Sunday, November 4, 2018

Sawala FC yaibuka Mshindi Misitu Sports Bonanza Tarafa ya I ya Shamba la Miti Sao Hill Irundi.

Na Amani Mbwaga, Mufindi.

Mabingwa Sawala FC wakiwa wamevaa Jezi mpya Kutoka Sao Hill Misitu
Timu ya SAWALA FC imefanikiwa kutwaa ubingwa kwa ushindi mabao ya mikwaju ya penati dhidi ya MNINGA FC baada ya kutinga fainali kutoka kwenye hatua za Makundi, timu hiyo sasa inaiwakilisha Tarafa ya kwanza ya Irundi kuelekea hatua ya nusu fainali itakayopigwa Siku ya Jumapili ijayo katika viwanja vya Ihefu Sao Hill Misitu ambapo ndio makao makuu ya Shamba la miti Sao Hill

Mashindano ya Mchezo wa Mpira wa miguu ya Misitu Sports Bonanza Chini ya Udhamini mkuu wa Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shamba la Misitu Sao-Hill yameendelea kutimua vumbi mapema jana Jumapili katika viwanja vya Kihanga vilivyopo ndani ya tarafa ya kwanza Irundi Wilayani Mufindi Mkoani Iringa.

Mashindano hayo yameshirikisha timu 8 kutoka katika vijiji mbalimbali vinavyozunguka shamba la miti Sao-Hill,ikiwemo Mninga FC. Nzivi FC, Kitilu FC, Lugongo FC, Kihanga FC, Irundi FC, Mtili FC na Sawala FC
Aidha Mshindi wa kwanza amepewa zawadi ya Pea moja ya jezi na mshindi wa pili amepewa zawadi ya mpira mmoja.

Mashindano haya ya bonanza yana lengo la kukumbusha jamii kuhusu matumizi bora ya moto hasa wakati huu wa maandalizi ya mashamba ili kuepuka hasara inayoweza kujitokeza kwa kuunguza misitu ya serikali na watu binafsi lakini vilevile kutoa elimu ya ufugaji nyuki na kuendeleza mahusiano mazuri baina ya Shamba na Jamii inayolizunguka.

Kwa Mujibu wa Mwenyekiti wa Mashindano ya Misitu Sports Bonanza 2018 na ambae pia ni Afisa Nyuki wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Said Aboubakar ametoa mwelekeo wa nusu fainali  itakavyopigwa  siku ya jumapili ikikutanisha timu 4 zinazowakilisha tarafa 4 za shamba la miti Sao Hill ambapo Tarafa ya kwanza inawakilishwa na Sawala FC, Tarafa ya II Ihefu Misitu FC, Tarafa ya III Ihalimba Misitu FC na tarafa ya IV ni Villa FC inayowakilisha Tarafa ya Mgololo.
HABARI PICHA
Mninga FC Washindi wa Pili Misitu Sports Bonanza Tarafa ya Irundi
Nzivi FC


Kitiru FC

Lugongo FC

Kihanga FC

Irundi FC

Mtili FC

Sawala FC Mabingwa Misitu Sports Bonanza Tarafa ya I ya Irundi


Ukaguzi wa Timu ukiendelea


Kulia waliokaa ni Afisa Habari TFS -Sao Hill Mwanaisha Luhaga, Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Misitu Sports Bonanza na Afisa Nyuki Shamba la Miti Sao Hill Bwana Said Aboubakar na anaefuatia ni Meneja msaidizi wa Tarafa ya I ya Irundi (Picha na Amani Mbwaga)





Wachezaji wote wakipata chakula cha mchana Kutoka Shamba la Miti Sao Hill










Kushoto ni Kapteni wa Sawala FC na Kulia ni Kapteni wa Mninga FC Wakati wa Fainali



Zawadi ya Jezi na Mpira zikiwa tayari kusubiri Mshindi

Mwenyekiti wa Misitu Sports Bonanza Bwana Said Aboubakar akitangaza Mshindi wa Bonanza hilo katika Tarafa ya Irundi

Mshindi wa Pili timu ya Mninga ikipata zawadi ya Mpira



Kapteni wa Timu ya Sawala akipoea zawadi ya jezi ya mshindi wa kwanza wa bonanza la Misitu Tarafa ya Irundi




Wachezaji wa Timu ya Sawalawakifurahia ushindi walioupata
 

Picha zote na Amanni Mbwaga
Kwa Maoni au Ushauri wasiliana nasi:
Mob:+255 656 632 566
E-mail:prof.mbwaga@gmail.com



No comments:

Post a Comment