesi

Wachezaji wa akiba


Barnaba Mlomo

Emmanuel Ernest

Hashim Bakari
Frank Ndola



Godfrey
Pan Sanga



James Chogela

Jonhson Mkushi
Nesto Simon
Steven
Wilson Kangusi



Stanley Kadege

Daniel Kibiki (Kinyambe)
Robert Mgindo
Said Aboubakar



Casto Jerry

Merick Mbembe

Kocha Mkuu  Sao Hill Forest FC Bakari Khasim (Kushoto) akibadilishana machache na Kocha Msaidizi Khalid Nguchuke wakati wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Juhudi FC katika Uwanja wa Kinesi Ubungo Dar es salaam.



Wachezaji wakifanya mazoezi (Warm Up)






Kocha Mkuu Sao Hill Forest Fc Bakari Khasim akitoa maelekezo kwa wachezaji












Baadhi ya washabiki wakifuatilia kwa makini mtanange mkali wa Juhudi FC Vs SaoHill Forest Fc Katika Uwanja wa Kinesi Ubungo Dsm (Picha zote na Amani Mbwaga)

No comments:

Post a Comment