Na Amani Mbwaga,
Mafinga.
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Salum Hapi leo amepata fursa ya kutembelea na Kuwasha mradi wa umeme wa REA awamu ya III Mzunguko wa Kwanza katika mtaa wa Ndolezi ulipo Halmashauri ya Mji Mafinga wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa
Mradi huo ulioanza kutekelezwa tarehe 3 Julai 2017 na kampuni ya M/S Sengerema Engineering Group Ltd wenye gharama ya jumla ya Tsh Bilioni 24.7 chini ya Usimamizi wa Shirika la Umeme Tanzania TANESCO.
“Umeme ni nyenzo
muhimu sana kwa wananchi wetu hasa vijijini, Serikalli ya awamu ya tano inayoongozwa
na Rais Dkt John Pombe Magufuli kupitia ilani ya chama acha mapinduzi
tumedhamiria kuhakikisha vijiji vyote kwenye nchi yetu vinapata umeme wa uhakika”
alisema Mhe Hapi.
Aidha Mhe Hapi
ameamua mwenyewe kuanza kufuatilia miradi ya REA ili kujiridhisha kama kasi ya
upelekaji umeme vijijini inaridhisha na alisema “Nataka niwahakikishie kuwa
hakuna kijiji hata kimoja kwenye mkoa wetu ambacho kitabaki bila kupata umeme
hiyo ni ahadi ya Mhe Rais na mimi kama muu wenu wa mkoa tutaendeleakufuatilia
kuhakikisha wananchi wetu wote wanapata umeme katika vijiji vyote.”
Mhe. Hapi
amesisitiza kuhakikisha umeme unapokwenda vijijini ni lazima kutoa kipaumbele
cha ugawaji wa umeme katika maeneo muhimu kwanza ya zahanati, visima vya maji, na
shuleni.
Jumla ya wateja 2596
wanategemewa kuunganishwa na umeme kati yao 2333 ni wa njia moja na 263 ni wa
njia tatu na mpaka kufikia tarehe ya leo jumla ya vijiji 18 vimeungwa umeme na
Transfoma 18 zimefungwa katika maeneo mbalimbali ya mradi.
Mkuu wa Wilaya
Mufindi Mhe Jamhuri William akitoa salamu za wilaya kwa mkuu wa mkoa alisema
kupitia mradi wa umeme vijijini REA, Wananchi
wa Ndolezi walikua na shida sana ya umeme na walipiga kelele sana lakini
aliwambia umeme utafika tu na sasa uefika.
“Kwa kupitia
juhudi za Mbunge wa Mafinga mjini Mhe Cosato Chumi alipiga kelele sana bungeni
lakini aliwasumbua sana TANESCO na hatimae leo umeme umewashwa rasm”
alisema Mhe. William.
Kwa Upande wake
Mwenyekiti wa bodi ya Shirika la umeme Tanzania TANESCO Profesa Alexander
Kyaruzi ameipongeza serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John
Pombe Magufuli kwani amedhamiria kulitoa Taifa hili kwenye hali lilipo na
kulipeleka kwenye uchumi wa kati ambao utaendana na Tanzania ya viwanda.
Lakini huwezi kwenda
katika uchumu wa kati wakati watu wako gizani, kwa hiyo rais ametoa fedha
nyingi sana kupitia REA ili kupata umeme wa uhakika vijijini.
“Iringa kwa awamu hii
takribani vijiji 179 vitapata umeme na ikija awamu ya III Mzunguko wa pili kila
Mtanzania atapata umeme na hili Mhe Rais amedhamiria haswaa ifikapo 2021 kila
Mtanzania awe na umeme na kwa mujibu wa takwimu zilizopo kwa sasa asilimia
takribani 67.5 umeme umewafikia wananchi kote nchini”
alisema Profesa Kyaruzi.
Akisoma taarifa ya
utekelezaji wa mradi wa umeme kwa Mkuu wa Mkoa Iringa Meneja TANESCO Wilaya ya Mufindi
Mhandisi Omary Ally amesema Jumla ya wateja 616 wamelipia kuunganishiwa umeme
kati yao 263 wameunganishwa na 353 bado hawajaunganishwa kutokana na ukosefu wa
Mita kutoka kwa mkandarasi.
