Wednesday, August 29, 2018

Halmashauri ya Wilaya Mufindi yavuka lengo Ukusanyaji wa mapato na kufikia asilimia 90.96


Na Amani Mbwaga Mafinga.
Halmashauri ya Wilaya Mufindi Imevuka lengo la Ukusanyaji Mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani katika mwaka wa fedha 2017/2018, na kufikia silimia 90.96.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina wakati wa kutano wa Baraza la Madiwani la robo ya nne lililofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mkoani Iringa.

Ilielezwa kuwa katika kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 Halmashauri ilikusanya na kupokea jumla ya Tsh Bilioni 35.3 kati ya mapato hayo Tsh Bilioni 3.5 ni mapato yaliyotokana na vyanzo vya ndani, Tsh Bilioni 24.6 ni mishahara, Tsh bilioni 5 ni miradi ya maendeleo na Tsh Bilioni 2 ni matumizi ya kawaida.

Aidha katika kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 mchango wa wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo ulikuwa na thamani ya Tsh Milioni 793.5.

Mlinganisho wa mapato halisi ya Tsh Bilioni 35.3 kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 na makisio ya Tsh Bilioni 51.13 ya mwaka 2017/2018 unaonesha kuwa Halmashauri imekusanya asilimia 68.4 ya lengo la mwaka wa fedha wa 2017/2018.

Aidha mlinganisho wa mapato yatokanayo na vyanzo vya ndani yaliyokusanywa kwa kipindi cha Julai 2017 hadi Juni 2018 ya Tsh  Bilioni 3.5 na makisio ya mapato yanayotokana na vyanzo vya ndani ya Bilioni Tsh 3.8 kwa kipindi hicho yanaonesha kuwa Halmashauri ya Wilaya Mufindi imekusanya asilimia 90.96 ya lengo la mwaka.

“Mimi nawapongeza sana Mkurugenzi na timu yako kwa kufikia mafanikio Makubwa ya ukusanyaji mapato katika Halmasahuri yetu, niwasihi muendelee kufanya vizuri zaidi katika ukusanyaji lakini pia ni lazima tuongeze kasi na kuwa wabunifu wa kuwapata watu wakorofi wanaokwepa kulipa ushuru na kodi mbalimbali za serikali” alisema Mhe Mgina.

Aidha amewaasa Waheshimiwa Madiwani kushirikiana na kuendelea kujenga Mahusiano mazuri zaidi na Ofisi ya Mkurugenzi na wataalamu wake ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Mufindi na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William aliwashukuru waheshimiwa madiwani kwa kuasidia utekelezaji wa majukumu ya serikali na hasa katika uhamasishaji wa kampeni ya ujenzi wa vyoo bora kwa wanachi.

Mhe Mwenyekiti tumezindua kampeni ya ujenzi wa vyoo bora kwenye wilaya yetu na haya ni maelekezo ya serikali, na sisi mufindi katika utekelezaji wa hilo tumejipa hadi tarehe 30 Oktoba 2018, tuhakikishe kila kaya inakuwa na choo bora. Alisema Mhe William.

Tafsiri ya choo bora tayari imekwishatolewa na wananchi wanaelewa, waheshimiwa madiwani wote wameombwa kuzungumza lugha moja, ili kuhakikisha wananchi wote wanakuwa na vyoo bora.

Utekelezaji wa kampeni hiyo unaambatana na usimamizi wa sheria ya mazingira.

Takribani asilimia 20% ya kaya ndio zenye vyoo bora Wilaya ya mufindi na asilimia 80% ni vyoo ambavyo si bora, kaya nyingi zinatumia vyoo vya asili sasa ni wakati wa kuhakikisha jamii inakuwa na vyoo bora.

Nae Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Bwana Isaya Mbenje amewakumbusha waheshimiwa madiwani kuhusu kulinda mali za asili na mazingira kwa ujumla kutokana Msimu wa kulimo unaokuja hivi karibuni ambapo watu wakati wa kuandaa mashamba huchoma moto hovyo unaoathiri mazingira na maliasili zilizopo.


