Tuesday, September 18, 2018

DC Mufindi akagua Marekebisho ya Barabara ya Changarawe - Matanana

Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William akiongea na Wananchi wa Changarawe
 Na Amani Mbwaga, Mafinga.
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William leo amekagua barabara ya Changarawe hadi Matanana iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe ikiwa ni kutekeleza agizo la kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa mwaka 2018 Ndugu Charles Kabeho alipolitoa Mei 27, 2018 baada ya kukataaa kuizindua kutokana na kuwa chini ya kiwango.
Akiambatana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mufindi Mhe William amekagua na kujiridhisha kwa baadhi ya marekebisho yaliyofanywa na mkandarasi na kisha kuweka jiwe la msingi la kukagua barabara hiyo.
“Nieleze tu masikitiko yangu kwamba wakati kiongozi wa mbio za  mwenge 2018 anakuja hapa mwezi mei mwaka huu barabara yetu haikufikia vigezo vilivyoweka, hivyo haikuzinduliwa, na maelekezo yake yalikuwa ni kufanya marekebidho kasha kukaguliwa na nikishakagua nimpelekee taarifa  na leo hii nimepata fursa ya kukagua alisema Mhe William
Kabla ya kukagua Mhe William aliagiza wataalamu wake kupiti barabara yote KM 15 kupima na   kubainisha maeneo ambayo hayakukidhi vigezo na kisha  kuyafanyia marekebsho ili kukikidhi vigezo vilivyowekwa kwa mujibu wa mkataba ili fedha ya serikali iliyotumika thamani na ubora uonekane.
Katika taarifa yao takribani maeneo 300 yalipitiwa na wataalamu na  mengi hayakukidhi vigezo kwa utaratibu huo mkandarasi aliagizwa kufanya marekebisho.
Aidha Mhe William amemwagiza Injinia wa TARULA kupita tena kwa mara nyingine ili kujiridhisha zaidi na pia ametaka kufahamu kiwangao cha changarawe kilichotumika baada ya marekebisho hayo kutokea
Ametoa rai kwa TARULA kupitia barabara zote za mji wa Mafinga ili kufanya usanifu upya ili kuleta sura ya mji ili ikifika wakati serikali imepata fedha kwa ajili ya kujenga lami kwenye barabara hizo basi isianze tena kuweka X kwenye nyumba za watu.
Barabara ya Changarawe Matanana ina urefu wa KM 37.67 ambayo yote ni ya udongo.
Katika mwaka wa fedha 2017/2018 serikali kupitia wakala wa barabara vijijini TARULA Mafinga Mji imefanya matengenezo makubwa ya barabara na upandisha hadhi KM 15 za barabara kuwa ya Changarawe.
Matengenezo yalianza tarehe 26 April 2018 na yalitarajiwa kukamulika tarehe 15 Septemba 2018
Barabara hii inaunganisha kata 03 yaani changarawe, SaoHill, na Bumilayinga zinazokadiriwa kuwa na zaidi ya watu laki mbili na pia inaunganisha kata hizo na barabara kuu ya TANZAM yaani Iringa-Mbeya.
Barabara hiyo inapita katika maeneo makubwa ya uzalishaji mali na biashara ikiwemo skimu ya umwagiliaji ya Mtula.
Mradi huo unakisiwa kugharamia zaidi ya Tsh Milioni 331 kutoka katika mfuko wa barabara (Road Fund)
Kwa mujibu wa Meneja TARULA Mafinga Injinia Patrick Kabadi anabainisha kwamba matengenezo ya barabara hiyo yalifanywa na Mkandarasi aitwae GILCO na Mpaka sasa amelipwa takribani Tsh Milioni 258.
Meneja wa TARULA aliongeza kwamba lengo la marekebisho ya barabara hiyo ni kurahisiha shughuli za usafirishaji ili kuiwezesha jamii kupata huduma za kijamii na kiuchumi kwa haraka zaidi.

HABARI PICHA


Uhakiki wa Vipimo na Ubora Ukiendelea 


Mkuu wa Wilaya Mufindi akimuonesha Mmoja wa Wananchi BOQ Inayoonesha Viwango vya ubora na vipimo vinavyotakiwa katika Barabara ya Changarawe - Matatnana Km 15




Katibu Tawala (DAS) Mufindi Bwana Allan Benard Mwalla akishuhudia uhakiki wa marekebisho ya barabara kwa Vipimo

Kamati ya Ulinzi naUsalama ikiwa na Wananchi wa Changarawe wakishuhudia Uhakikiki wa vipimo vya barabara  mara baada ya kurekebishwa na Mkandarasi



DC Mufindi  Jamhuri William (Kushoto) akihakiki vipimo

Barabara ya Changarawe - Matanana


Kaimu Meneja TARULA Mafinga Injinia Patrick Kabadi akisoma taarifa ya utekelezaji wa Marekebisho ya Barabara ya Changarawe - Matanana




DC Mufindi akiweka Jiwe la Ukaguzi wa Barabara











DC William akiongea na Wananchi wa Changarawe baada ya Kuweka Jiwe la Ukaguzi katika Barabara ya Changarawe - Matanana (Picha zote na Amani Mbwaga)

No comments:

Post a Comment