Aidha kwa mujibu wa Mkandarasi wa REA Kampuni ya M/S Sengerema Engineering Group Ltd inyotekeleza mradi huu kupitia kwa Mhandisi Bryson Chegula amemthibitishia Mkuu wa Mkoa na wananchi wa Ndolezi na Mafinga kwa ujumla kuwa zaidi ya Mita 1000 za umeme zinainga siku ya Jumapili hali itakayochochea uunganishwaji wa wateja wengi wa umeme na hatimae kuondokana na changamoto yakukosa umeme.
Aidha kwa mujibu wa Mkandarasi wa REA Kampuni ya M/S Sengerema Engineering Group Ltd inyotekeleza mradi huu kupitia kwa Mhandisi Bryson Chegula amemthibitishia Mkuu wa Mkoa na wananchi wa Ndolezi na Mafinga kwa ujumla kuwa zaidi ya Mita 1000 za umeme zinainga siku ya Jumapili hali itakayochochea uunganishwaji wa wateja wengi wa umeme na hatimae kuondokana na changamoto yakukosa umeme.
“Wilaya ina jumla ya
vijiji/mitaa 161 na vitongoji 562 kati ya hivyo vijiji/mitaa 95 vimeshapata
umeme REA I&II na vijiji 54 vipo kwenye REA awamu ya III Mzunguko wa kwanza
katika utekelezaji” alisema Mhandisi Omary.
Kukamilika kwa miradi
ya umeme awamu ya kwanza, ya pili na ya tatu itachochea kwa kiasi kikubwa
maendeleo ya viwanda vidogo vijijini na kuongeza wigo mkubwa kwa wananchi wa
Mufindi waliofikiwa na huduma ya umeme hatimae kukua kwa uchumi na hatimae kuongeza pato la Taifa.
HABARI PICHA
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Ally Hapi akiongea na wananchi wa mtaa wa Ndolezi kabla ya kuwasha umeme |
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri Davidi William akitoa salamu za Wilaya |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga akitoa neno la Shukrani |
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania Profesa Alexander Kyaruzi akitoa salamu za TANESCO Makao Makuu |
Meneja wa TANESCO Wilaya ya Mufindi Mhandisi Omary Ally akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Umeme kwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Ally Saul Hapi |
Wananchi wa Mtaa wa Ndolezi Mjini Mafinga Wakifurahia kuwashwa kwa umeme katika mtaa wao na kuipongeza serikal kupitia TANESCO kwa kuwafikishia huduma hiyo muhimu kwa maendeleo ya Uchumi wa Taifa |
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Hapi akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Umeme Tanzania Prof. Kyaruzi |
Baadhi ya watumishi wa serikali ikiwemo kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya mufindi wakifuatilia kwa karibu zoezi la uwashwaji wa umeme katika mtaa wa Ndolezi Mjini Mafinga |
Mkuu waMkoa Iringa Mhe Hapi Akiongea na Wananchi wa Mtaa wa Ndolezi |
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Hapi (Kulia ) akimkabidhi Kisemeo Meneja TANESCO Mufindi Mhandisi Omar Ally Kujibu hoja za wananchi mbalimbali kabla ya kuzindua uwashaji wa umeme katika mtaa wa Ndolezi. |
Wananchi wa Mtaa wa Ndolezi wakimsikiiza kwa makini Meneja TANESCO Wilaya ya Mufindi Mhandisi Omary Ally |
Mmoja wa Wafanyakazi wa TANESCO akisubilia kwa hamu kuzinduliwa rasmi kwa uwashaji wa Umeme katika Mtaa wa Ndolezi |
Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Hapi akipata ufafanuzi wa suala la Mita kutoka kwa Mkandarasi wa REA M/S Sengerema Engineering Group LTD Mhandisi Bryson Chengula |
Tayari kwa umeme Kuwashwa Rasmi Mtaa wa Ndolezi |
Taa imewashwa rasmi na Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Hapi kuashiria uwashaji wa umeme Katika Mtaa wa Ndolezi |
No comments:
Post a Comment