Ihefu Fc Mabingwa Tarafa ya II Ihefu |
Mashindano ya Mpira wa miguu ya Misitu Sports Bonanza Chini
ya Udhamini mkuu wa Wakala wa huduma za Tanzania (TFS) Shamba la Misitu
Sao-Hill yameendelea kutimua vumbi mapema leo hii katika viwanja vya Misitu Sao
Hill vilivyopo ndani ya tarafa ya pili Ihefu Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.
Mashindano hayo yameshirikisha timu 8 kutoka katika vijiji
mbalimbali vinavyozunguka shamba la miti Sao-Hill Kundi A ilishirikisha timu za
Matanana FC, Mtula FC, Sao Hill FC na Bumilayinga FC Kundi B ni TWICO FC, Ihefu FC, Changarawe FC na
Nyororo FC.
Timu ya IHEFU FC imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa ushindi
mabao 2-0 dhidi ya SAO HILL FC Magoli yote yamefungwa na mshambuliaji hatari EDWINI
ILOMO timu hiyo sasa inaiwakilisha Tarafa ya pili ya Ihefu kuelekea hatua ya nusu fainali.
Aidha Mshindi wa kwanza amepewa zawadi ya Pea moja ya jezi
na mshindi wa pili amepewa zawadi ya mpira mmoja.
Mgeni wa Heshima wa bonanza hilo alikuwa Meneja wa Shamba la
Miti Sao Hill Bwana Heriberth Haule.
Mashindano haya ya bonanza yanalengo la kukumbusha jamii
kuhusu matumizi bora ya moto hasa wakati huu wa maandalizi ya mashamba ili
kuepuka hasara inayoweza kujitokeza kwa kuunguza misitu ya serikali na watu
binafsi lakini vileveile kutoa elimu ya ufugaji nyuki na kuendeleza mahusiano
mazuri baina ya Shamba na Jamii inyozunguka.
Shamba la miti Sao Hill lina dira ya kuwa na misitu
iliyojifadhiwa ikiwa na matumizi endelevu na kulinda kwa kushirikisha jamii.
HABARI PICHA
Mgeni wa Heshima Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herberth Haule akimkabidhi zawadi Mshindi wa Pili wa Tarafa ya Pili ya Ihefu timu ya Sao Hill Kijiji |
Timu ya Sao Hill Kijiji FC |
Mgeni wa Heshima Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herberth Haule akimkabidhi zawadi Mshindi wa Kwanza wa Tarafa ya Pili ya Ihefu timu ya Ihefu FC |
Timu ya Ihefu FC Washindi wa kwanza wa Tarafa ya II ya Ihefu |
No comments:
Post a Comment