Thursday, November 15, 2018

TFS Saohill Yatembelewa na Wahasibu wa Kanda

Wahasibu Tfs Kanda  na Watumishi wa Shamba Sao Hill Wakifurahia Asali
Kwa Hisani ya Afisa Habari TFS - Sao Hill
Shamba la Miti Saohill Chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS mapema wiki hii imetembelewa na Wahasibu kutoka katika ofisi mbalimbali za Kanda (TFS) kwa lengo la kukagua, kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba la miti Sao Hill.

Wahasibu hao wamejifunza jinsi shamba linavyofaya kazi ikiwa ni pamoja na kufahamu changamoto za kila siku katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali kama vile ukusanyaji wa mapato na kuona namna malipo yanavyofanyika. 

Ugeni huo umetembelea maeneo mbalimbali ya shamba ikiwemo sehemu ya kuchakatia asali, Manzuki, bustani ya miti, (Miche) minara ya mawasiliano ya moto kuangalia zoezi la uvunaji wa miti na majaribio yanayoendelea ya uvunaji wa utomvu kutoka kwenye miti na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii ndani ya shamba.

Shamba la miti Sao Hill ni la kwanza kwa ukubwa kati ya mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya Taifa. Kwa sehemu kubwa Shamba hili lipo katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na eneo dogo lipo katika mkoa wa Morogoro.

Shamba hili lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi 1951 na upandaji kwa kiwango kikubwa ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980
                        HABARI PICHA
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herberth Haule aliyesimama akiongea na Wahasibu kutoka Kanda mabalimbali za TFS a baadhi ya watumishi wa Shamba hilo katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya shamba Sao Hill










Meneja Tarafa ya kwanza  Irundi Bi Glory (aliyenyoosha mkono)  akionesha wageni  jinsi shamba linavyoonekana  katika moja ya mnara wa asili wa Mawasiliano (Watch Tower) kwa ajili ya ulinzi wa msitu endapo utavamiwa na moto sehemu yoyote ili ili kuchukua hatua yankudhibiti mapema 



Baadhi ya Mizinga ya Nyuki






Mmoja wa Wageni akichuguza kwa makini (Packaging)ya Asali ya Saohill



Mmoja wa Wa wageni akionja Asali tamu ya Saohill

Wahasibu wakiwa katika chumba cha kuchakatia Asali  ambapo wamepata maelezo kuhusu zoezi zima la uchakataji

Wageni mbalimbali na Watumishi  wa Shamba la Miti SaoHilll wakiongozwa na Afisa Nyuki wa Shamba hilo Bwana Said Aboubakar  wa kwanza kushoto waliochuchumaa wakifurahia Asali ya Saohill Honey yenye ubora wa kiwango cha juu (Picha zote na Afisa Habari TFS Sao Hill Mwanaisha Luhaga)

No comments:

Post a Comment