“Katika Wilaya yetu tunatarajia msimu wa kilimo na tunaanza maandalizi ya mashamba kwa ajili ya kilimo hivyo tunaenda kuwa na kampeni ya kuhakikisha wananchi wanapoenda kusafisha mashamba yao wasichome na maeneo mengine” alisema Bwana Mbenje.

HABARI PICHA















Friday, August 24, 2018

Halmashauri ya Mji Mafinga Kununua Gari ya Taka.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga akiongea na Wajumbe wakati wa Mkutano wa  Baraza la Madiwani uliofanyika leo hii katika ukumbi wa Halmashauri mjini Mafinga (Picha  na Amani Mbwaga)

Na Amani Mbwaga, Mafinga.
Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga limedhamiria kununua gari ya taka katika mwaka huu wa fedha ili kuongeza kasi ya ukusanyaji taka katika mji wa Mafinga na kuhakikisha mji unakuwa safi wakati wote.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga katika Mkutano wa baraza la Madiwani wa Robo ya nne 2017/18 uliofanyika leo katika Ukumbi wa Halmashauri mjini Mafinga, Mkoani Iringa.

Tumenunua trekta jipya pia tuna gari nyingine kwa ajili ya kubeba taka lakini mwaka huu tunanunua gari nyingine ya taka kuhakikisha kwamba tunakuwa na magari ya kutosha kubebea taka katika mji wetu ili uwe safi zaidi na tutasimamia hapo” alisema Mhe Makoga.

Baraza limeagiza pia kila duka, taasisi za serikali na zile za binafsi kuhakikisha zinakuwa na vyombo vya kutunzia taka.

Agizo la Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William linawataka Wananchi wote kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi kufanya usafi wa kina katika maeneo yote yanayowazunguka.

“Usafi ni jukumu la sisi wote hata Waheshimiwa Madiwani tunatakiwa kwenda kufanya usafi, basi kesho ni siku ya usafi tuungane wote kwenda kushiriki kufanya usafi katika Mji wetu wa Mafinga” alisema Mhe Makoga.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya  ambae pia ni Afisa Tarafa wa Tarafa ya Malangali Ndugu Daniel Dugange akitoa salamu za Mkuu wa wilaya amewataka watendaji kuja na mikakati bora zaidi ili kuboresha huduma bora kwa wananchi.

Amehimiza kudumisha ushirikiano zaidi katika kutatua changamoto mbalimbali ikiwemo migogoro ambayo viongozi wa ngazi ya kijiji, Kata na Tarafa imeshindikana ili kuwahudumia wananchi kwa ukaribu.

“Tukumbuke kwamba katika kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2015 tumeshatafuna miezi 32 bado miezi 28 tu tumalize kipindi cha miaka 05, kwa hiyo tujipange vizuri tuwe na mpango mkakati mpango ambao unaangalia mambo 04, uwezo tulionao, udhaifu, fursa zilizopo na matatizo yaliyopo” Alisema Bwana Dugange.

Rasilimali ni chache lakini ni lazima kujipanga kwa uchache wa rasilimali zilizopo ili kuweza kufikia malengo na dira ya Taifa ya 2025.

Aidha Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Mafinga Bwana Voster Mgina amelieleza baraza la madiwani kuhusu ushirikiano ulioanza kufanywa baina ya shule za serikali na zile za binafsi ili kuongeza ufaulu katika Halmashauri ya mji Mafinga ukizingatia shule nyingi za binafsi katika mji huu zinafanya vizuri katika matokeo ya mitihani ya Taifa zaidi ya shule za serikali.

“Sasa hivi Waheshimiwa Madiwani tuna mitihani yetu ya Muhula ambapo tunatarajia kuwa na mtihani mmoja kwa shule zote za serikali na zile za binafsi hata hivi leo ninavyozungumza waalimu wetu wa shule zote wako shule ya Sekondari Bethel wakipitia mitahani ambayo itafanyika mwezi wa Novemba 2018 ni mtihani mmoja unatungwa na Waalimu wana upitia pale kuhakikisha unakuwa vizuri” alisema Bwana Mgina.

