Na Amani Mbwaga, Mufindi
Mkuu wa Wilaya
Mufindi Mhe Jamhuri David William ameyasema hayo jana Jumapili kwenye ibada na
Waumini wa dini ya kikristo katika Kanisa la EAGT Jerusalemu Tempo liliopo
Mafinga Mjini baada ya kupata mwaliko kwa ajili ya kuwatembelea wananchi wake
na kuona maendeleo ya Ujenzi wa Kanisa.
“Ninashukuru sana
Kuja kuwasalimia Wakristo wenzangu Mlinipokea na familia yangu viuri sana toka
nahamia Wilaya hii mpaka sasa tumekuwa wenyeji, nawaomba sana muendelee
kudumisha Amani iliyopo katika Mji wetu wa Mafinga na Taifa kwa ujumla” alisema
Mhe William
Aidha ameliomba
kanisa kuendelea kuwaombea viongozi wote wa serikali kuanzia Rais Dkt John
Pombe Magufuli na Wasaidizi wake ili waliongoze vyema Taifa na kuwaletea
maendeleo watanzania kwa lengo la kufikia Tanzania tunayoitaka.
“Mimi kila wakati
ninapoona kanisa limefurika namna hii huwa ninafarijika sana kwa sababu ninajua
uimara wa kanisa ndio usalama wa Wilaya yetu na Taifa kwa ujumla” Mhe
William.
Amewaomba Waumini
kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano ili iendelee kuwaletea
maendeleo katika shughuli mbalimbali ikiwemo kampeni za Usafi wa Mazingira,
chanjo, ulinzi na usalama katika mitaa na mengine mengi.
Ametoa wito kwa
wageni wanaohamia Mafinga mjini na Wilaya ya Mufindi Kwa Ujumla wawe makini na
janga la ukimwi kwani Mkoa wa Iringa unashika nafasi ya pili kitaifa kwa
maambukizi ikiwa na asilimia 11.2 ikiongozwa na Mkoa wa Njombe hivyo wanatakiwa
kuchukua tahadhari na asingependa kuona mgeni anakuja hapa mzima haafu anarudi
kwao anumwa.
Wakati huo huo Mhe
William Amechangia Mifuko 10 ya sementi kwa ajili ya shughuli za ujenzi wa
kanisa la kisasa unaoendelea kanisani hapo na kuwaahidi kushirikiana nao katika
kuwapatia fursa za ujasiriamali kinamama wa kanisa hilo wanaojishughulisha na
ujasiriamali katika shuguli mbalimbali za kuwaletea maendeleo.
Kwa upande wake
Mchungaji Wailes Howa wa kanisa hilo la EAGT Jerusalemu Tempo Mafinga Mjini
amemkaribisha mkuu wa Wilaya na kumuomba aendelee kushirikiana na kanisa kwa
maendeleo ya Taifa.
Mchungaji Howa amesema
tunapokuwa na viongozi wanaomcha mungu huwa tunabarikiwaasana cha msingi ni mtu
kuwa uhusiano na mungu na ndilo ambalo linabariki mioyo ya watu.
Mimi ni miongoni mwa
Wapenzi au Washabiki wa Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli nimempenda sana hasa
katika utendaji wake wa kazi na kanisa ni shahidi huwa ninamzungumza sana hapa
kanisani, tulikuwa tuanahitaji watu wa namna hii ambao wanaweza kututoa sehemu
moja kwenda nyingine.
Si kwamba wengine
waliopita hawakufanya chochote hapana kila mmoja ana cha kwake alichokifanya
anaamini atakaekuja mwingine nae atatutoa mahali tuulipo na kutupeleka kwingine
na anaaamini Mungu atatengeneza wepesi na kutuletea mtu ambae atatutoa hapana
kutufikisha sehemu nyingine.
Katika Ibada hiyo Mchungaji
Howa alimpatia zawadi ya Biblia Mhe Mkuu wa Wilaya pia Umoja wa Wanawake wa
Kanisa hilo walimpatia zawadi mke wake
ikiwa ni moja ya kuonesha upendo mkubwa walionao kwa Mkuu huyo ambae anaiongoza
wilaya ya Mufindi vyema na hasa kwa kuzingatia sheria taratibu, kanuni na hofu
ya mungu.
No comments:
Post a Comment