Na Amani Mbwaga, Mafinga.
Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga leo ameongoza wananchi katika
shughuli za maendeleo ya kijiji cha Isalavanu katika ukarabati wa Shule ya
Msingi Mamba iliyoko katika Kata ya Isalavanu Halmashauri ya Mji Mafinga M`koani
Iringa.
Zaidi ya Milioni 4
zimeokolewa kwa siku moja kutokana na nguvu za Wananchi, Mchango wa Mhe Charles
Makoga akishusha Mifuko 60 ya Cement yenye thamani ya Tsh 900,000/= na Mdau wa
Maendeleo ambae ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Tumain Jipya Dkt. Basil Tweve ambae
amechangia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 4.
Mhe Makoga amewapongeza
wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ambapo zaidi ya wananchi
300 wa kijiji cha Isalavanu wameshiriki katika ujenzi huo na kumtaka Afisa
mtendaji wakijiji kuthaminisha nguvu ya wananchi kama Rais Dkt John Pombe
Magufuli anavyotaka nguvu ya wananchi ithaminishwe na isomwe kwenye taarifa za
mapato na matumizi ya kijiji na Shule hii ndio aliyoisoma Mhe Makoga.
“Wananchi
ninawapongeza kwa mwitilio wenu na mmejenga wenyewe kwa nguvu zenu, naomba
tumalizie jengo hili na tutahakikisha majengo yote yanapakwa rangi na tayari
nimeshamwagiza Afisa Mipango Miji aje afanye tathimini hapa ya kazi iliyobakia
ili serikali iweze kuwaletea fedha kama Milioni 10 hivi kwa sababau tayari
mmeonesha nia” alisema Mhe Makoga
Akisoma taarifa ya
utekelezaji wa ujenzi huo kwa wananchi Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Isalavanu
Bwana Noel Kabinda alisema wanachi wamejitokeza kwa wingi kutokana na
uhamasishaji uliofanywa na Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri yaMji Mafinga ambae
ndie diwani wa kata hiyo ya Isalavanu, kutokanana na Mahafali ya darasa la saba
lilipoibuka suala la ukarabati wa shule hiyo kupitia kwa aliyekuwa mgeni rasmi
Dkt Basil Tweve.
Jumla ya vyumba 02
vya madarasa ofisi 01 ya waalimu, Jiko la Muda la Kupikia chakula cha wanafunzi
shuleni, ujenzi wa vyoo vya wanafunzi vyenye matundu 14 vimekarabatiwa kwa siku
moja, aidha oparesheni ondoa nyasi kwenye nyumba za waalimu imefanyika ili
kuweka mazingira mazuri ya kuishi kwa waalimu wa shule hiyo.
Akitoa shukrani za
pongezi kwa niaba ya Wananchi Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Isalavanu ambae pia
ni katibu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata hiyo Bwana
Fulgence Kadinde ambae pia alisoma shule hiyo toka mwaka 1981 hadi mwaka 1987
ameishukuru serikali chini ya Mhe Makoga kwa kushirikiana kuhamasisha wananchi katika shughuli hizo za
maendeleo.
“Maendeleo hayana
chama kwani leo wote tupo hapa bila
kujali vyama vyetu katika shughuli za kuleta maendeleo yetu hasa katika ujenzi
wa shule yetu hii ya msingi Mamba, nakupongeza kwa kutafuta wadau lakini pia
ongeza badii ya kiutendaji na katika hili tunakusifu na tunakupenda sana maneno
ya kisiasa tuyafunike endelea kupiga kazi” alisema Ndugu
Kadinde
Kwa upande wake
mmoja wa waalimu wakongwe na waanzilishi wa shule hiyo toka inafunguliwa rasmi
mwaka 1977 akiwa Mwalimu Mkuu Msaidizi Mwl. Leonya Victory Kalinga amesema toka
shule hiyo inaanzishwa hajawahi kuona mwitikio mkubwa wa wananchi katika
shughuli za maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo imekuwa historia kubwa katika
kijiji hicho kuwahi kutokea.
Shule ya Msingi
Mamba ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 07 Novemba 1977 chini ya Mwalimu Mkuu wa
Kwanza Mwl. Joseph Mbishi na inamilikiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga Mkoani
Iringa na ndio shule aliyoisoma Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe.
Charles Makoga toka darasa la kwanza hadi hadi la saba.
HABARI PICHA
No comments:
Post a Comment