Aliongeza pia kumekuwa na mafunzo ya pamoja kwa waalimu wa shule zote za binafsi na serikali ambayo hufanyika mara kwa mara, na jana tu Baadhi ya waalimu wa Sayansi walikuwa wakipewa mafunzo ya vitendo katika sule ya Sekondari JJ Mungai kutoka kwa wakufunzi wa Chuo cha Kleruu ili kuwafundisha waalimu namna nzuri ya kuandaa masomo ya sayansi kwa vitendo.

Mkutano huu wa Baraza la Madiwani wa robo ya nne 2017/2018 umefanyika kwa mujibu wa sheria, kanuni za kudumu, na taratibu za uendeshaji wa serikali za mitaa.

HABARI PICHA

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga akisisitiza Jambo.
Mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Mufindi, Afisa Tarafa ya Malangali Bwana Daniel Dugange akitoa salamu za Mkuu wa Wilaya katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga.
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bwana Voster Mgina akitolea ufafanuzi jambo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga 
Diwani wa Kata ya Boma Mhe Julist Kisoma akiuliza swali katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga
Diwani Mhe Chesco Lyuvale akichangia katika moja ya agenda iliyokuwa inaendelea katika Mkutano wa Baraza la Madiwani
Diwani Mhe Denis Kutemile akiuliza swali wakati wa maswali ya papo kwa papo kwa Mwenyekiti wa Baraza la Madiwani  Halmashauri ya Mji Mafinga
Waheshimiwa Madiwani wakifuatilia kwa makini Mkutano wa Baraza la Madiwani wa Kwanza Kushoto ni Diwani wa kata ya Boma Mhe Damian Kyando naNyuma ni Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Mafinga.




Picha zote na Amani Mbwaga
Kwa Maoni au Ushauri Wasiliana nasi,
Mob:+255 656 632 566
E-mail:prof.mbwaga@gmail.com

Tuesday, August 21, 2018

Ziara ya Madiwani Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Halmashauri ya (W) Mufindi yakagua Miradi ya Maendeleo na Kuridhishwa nayo

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina akipampu maji katika kisima kinachotumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgalo Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi na Diwani Kata ya Sadani Mhe Ashery Mtono (Picha na Amani Mbwaga)
Na Amani Mbwaga, Mufindi
Ziara ya Waheshimiwa Madiwani Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Ikiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina Kukagua Miradi ya Maendeleo ikiwa ni Robo ya Nne 2017/2018

Kamati Imetembelea na Kukagua Miradi ya Ujenzi wa Madarasa 02 na Ukarabati wa Madarasa 04 katika Shule ya Sekondari Igombavanu.

Imetembelea na Kukagua Lambo la Maji lililojengwa kutokana na Juhudi za Wanufaika wa Mfuko wa TASAF Ambaposasa linatumika katika Shughuli za Kilimocha Umwagiliaji na Unyweshaji Mifugo katika Kata ya Igombavanu.

Aidha Kamati iikagua Mradi wa Ujenzi wa Hosteli ya Wasichana katika Shule ya  Sekondari ya Mgalo iliyopo kata ya Sadani ambayo Mpaka sasa imejengwa kwa nguvu za Wananchi na Mbunge wao.

HABARI PICHA
Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango Ikikagua Madarasa yaliyokarabatiwa na Serikali  tayari kwa matumizi ya Wanafunzi Katika Shule ya Sekondari Igombavanu


Madarasa  04 ya Shule ya Sekondari Igombavanu yaliyokarabatiwa na Serikali
Madarasa Mapya 02 yaliyojengwa na Serikali katika Shule ya Sekondari Igombavanu

Ukaguzi wa Choo cha Wanafunzi Kikikiwemo cha Walemavu Shule ya Sekondari Igombavanu


Lambo la Maji Lililopatikana kutokana na Juhudi za TASAF Ktika Kusaidia Kaya Masikini amblo linatumika katika Kilimo cha Umwagiliaji na Kunyweshea Mifugo Katika Kata ya Igombavanu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mwenyesuti akipokea Malezo ya Mradi kutoka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Igombavanu Katikakti ni Mratibu wa TASAF na Mwisho ni Makamu Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Mufindi

