Sunday, September 30, 2018

Naibu Waziri Maliasili na Utalii Mhe Hasunga Kuunda Tume ya Kuchunguza Chanzo cha Moto Ulioteketeza Takribani Hekta 400 za Miti SaoHill.

Na Amani Mbwaga, Mafinga- Iringa
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Japhet Hasunga wa kwanza kulia
Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhe Japhet Hasunga ametoa tamko la kuundwa kwa tume ya kuchunguza chanzo cha matukio ya moto ambayo yametokea kwa muda wa siku nne mfululizo  kuanzia tarehe 25 Septemba hadi 28 Septemba 2018 katika Shamba la Miti Saohill na kuteketeza karibia hekta 400 za  miti katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

“Nitahakikisha tume inaundwa haraka sana  ambayo itafanya kazi kwa muda wa mwezi mmoja, itupe majibu, ifanye uchunguzi wa kina ijue ni kwa nini matukio haya yanatokea kipindi hiki, ni lazima turudi kwenye mstari na tufanye kazi kwa mujibu sheria, kanunni na taratibu na viongozi wote lazima tukabiliane na janga hili” alisema Mhe Hasunga.

Tukio la moto la kwanza lilitokea mnamo tarehe 25 Septemba 2018 katika eneo la “Majinja”eneo ambalo halijapandwa miti na ambalo bado lipo kwenye mgogoro wa umiliki na JKT Mafinga.

Mnamo tarehe 26 Septemba 2018 majira ya saa nane mchana moto ulizuka tena katika eneo la sao hill safu ya pili, jitihada za kuuzima zilifanyika na kufanikiwa kuuzima sanjari na uwepo wa upepo mkali, jumla ya viunga (Compartments) 11 ziliungua zenye ukubwa wa hekta 347.314.

Aidha Kijiko (Grader) kimoja ambacho kilitumika katika kutengeneza barabara ya kuzuia moto usiruke katika jitihada za kukabiliana na moto huo kilipata hitilafu ya kiufundi na kushindwa kutembea na hivyo kupitiwa na moto lakini yameungua tu matairi na baadhi ya paipu tu za kijiko.
Tarehe 27 Septemba 2018 moto tena ulitokea majira ya saa tatu usiku katika safu ya matanana na kuunguza takribani hekta 5.9.

Hata hivyo tarehe 28 Septemba moto mwingine ulitokea katika safu ya Ngwazi kutokana na shughuli za usafi katika maeneo ya makazi ya watumisha wa Taasisi ya utafiti wa chai na kupelekea kuunguza jumla ya hekta 28 yenye miti ya kupandwa.

Kwa Mujibu wa Taarifa ya Meneja Mkuu wa Shamba la Sao Hill inaeleza kwamba Ukitoa tukio la moto ulioanza kwenye makazi ya watumishi wa Taasisi ya utafiti wa chai kule Ngwazi mpaka sasa chanzo kamili cha moto katika matukio mengine manne hakijafahamika.

Lakini kuna taarifa zinaeleza kuwa katika safu ya Sao Hill Kikosi cha doria kiliona nyayo za mtu zilizotokea maeneo ya Makalala (Mto Ruaha) na kuingia shambani na kutoka katika eneo ambalo moto ulikuwa unawaka na kushindwa kumkamata.

Taarifa za Kiintelejesia zianaeleza kuwa matukio haya ya moto yamepangwa (Hujuma) na baadhi ya vibarua wanaofanya kazi katika shamba la Sao Hill hii ni kutokana na kukosa mishahara yao ya kuanzia mwezi wa saba mwaka huu 2018. 
  
Aidha Mhe Hasunga ametoa maelekezo kwa uongozi wa shamba la Miti Sao Hill ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya kina kujua hasara iliyopatikana, ameagiza Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) kuongeza vifaa vya kupambana na kuzima moto, na pia katika maeneo yote yaliyoungua kuongeza juhudi za kupanda miti.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William baada ya kuona matukio hayo kuzidi ndani ya Wilaya ya Mufindi na kufuatia kuwa na hali ya upepo ametoa tamko la kusimamisha shughuli zote za maandalizi ya Mashamba kwa kutumia moto.

