Saturday, November 17, 2018

MKUU WA WILAYA MUFINDI AHITIMISHA “MISITU SPORTS BONANZA” WAKATI HUO IHALIMBA MISITU FC IKIIBUKA BINGWA.

Na Amani Mbwaga, Mafinga.
Mabingwa wa Misitu Sports Bonanza 2018
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri David William leo Jumamosi  tarehe 17 Novemba 2018 akiwa mgeni wa heshima katika kuhitimisha  Bonanza la Michezo lililoandaliwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shamba la Miti Sao hill amelipongeza Shamba hilo kwa kuona umuhimu wa kuanzisha mashindano hayo yanayotumika katika kuelimisha jamii juu ya utunzaji bora wa mazingira na uhfadhi bora wa misitu.
Mhe William amewataka wachezaji kuzingatia sheria 17 za mchezo huo zilizowekwa na FIFA ili wacheze kwa amani na utulivu kwani michezo ni umoja ni ajira, afya na ni furaha.

Bonanza hilo lililanza toka tarehe 27 Oktoba 2018 na kushirikisha timu 32 kutoka katikaTarafa zake kuu  nne za Mgololo, Ihalimba, Ihefu na Irundi na hatimae kufikia tamati leo ambapo Ihalimba Misitu wameweza kuibuka washindi wa mashindano haya ya Bonanza la Misitu mwaka 2018  kwa kuifunga Ihefu Misitu Bao Moja kwa nunge  na kufanikiwa kuondoka na Medali na kitita cha Shilingi Laki 6.


Aidha Ihefu Misitu imeibuka mshindi wa pili na mshindi wa tatu ni Sawala FC Baada ya Kuichabanga Villa FC mbali na hiyo kulitanguliwa pia na mechi kali ya Mafinga veterani Vs Saohill Misitu Veterani na baadae Makambako Veteran Vs Mafinga Veterani bila kusahau netball iliwakutanisha Saohill Misitu Vs Polisi Mafinga ambapo Sao Hill Misitu iliibuka bingwa wa mchezo huo.

Mwaka huu wa Fedha 2018/2019 Shamba la Miti Sao Hill limedhamiria kushirikiana na vijiji vinavyozunguka mradi wa shamba  kwenye suala zima la Michezo ambayo imehitimishwa leo katika Viwanja vya  Sao Hill Misitu (Ihefu) iliyoanza saa 1:00 Asubuhi kwa kuanza na michezo mbalimbali  ikiwemo     Riadha (Sao Hill Marathon Kilomita 7 ) Kukimbiza kuku,  kukimbia kwenye magunia, kuvuta kamba, draft, netball, volley ball, football iliyoanza na Mchezo wa timu ya Mafinga Veteran Vs Misitu veteran, Makambako Veteran Vs Mafinga veteran, mpira wa watoto baina ya timu ya Twico na Misitu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mashindano hayo na Afisa Nyuki Shamba la Miti Sao Hill Bwana Said Aboubakar amethibitisha kwamba mara baada ya fainali hiyo kuisha tayari shamba limeandaa (Tour) ziara ya kutembelea Mikoa mbalimbali na kujionea vivutio lakini pia kucheza mechi za kirafiki na timu kubwa hapa Tanzania kwa wachezaji ambao watachaguliwa kuunda timu ya Misitu Saohill kutoka katika vijiji vyote vilivyoshiriki mashindano hayo.

Lengo la Mashindano hayo ilikuwa ni kutoa elimu juu ya masuala ya majanga ya moto kichaa hasa wakati huu wa maandalizi ya mashamba lengo ambalo limetimia kwa asilimia nyingi zaidi, lengo lingine ni kuimarisha uhusiano uliopo baina ya Shamba la Miti Sao-Hill na Vijiji vinavyozunguka, shamba, kujenga afya, ajira, sanjari na kurudisha shukrani kwa jamii (Corporate Social Responsibility) inayoambatana na zawadi nono kwa washindi walioshiriki michezo mbalimbali.

Michezo hiyo ilikuwa ikiambatana na kauli mbiu ya “Utunzaji wa Rasilimali za Misitu na Nyuki ni Jukumu letu sote Katika Kukuza Uchumi wa Viwanda”


 HABARI PICHA
Sao Hill Misitu Veteran

Mafinga Veteran

Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William Kushoto akiwa  na Meneja wwa Shamba la Miti Saohill wakifuatilia kwa makini Misitu Sports Bonanza 2018 (Picha Na Amani Mbwaga)

Mwenyekiti wa Mashindano Bwana Said Aboubakar akitoa maelezo ya mashindano hayo kwa mgeni wa heshima hayupo pichani Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William

Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William akisalimiana na wachezaji wa Sao Hill Misitu Veteran

Mkuu wa Wilaya Mufindi akisalimiana na mmoja wa waamuzi wa mashindano ya Misitu Sports Bonanza Bwana Lupakisyo Mwakibinga

Mkuu wa Wilaya Mufindi Akisalimiana na Kamishina wa Mashindano na Refarii Mkongwe Bwana Turka

Mkuu wa Wilaya akisalimiana na Wachezaji wa Mafinga Veteran na hapo anasalimiana na Mchezaji Peter Kibona



Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William akipiga Penati ya Ufunguzi wa  Fainali za Misitu Sports Bonanza wakati huo golikipa ni Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herberth Haule.

Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill  Bwana Haule nae akipiga penati wakati huo golikipa ni meneja wa benki ya CRDB









Kufukuza Kuku

Mshindi wa kukamata kuku


Washindi waliokamata kuku

Mkuu wa Wilaya Mufindi  Mhe Jamhuri William akiongea na wachezaji na wananchi kuhusu umuhumu wa shamba la miti Sao Hill katika fainali za Misitu Sports Bonanza

Mkuu wa Wilaya akisalimiana na Makambako Veterani

Kikosi cha Makambako Veteran

Kikosi cha Mafinga Veteran


Mashindano ya Draft 



Kikosi kazi cha Kuzima Moto cha Shamba la Miti Sao Hill  kikifanya onesho lake mbele ya mgeni wa heshima Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William



Mechi Kikosi cha Watoto Twico Fc

Mechi Kikosi cha Watoto Misitu Sao Hill FC


Villa FC

Sawala FC

Ihalimba Misitu FC Mabingwa wa  Bonanza 2018


Ihefu  Misitu FC Washindi wa Pili Mwaka 2018



Sao Hill Misitu Netball

Polisi Mafinga NetBall






















Picha ya Pamoja na washindi  wa michezo mbalimbali ya Misitu Bonanza Mwaka 2018 (Picha zote na Amani Mbwaga)

No comments:

Post a Comment