Na Amani Mbwaga,
Mafinga.
Waziri wa Wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Isaack Kamwelwe |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaack Kamlwelwe anataraji kupeleka bungeni mswaada wa sheria ya Mabasi kuendeshwa na Madereva wasio chini ya umri wa miaka 45 na kuendelea ili
kupunguza ajali nyingi zinazotokea na kupoteza maisha ya watanzania.
Ameyasema hayo leo wakati
wa ziara yake ya kukagua maendeleo ya matengenezo ya barabara ya lami ya
Mafinga hadi Igawa ambayo imekamilika kwa takribani asiimia 98 kwa kipande cha
Mafinga –Nyigo na kuridhishwa na hatua hiyo iliyofikiwa, na kusisitiza mambo
madogomadogo yaliyobakia yakamilke kwa wakati na ndani ya mkataba ikiwemo
uwekaji wa alama za barabarani na kupaka rangi.
Lakini imegundulika kuwa
kuna eneo karibu na barabara kuna mmomonyoko mkubwa wa udongo lakini tayari
TANROADS wanalifanyia kazi na usanifu unaendelea kwa ajili ya utekelezaji.
“Lakini nisikitike
sana mara baada ya barabara kukamiika ajali zimeanza kuongezeka na nimeambiwa
kwamba ajali nyingi zinatokana na magari yanayobeba mafuta madereva mnajisahau
sana barabara imekuwa nzuri mnapiga spidi zote tu, hapana ni lazima tuweke
sheria kali, ndugu zangu tutembee taratibu kwa sababu tunakokwenda tutafika tu”
alisema Mhe Kamwelwe.
Mhe Waziri ameleza
kuwa miundo mbinu hiyo imeimarika ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya chama tawala
chama cha Mapinduzi waliahidi na wanatekeleza aidha utekeelezaji huo umefikiwa
kwa sababu watu wamekubali kulipa kodi, Mhe Rais Dkt John Pombe Magufuli
amesimama imara kuhakikisha kodi inarudi kwa wananchi ili waitumie ipasavyo.
“Uboreshaji mzuri wa
barabara usigeuke kuwa vilio vya familia nasisitiza tutembee taratibu,
baada ya kuona ajali zinakuwa nyingi mimi nitaomba wabunge mnikubalie inabidi
tupeleke mswaada wa sheria bungeni dereva anae endesha basi ya abiria asiwe
chini ya miaka 45 hatuna namna nyingine maana hatutaki kuona tunaendelea kuuwa
ndugu zetu watanzania kwa sababu ya mtu
kuendesha gari akiwa na umri ambao haujafika miaka 45 na sisemi ndio nimeagiza
sas hivi, hapana napeleka mswaada wa sheria bungeni ili tuupitishe” alisema Mhe Waziri.
Hilo limekuja baada
ya kufanya utafiti kutoka kwa Mhandisi Mshauri aliyekuwa akitafiti vyanzo vya
ajali nyingi barabarani na kugundua kuwa kwa sehemu kubwa ajali nyingi zinasababishwa
na Binadamu (Human Error) sasa ni lazima kuweka sheria mbalimbali ii kupunguza
na kuondoa kabisa ajali.
Aidha Mhe Waziri
alianza ziara yake iringa mjini na kukagua maendeeo ya marekebisho ya uwanja wa
ndege iringa ambapo upo katika hatua za mwisho kukamilika na tayari kwa kuanza kutumika.
HABARI PICHA
Barabara ya Mafinga - Igawa |
Waziri waUjenzi Mhandisi Kamwelwe Kushoto akitata jambo na Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William (kulia) |
Waziri wa Ujenzi Mhandisi Kamwelwe akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga |
Waziri wa Ujenzi Mhandisi Kamwelwe Akisalimiana na Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi |
Eneo lenye mmomonyoka wa udongo linaloelekea kuhatarisha usalama wa barabara liko kama mita 30 |
Waziri Kamwelwe akisalimiana na Mbunge wa Mufindi Mhe Menrad Kigola |
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Kamwelwe akiagana na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi ndugu Yassin |
Picha ya Pamoja Picha zote na Amani Mbwaga |
No comments:
Post a Comment