“Kutokana na upepo mkali unaovuma hivi sasa katika Wilaya yetu na kusababisha hatari ya moto katika misitu ya hifadhi na ya jamii nasitisha maandalizi ya mashamba kwa kutumia moto na pia uchomaji wazi wa taka kwa muda wa siku saba kuanzia leo taehe 30 Septemba 2018 hadi tarehe 7 Oktoba 2018 baada ya hapo wananchi wanaweza kuandaa mashamba yao kwa tahadhari na kwa kuzingatia sheria zilizowekwa na vijiji na Halmashauri” alisema Mhe William

Nae Meneja mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Heribert Haule alieleza malengo makuu ya kuanzishwa kwa hifadhi ya shamba hilo ikiwa ni pamoja na kuwa chanzo cha mapato serikalini, kupunguza utegemezi wa misitu ya asili, kutoa ajira, kuhifadhi ardhi na vyanzo vya maji, kutoa malighafi kwa ajili ya viwanda vinavyozalisha karatasi, mbao, nguzo za umeme na viberiti na pia kuboresha mazingira na mandhari ili kuwa na mazingira ya kuvutia.

“Uwekezaji Katika shamba la Sao Hill uelenga katika upandaji mkubwa wa miti ili kuhakikisha upatikanaji endelevu wa mazao ya misitu kwa kizazi cha sasa na vizazi vijavyo” alisema Bwana Haule.

Shamba la Miti Sao Hill ni la kwanza kwa ukubwa kati ya mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya Taifa, shamba hili lina ukubwa wa hekta Zaidi ya laki 135 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya upandaji miti na hifadhi ya mazingira na lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi 1951 na upandaji wa kiwango kikubwa ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980.

HABARI PICHA
Naibu Waziriwa Maliasili na Utalii Mhe Japhet Hasunga akipokelewa na Mkuu wa Wilaya Mufindi
Naibu Waziri Mhe Hasunga akisalimiana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mufindi Bwana Allan Mwala






Naibu Waziri Mhe Hasunga akisaini Kitabu cha Wageni


Baadhi ya Watumishi wa Shambala Misitu Sao Hill

Meneja Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Heribert Haule akisoma taarifa ya Shamba la Sao Hill



Naibu Waziri Mhe Hasunga akitembelea eneo la kwanza la  chanzo cha moto uliounguza baadhi ya Miti Katika Shamba la Sao Hill

Naibu Waziri Mhe Hasunga akisalimiana na Mzee Mosha mmoja wa wadau wa Wavunaji wa miti katika shamba la miti Sao Hill









Baadhi ya Miti iliyoungua kutokana na uchomaji hovyo wa moto


Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William akionesha shamba lingine lililoathirika na moto










Baadhi ya Watumishi wa Shamba la Misitu Sao Hill



Wadau wa uvunaji wa misitu Sao Hill



Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Japhet Hasunga akitoan Maelekezo kwa Watumishi wa shamba la Sao Hill

Picha zote na AmaniMbwaga
Kwa Maoni au Ushauri Wasiliana nasi:
Mob:+255 656 632 566
E-mail:prof.mbwaga@gmail.com

Saturday, September 29, 2018

RC HAPI AHITIMISHA ZIARA YA IRINGA MPYA

Na Amani Mbwaga, Iringa. "Leo nimehitimisha ziara ya Iringa mpya.Nimetembelea tarafa zote15 na kusafiri umbali wa KM 3345. Nimefanya mikutano mikubwa 20,midogo 65,kusikiliza kero mbalimbali 849 za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo yenye thamani ya Sh bilioni 78.1.Asanteni sana wana Iringa,Nitarudi" RC Hapi

HABARI PICHA