Na Amani Mbwaga.
Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu amewasha umeme katika kijiji cha Ikongosi na Kufanya
ziara ya kutembelea chanzo cha Umeme kutoka kwa Mzalishaji binafsi MWENGA HDRO
POWER Chini ya Kampuni tanzu ya RIFT VALLEY ENERGY iliyopo wilayani Mufindi
Mkoani Iringa.
“Nimefurahi kufika
Mwenga hapa na nadhani ni mradi wangu wa kwanza kufika katika mradi kama huu wa
sekta binafsi tangu nimeteuliwa kuwa
naibu waziri wa Nishati katika uzalishaji huu wa umeme kwa kutumia maporomoko
ya maji, nawapongeza sana Mwenga”. anasema Mhe Mgalu
Katika suala la uhifadhi
mazingira Mhe Mgalu ameitaka kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Mufindi kuchukua
hatua za makusudi ili kuhakikisha vyanzo vya maji ikiwemo chanzo cha mto mwenga
vinatunzwa ipasavyo ili kuwa na umeme wa uhakika na wale wanaofanya shughuli za
kilimo karibu na vyanzo vya maji waondolewe mara moja bila kuoneana haya.
“Tupo katika vita ya
kuhakikisha miradi inayozalishwa kwa kutumia umeme inafanya kazi kama
ilivyokusudiwa, nashukuru mungu mwaka huu hatujaona athari katika Mtera na
Kidatu” alisema Mhe Mgalu.
Akitoa wito kwa
wakazi wa maeneo ya chanzo cha umeme wa maji Mwenga, amewataka wananchi kuendelea kutii maagizo ya serikali za mitaa ya
kutunza vyanzo vya maji, aidha amewaomba viongozi wa kisiasa kufanya maamuzi
magumu katika utekelezaji wa usimamizi wa kutunza mazingira na hasa kuwasihi
wananchi wasilime vinyungu kando na vyanzo vya maji kwa faida ya vizazi vya
sasa na vijavyo.
Kwa upande wake Mkuu
wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William amesema katika utunzaji wa vyanzo vya
maji tayari wako katika hatua mbalimbali za utunzaji na tayari wamebainisha zaidi
ya vyanzo 1900 vya maji ndani ya Wilaya ya Mufindi ambavyo vimewekewa mkakati
kabambe wa kuvitunza.
Amewaomba wananchi
kuendelea kuheshimu alama zilizowekwa na maelekezo waliyopewa kwa mujibu wa
sheria.
“Lakini kama tukiona
haiwezekani hatutasita kuwachukuia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
kuwapeleka mahakamani wote wanaokiuka sheria na taratibu za utunzaji mazingira
kati vyanzo vyetu vya maji” Alisema Mhe. William.
Ikumbukwe kuwa
sheria ya mazingira inasema kuwa ndani ya mita 60 katika eneo la chanzo cha
maji hairuhusiwi kufanya shughuli yoyote.
Nae Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo
Mgina amesema wao kama wanasiasa wanaungana na viongozi wa serikali kuendelea kutoa
elimu ya mazingira kwa wananchi ili waendelee kutambua umuhimu wa utunzaji wa vyanzo
vya maji.
Aidha Meneja Mkuu wa
Mwenga Hydro Power chini ya Kampuni tanzu ya Rift Valley Energy Mhandisi Joel
Gomba amesema wameanza kujena mitambo ya kuzalisha umeme kwa kutumia upepo
ambao unatarajiwa kukamilika na kuanza kutumika mwakani ili kuongeza nguvu
kwenye gridi ya Taifa na inategemewa kuzalishwa Megawati 2.4.
Kwa upande wake
Meneja TANESCO Wilaya ya Mufindi Mhandisi Omary Ally akitoa taarifa ya utekelezaji
wa umeme Wilaya ya Mufindi kwa Naibu Waziri wa Nishati alisema Wilaya inapokea
umeme kutoka kwa mzalishaji binafsi MWENGA HYDRO POWER anaezalisha kiasi cha zaidi
ya Megawati 3.5 MW na kuvisambazia umeme jumla ya vijiji 32 na wateja 2800.
