Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imekabidhi Pikipiki ishirini na saba (27) aina ya Honda kwa Maofisa elimu kata kutoka kata zote ishirini na saba (27) za Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mkoani Iringa.
Akizungumza mara
baada ya kukabidhi Pikipiki hizo Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri David William,
amesema Pikipiki hizo zimefika kwa wakati muafaka ili kurahisisha jukumu la
ufuatiliaji na usimamizi wa elimu katika Halmashauri.
“Mmepata usafiri huu
ambao utachangia kutatua changamoto za kufanya kazi zenu hivyo, hatutaki kuona
utoro unaendelea, hatutaki kuona mimba zinandelea hasa katika shule za
sekondari, sasa hatuna sababu ni lazima tuhakikishe elimu inakua bora zaidi na
ufaulu wetu kitaifa kama Halmashauri unapanda” alisema Mhe
William.
Aidha, Mhe. William,
ametoa wito kwa Maofisa elimu kata kuhakikisha wanazitunza Pikipiki hizo na
kusisitiza kwamba usafiri huo sio kwa ajili ya kufanyia biashara ya bodaboda
bali zifanye kazi iliyokusudiwa.
Naye, kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Bw. Isaya Mbenje, amesema
Pikipiki hizo ni mali ya Serikali hivyo zitasimamiwa kwa mujibu wa taratibu na
sheria za serikali ikiwa ni pamoja na kufanyiwa matengenezo kwenye kalakana kwa
mujibu wa sheria ya manunuzi ya umma.
Kwa upande wake Ofisa
Elimu Msingi Bw. Kennedy Bukagile, amesema, lengo la Pikipiki hizo ni
kuwawezesha Maofisa elimu kata kutembelea shule zilizopo katika kata zao ili
kufuatilia maendeleo ya utendaji kazi.
“Mfano
Ofisa elimu kata mwenye shule nyingi ni kumi (10) kwa hiyo ni rahisi sana
kuzifuatilia shule zake ndani ya mwezi mmoja anaweza kuzifikia shule zote”
alisema Bw. Bukagile.
Akitoa shukrani mara
baada ya hafla ya makabidhiano kiongozi wa Maofisa elimu kata ambaye pia ndiye
Ofisa elimu wa kata ya Ifwagi ameishukuru serikali ya awamu ya tano chini Rais Dkt.
John Pombe Magufuli, kwa kuwapatia nyenzo hiyo muhimu katika utendaji kazi lakini
pia akawashukuru Wabunge, Madiwani pamoja na Mkurugenzi Mtendaji kwa kuishauri
vizuri serikali na hata kupatiwa usafiri huo.
Kutolewa kwa usafiri
huu ni mwendelezo wa Serikali unakusudia kuiboresha sekta muhimu ya elimu,
kwani mapema mwaka 2016 Serikali ilianza kutoa kiasi cha Shilingi. 250,000 kama
posho ya madaraka kwa Maofisa elimu kata, wakati wakuu wa shule wakipokea 200,
000 kila mwezi.
.
HABARI KATIKA PICHA
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William akikabidhi pikipiki kwa mmoja wa Maafisa Elimu Kata |
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri William akiongea na Maafisa Elimu Kata wakati wa Makabidhiano ya Pikipiki |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina (Kushoto) nae akitoa salamu zake za shukrani kwa serikali. |
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Bwana Issaya Mbeje aktoa neno kwa Maafisa Elimu Kata wakati wa Makabidhiano ya Pikipiki |
Afisa Elimu Msingi (W) Bwana Kennedy C. Bukagile akiongea na Waandishi wa Habari hawapo pichani baada ya kupokea pikipiki 27 katika Halmashauri ya Wilaya Mufindi |
Afisa Elimu Kata ya Ifwagi Bwana Jordan Ngogo kwa niaba yaMaafisa Elimu Kata Halmashauri ya Wilaya Mufindi akitoa Shukrani kwa Serikali |
Kaimu Kamanda Usalama Barabarani (W) Mufindi Koplo Hassan Khatib akitoa elimu ya usalama barabarani kwa Maafisa Elimu Kata Wote Waliokabadhiwa pikipiki.. |
(Picha zote na Amani Mbwaga)
No comments:
Post a Comment