|
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Salum Hapi Akihutubia Mamiaya Wananchi wa Mapanda Katika Viwanja vya Shule ya Sekondari Kihansi ikiwa ni Siku ya Nne Ndani ya Ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa ya IRINGAMPYA |
Na Amani Mbwaga, Mufindi
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi ameapa kutowafumbia macho watendaji wa serikali watakaoshindwa kuendana na kasi ya Rais Mgufuli na ile ya Iringa mpya na kuwanguza watendaji wote wa serikali ambao ni mizigo.
Ameyasema hayo leo wakati akihutubia mamia ya wananchi wa Mufindi katika viwanja vya Shule ya Sekondari Kihansi iliyoko kata ya Mapanda Tarafa ya Kibengu Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa
Mhe Hapi amewataka watumishi kutekeleza maagizo anayoyatoa kwa wakati muafaka na kutimiza majukumu yao kwa kufuata taaluma zao, misingi, sheria na taratibu za nchi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya uchumi wa Taifa na kusikiliza kero za wananchi wakati wote.
"Haiwezekani Rais anazunguka nchi nzima kusikiliza kero kwa wananchi halafu wewe mtu mdogo tu unashindwa kuwasikiliza haiwezekani, na wote mnaokula mishahara ya bure bila kufanya kazi mtaitapika hakuna mambo ya kula mshahara wa bure hapa " alisema Mhe Hapi.
Aidha amewasisitiza Wakurugenzi wote wa Halmashauri kuhakikisha wanakuwa na ripoti za utendaji kazi kwa watumishi wote wa umma kila wiki ripoti ya mtumishi ieleze kwa kila siku amefanya shughuli gani na pia wiki ijayo anatarajia kufanya nini.
Katika ziara yake ya leo katika tarafa ya KibenguMkuu wa Mkoa amezindua rasmi mradi wa ujenzi wa nyumba 6x1za Waalimu katika shule ya sekondari Ilogombe, amekagua ujenzi wa bweni la Wanafunzi na miundombinu shule ya Sekondari Kahansi
|
RC Ally Hapi akipokelewa na Mkuuwa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William katika Shule ya Sekondari Ilogombe |
|
RC Hapi akitoa Maelekezo kwa Wasimamiziwa Miradi ya Serikali kuhakikisha wanasimamia Ubora na Thamani ya pesa ionekane kwenye Miradi inayotekelezwa |
|
RC Iringa Mhe Ally Hapi akizindua Jengo la Nyumba za Waalimu 6 x1 Katika Shule ya Sekondari Ilogombe |
|
Wananchi wa Kijiji cha Ilogombe Wakishangilia Uzinduzi wa Nyumba za Waalimu zilizozinduliwa na Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi |
|
RC Ally Hapi Ally Hapi Baada ya Kukagua Mradi wa Ujenzi wa Bweni la Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kihansi utakaogharimu kiasi cha fedha Milioni 98 na Kubeba Wanafunzi 80 |
|
Viongozi wa Jadi wa Kata ya Mapanda Wakimshangilia Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi |
|
Baadhi ya Wananchi waliojitokeza Kumsikiliza Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi katika Kijiji cha Mapanda |
|
Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe Jamhuri David William Akiwasalimia Wananchi wa Mapanda |
|
Diwani Obadia Kalenda wa Kata ya Mapanda akiwasalimia Wananchi wake |
No comments:
Post a Comment