Friday, September 7, 2018

Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi Kuzindua Kampeni ya Iringa Mpya Mufindi.


Maandalizi ya Uzinduzi wa Kampeni ya Iringa Mpya yamepamba moto leo jioni jukwa hili likielekea kukamilika
Na Amani Mbwaga Mafinga
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Salum Hapi anataraji kufanya ziara ya kikazi katika Wilaya ya Mufindi na Halmashauri zake kuzunguka Tarafa zote kati ya tarehe 08 Septemba hadi tarehe 13 Septemba 2018.

Katika ziara hiyo Mhe Hapi atazindua rasmi maadhimisho ya mikutano ya kampeni ya “IRINGA MPYA” kwa wananchi wa Mkoa wa Iringa, maadhimisho hayo yatafanyika kesho Tarehe 08 Septemba 2018 siku ya Jumamosi katika viwanja vyaCOTC vilivyopo karibu na Hospitali kuu ya Mafinga Mjini Kuanzia Saa 2:30 asubuhi.

Madhimisho hayo yataambatana na Maonesho ya Wajasiriamali, Uzinduzi wa kampeni ya upimaji VVU na saratani kwa watu wote hasa wanaume, kupokea maandamano ya kikundi cha hamasa cha usafi wa mazingira, burudani mbalimbali za wasanii ikiwemo muziki wa Live band kutoka JKT Mafinga.

Aidha Mkuu wa Mkoa atatumia fursa hii ya uzinduzi kusikiliza kero za wananchi na kuzitolea majibu, yaani Mahakama ya Wananchi.

Baada ya uzinduzi Mkuu wa Mkoa ataanza ziara yake ya tarafa kwa tarafa kukagua, kuzindua na kufungua miradi ya maendeleo kufanya mikutano ya hadhara na kusikiliza kero za wananchi ambapo tarehe 9 Septemba atakuwa Tarafa ya Kasanga, tarehe 10 Tarafa ya Malangali, Tarehe 11 Tarafa ya Kibengu, Tarehe 12 Tarafa ya Sadani na Tarehe 13 Tarafa ya Ifwagi.

Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William anawaomba wananchi wote, wafanyakazi, wakulima, wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huu wa “IRINGA MPYA” Ili kupokea na kutekeleza dhana ya ujenzi wa Iringa Mpya kwa vitendo.
























No comments:

Post a Comment