TANESCO Wilaya ya
Mufindi inaundwa na Halmashauri ya Mji Mafinga na Halmashauri ya Wilaya Mufindi
yenye Kituo cha kupooza umeme Mgololo (220/33/11) Kv, Wilaya ina hudumia wateja
wapatao 16,436 wa Halmashauri ya Mji Mafinga na Mufindi wateja wakubwa 108 wa
kati 370 na wadogo 15, 958 aidha Wilaya inauwezo wa 30MW (Capacity) na matumizi
ya juu ni 9.5MW Megawati.
HABARI PICHA
|
Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu akipokelewa na Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William |
|
Naibu Waziri Subira Mgalu akisalimiana na Kamanda Kikosi wa Mafinga JKT Luteni Kanali D. Chalamila |
|
Naibu Waziri Mgalu akisalimiana na Afisa Uhamiaji Wilaya ya Mufindi |
|
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akisalimiana na Kamanda wa Zimamoto Wilaya ya Mufindi Jackline Mtei |
|
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga |
|
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akisalimiana na Meneja TANESCO Wilaya ya Mufindi Mhandisi Omary Ally |
|
Naibu Waziri Nishati Akisaini Kitabu katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mufindi |
|
Naibu waziri Mgalu akieleza lengo kuu la Ziara yake Wilaya ya Mufindi |
|
Pichani: Katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu Kulia Kwake ni Mwenyekiti wa ccm Wilaya ya Mufindi na Kushoto kwake ni Mkuu waWilaya ya Mufindi Mhe Jamhuri William na wa mwisho kulia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga na Mwisho Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina |
|
Naibu waziri Subira Mgalu akiwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mufindi |
|
Meneja TANESCO Wilaya Mufindi Mhandisi Omary Ally akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Nishati Katika Kijiji Cha Ikongosi |
|
Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikongosi akitoa salamu za shukrani kwa Naibu Waziri wa Nishati Wakati wa hafla ya Uwashaji wa Umeme katika Kijiji Hicho |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina |
|
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga |
|
Meneja TANESCO Kutoka Ofisi za Nyanda za Juuu Kusini |
|
Meneja TANESCO Mufindi Mhandisi Omary Ally |
|
Naibu Waziri wa Nishati Mhe Subira Mgalu akiongea na Wananchi wa Kijiji cha Ikongosi wakati wa Uwashaji wa Umeme katika Kijiji hicho |
|
Ukataji wa tepe kuashairia uwashaji wa umeme Ikongosi |
|
Katika Ofisi ya Kijiji |
|
Katika Ofisi za Mwenga |
|
Meneja Uendeshaji Mwenga Hydro Power chini ya Kampuni tanzu ya Rift Valley Energy Eng. Joel Gomba |
|
Kuelekea kwenye chanzo cha Umeme Mwenga Hydro Power |
|
Mwenga Hydro Power Mufindi |
|
Eng. Joel Gomba akimuonesha Naibu Waziri wa Nishati hatua za uzalishaji umeme kwa njia ya maji katika chanzo cha umeme Mwenga |
|
Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu akifurahia chanzo cha umeme wa nguvu ya Maji Mwenga |
|
Naibu Waziri Nishati Subira Mgalu |
|
Amani Mbwaga |
|
Kulia nia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe festo Mgina na Kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga wakiwa katika Chanzo cha Umeme Mwenga |
|
Baadhi ya Mitambo |
|
Naibu Waziri Nishati akikagua Mitambo ya uzalishaji Umeme |
|
(Picha zote na Amani Mbwaga) Kwa Maoni Au Ushauri Wasiliana nasi: Mob:+255 656 632 566 E-mail:prof.mbwaga@gmail.com Twitter:@amanimbwaga |
No comments:
Post a Comment