Monday, August 20, 2018

PROF. SHEMDOE AKABIDHI MIKOBA YA UKURUGENZI HALMASHAURI YA MUFINDI.

Na Amani Mbwaga, Mufindi.
Hatimaye aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe, ambae kwa sasa ndiye Katibu Talawa wa Mkoa wa Ruvuma kufuatia uteuzi wa mkuu wa nchi, amekabidhi rasmi Ofisi na madaraka ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi kwa kaimu Mkurugenzi Ndugu. Isaya Mbenje, kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uongozi katika taasisi za umma.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika ofisini kwa Mkurugenzi mtendaji, Prof. Shemdoe, amewashukuru wakuu wa idara, vitengo na watumishi wote kwa ujumla ambao  walimsaidia kazi kwa juhudi maarifa na uaminifu jambo ambalo limesababisha aonekane na mamlaka za juu na hata kupata madaraka makubwa zaidi.
“Ninyi wakuu wa idara ndiyo mlioanifundisha kazi huku Serikali za mitaa, wakati nakuja huku nilikuwa sijui kitu, huku tofauti sana na  kule chuo kikuu nilikotoka, kule niljiua leo ninakipindi saa nne, nikitoka darasani najifungia kundika maandiko, ni kweli kwamba Mufindi ndiyo sehemu pekee ambayo kwa kiasi kikubwa nimejifunza uongozi hivyo, popote nitakapokuwa sitaisahau katika maisha yangu”
Aidha, Prof. Shemdoe, amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kutolinganisha uongozi wake na ule wa kaimu aliyemwanchia Ofisi wala kiongozi atakayeteuliwa rasmi kurithi nafasi yake na kusisitiza kuwa binadamu wanatofautiana na hata siku moja hawawezi kufanana kwa kila kitu kwani kila mmoja anamtazamo wake na namna yake ya kuongoza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ambaye ndiye alikuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo, amempongeza  kwa uadilifu na utendaji mzuri wa kazi na akabainisha kuwa mara zote alitumia taaluma yake kama Profesa kutatua changamoto zilizokuwa zikijitokeza.
Hakika kulikuwa hakuna changamoto ambayo ilikuwa haipati utatuzi kwa Prof, alinisaidia sana kupata shuluhisho la mambo mengi hata kwa mambo yangu binafsi, alikuwa kiunganishi sahihi kati ya ofisi ya DC na Halmashauri ni katika kipindi chake uhusiano wa Ofisi hizi mbili ulikiwa imara zaidi, ungeweza kudhani Ofisi ya DC na Mkurugenzi ni moja.”Alisema  Mkuu wa Wilaya.
WASIFU. Prof. Riziki Shmdoe alizaliwa  Wilayani Lushoto Mkoani Tanga Mwaka 1974, alipata Shahada ya tatu ya  uzamivu PHD chuo kikuu cha Ghent kilichopo barani Ulaya Nchini Ubeligiji na kubobea kwenye taaluma ya (Applied Biological Sciences). Mwaka 2001 mpaka 2003 alisoma na kuhitimu shahada ya umahili (Masters) katika chuo kuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro akijikita kwenye (Management of Natural Resources For Sustainable Agriculture). Mwaka 1997 -2000 alisoma na kuhitimu Shahada ya kwanza ya taaluma ya Misitu katika chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine  (SUA) Morogoro’
Aidha, 1994 – 1996 kidato cha 5 -6 Shule ya Sekondari SAME
1990 -1993: Kidato cha nne LWANDAME Sekondari
1983 – 1989: NGWERO Shule ya Msingi .
HABARI PICHA
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe akiongea na Watumishi waliokuwa wakikshuhudia Makabidhiano ya Ofisi (Hawapo Pichani)

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina nae akisaini nyaraka za Makabidhiano ya Ofisi ya Mkurugenzi Mufindi (Picha zote na Ofisi ya Habari Mawasiliano naUhusiano).








No comments:

Post a Comment