Na Amani Mbwaga, Mafinga.
|
Furaha kubwa katika Ziwa Ngwazi linalopatikana katika Shamba la Miti Sao Hill |
Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) Shamba la Miti Sao Hill, iko katika mpango kabambe wa kuanzisha
Utalii wa Nyuki kwa kushirikiana na kampuni tanzu ya nyuki safari kutoka
Marekani na kampuni ya Follow the Honey Tanzania.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Follow The Honey Tanzania Bwana Kaizerege Camara ambae
aliambata na Mkurugenzi Mkuu na Mwanzilishi wa Kampuni Tanzu ya Nyuki Safari
kutoka Marekani na Follow the Honey Tanzania Bi Marry Canning katika Shamba la
Miti Sao Hill liliopo Wilayani Mufindi Mkoani Iringa .
Ziara hiyo
ilifanyika jana na kujionea shughuli
mbalimbali za ufugaji wa nyuki na uzalishaji wa asali ya SaoHill Honey
wamefurahishwa na jinsi shamba lilivyo na vivutio vingi hali itakayochangia
kuchochea utalii wa nyuki Tanzania.
“Tumegundua kwamba
Tfs ni Zaidi ya Misitu baada ya kujionea fursa zilizopo katika shamba la Miti
Sao Hil ikiwemo Miti iliyopandwa, Miti ya Asili, vyanzo vya maji, ziwa aina
mbalimbali za maua, kwa hiyo ni jambo la kujivunia kuona kwamba taasisi hii
inafursa kubwa sana ya kuweza kuitangaza Tanzania ndani na nje ya nchi kupitia
asali na baadhi ya vivutio vilivyopo katika shamba hilo”
alisema Bwana Camara.
Wameona ufugaji wa nyuki ambao umefikia kwa kiwango
kikubwa sana hadi kufikia ufugaji wa kibiashara na kuahidi kushirikiana na
serikali ili kuhakikisha asali inayozalishwa Tanzania katika Shamba la Miti Sao
Hill inapata masoko katika nchi mbalimbali duniani ikiwemo marekani na hatimae
kuitangaza nchi na kuingiza pato la Taifa.
Aidha wawekezaji hao
wameahidi kuandaa Makala (Documentary) kwa kushirikiana na wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) itakayoonesha vivutio vya kipekee vilivyopo katika shamba
la miti Saohill ili itumike kwenye Shirika la ndege Tanzania (ATCL) kwenye
video za ndege zake na ulimwenguni kote kuonesha Utalii wa nyuki na kuitangaza asali
ya Sao Hill Honey Tanzania.
Kwa upande wake
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herberth Haule kwa maslahi ya umma ameahidi
kutoa ushirikiano kwa kampuni hiyo kuhakikisha kwamba shamba la miti Sao hill linakuwa
zaidi ya Miti ambapo itaongeza fursa kwa Watanzania ikiwemo ajira, kipato
lakini pia kuchangia uchumi wa Taifa.
Aidha Afisa Nyuki wa
Shamba la Miti Sao Hill Bwana Said Aboubakar ameishukuru kampuni hiyo na kusema
kwamba kampuni hiyo imekuja wakati muafaka na kwa nia njema ya kukuza utalii wa
nyuki nchini Tanzania hususani katika Shamba la miti Saohill hivyo ameona kuna
fursa nyingi zinaweza kutumika kupitia Safari nyuki ambayo itaunganisha masoko
ya asali yenye ubora kutoka Tanzania na kuuza nnje ya nchi na hatimae kujipatia
fedha za kigeni.
Shamba la Miti Sao
Hill lina ukubwa wa hekta 135,903 ambazo zimehifadhiwa kwa ajili ya upandaji
miti na hifadhi ya mazingira, kati ya eneo hilo kiasi cha hekta 86,003 ni kwa
ajili ya upandaji miti kibiashara, hekta 48,200 kwa ajili ya utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji na kekta
1,700 ni kwa ajili ya makazi na uwekezaji.
HABARI PICHA
|
Bi Marry Canning Akisaini Kitabu Cha wageni Katika Ofisi ya Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill |
|
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herbert Haule |
|
Mkurugenzi na Mwanzilishi wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania Bi Marry Canning |
|
Majadiliano na Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Yakiendelea |
|
Picha ya Pamoja |
|
Banda la Uuzaji wa Asali ya Sao Hill Honey |
|
Happy mmoja wa waandaaji wa Asali ya Sao-hill kabla haijaenda Sokoni akionesha jinsi inavyopakiwa. |
|
Bi Mary Canning akiwa na Afisa Nyuki wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Said Aboubakar |
|
Moja ya Mzinga wa nyuki wa asili uliokuwa ukitumika katika Shamba la Miti Sao Hill kwa ajili ya ufugaji wa nyuki |
|
Mr Camara wa kwanza kushoto akiwa na Bi Marry na Kulia ni Bwana Side Aboubakar wakiangalia jinsi utomvu unavyovunwa Katika Shamba la Miti Sao-Hill ikiwani moja ya kivutio cha watalii. |
|
Mr Camara Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Follow the Honey Tanzania |
|
Baadhi ya miche iliyoandaliwa katika shamba la miti Sao Hill tayari kwa kupandwa katika msimu huu wa upandaji miti |
|
Baadhi ya Msitu wa Miti ya Sao Hll Katika Muonekano |
|
Furaha kubwa katika ziwa Ngozi linalopatikana ndani ya Shamba la Miti Sao Hill ni moja ya kivutio kikubwa cha utalii |
|
Afisa Nyuki Shamba la Miti Sao Hill Bwana Side Aboubakar Akiwaonesha viongozi waandamizi wa Kampuni ya Follow the honey Tanzania (Hawapo pichani) baadhi ya mizinga ya Nyuki liyopo katika shamba la miti Sao Hill |
|
Picha zote na Amani Mbwaga
Kwa Maoni au ushauri Wasiliana nasi;
Simu: +255 656 632 566
E-mail:prof.mbwaga @gmail.com |