 
Mwenyekiti wa Kijiji cha Igombavanu aliyeinama chini akionesha shamba la Matikiti Maji Yanayolimwa  kutokana na Umwagiliaji wa Lambo la Maji


Afisa Mtendaji Kata ya Sadani (Kulia) Bwana Romanus Nyigo akitoa Taarifa ya Mradi wa Ujenzi wa Hosteli ya Shule ya Sekondari Mgalo Mbele ya Kamati ya Fedha na Mipango

Kamati Ikikagua Ujenzi wa Hosteli ya Wasichana Iliyojengwa kwa Nguvu za Wananchi Katika Shule ya Sekondari Mgalo


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina akipampu maji katika kisima kinachotumiwa na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mgalo Kulia kwake ni Afisa Elimu Sekondari Bwana John Lupenza


Picha zote na Amani Mbwaga

Mob:+255 656632566
E-mail:prof.mbwaga@gmail.com

Monday, August 20, 2018

PROF. SHEMDOE AKABIDHI MIKOBA YA UKURUGENZI HALMASHAURI YA MUFINDI.

Na Amani Mbwaga, Mufindi.
Hatimaye aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe, ambae kwa sasa ndiye Katibu Talawa wa Mkoa wa Ruvuma kufuatia uteuzi wa mkuu wa nchi, amekabidhi rasmi Ofisi na madaraka ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi kwa kaimu Mkurugenzi Ndugu. Isaya Mbenje, kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uongozi katika taasisi za umma.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika ofisini kwa Mkurugenzi mtendaji, Prof. Shemdoe, amewashukuru wakuu wa idara, vitengo na watumishi wote kwa ujumla ambao  walimsaidia kazi kwa juhudi maarifa na uaminifu jambo ambalo limesababisha aonekane na mamlaka za juu na hata kupata madaraka makubwa zaidi.
“Ninyi wakuu wa idara ndiyo mlioanifundisha kazi huku Serikali za mitaa, wakati nakuja huku nilikuwa sijui kitu, huku tofauti sana na  kule chuo kikuu nilikotoka, kule niljiua leo ninakipindi saa nne, nikitoka darasani najifungia kundika maandiko, ni kweli kwamba Mufindi ndiyo sehemu pekee ambayo kwa kiasi kikubwa nimejifunza uongozi hivyo, popote nitakapokuwa sitaisahau katika maisha yangu”
Aidha, Prof. Shemdoe, amewataka watumishi wa Halmashauri hiyo kutolinganisha uongozi wake na ule wa kaimu aliyemwanchia Ofisi wala kiongozi atakayeteuliwa rasmi kurithi nafasi yake na kusisitiza kuwa binadamu wanatofautiana na hata siku moja hawawezi kufanana kwa kila kitu kwani kila mmoja anamtazamo wake na namna yake ya kuongoza.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe. Jamhuri William, ambaye ndiye alikuwa mgeni wa heshima katika hafla hiyo, amempongeza  kwa uadilifu na utendaji mzuri wa kazi na akabainisha kuwa mara zote alitumia taaluma yake kama Profesa kutatua changamoto zilizokuwa zikijitokeza.
Hakika kulikuwa hakuna changamoto ambayo ilikuwa haipati utatuzi kwa Prof, alinisaidia sana kupata shuluhisho la mambo mengi hata kwa mambo yangu binafsi, alikuwa kiunganishi sahihi kati ya ofisi ya DC na Halmashauri ni katika kipindi chake uhusiano wa Ofisi hizi mbili ulikiwa imara zaidi, ungeweza kudhani Ofisi ya DC na Mkurugenzi ni moja.”Alisema  Mkuu wa Wilaya.
WASIFU. Prof. Riziki Shmdoe alizaliwa  Wilayani Lushoto Mkoani Tanga Mwaka 1974, alipata Shahada ya tatu ya  uzamivu PHD chuo kikuu cha Ghent kilichopo barani Ulaya Nchini Ubeligiji na kubobea kwenye taaluma ya (Applied Biological Sciences). Mwaka 2001 mpaka 2003 alisoma na kuhitimu shahada ya umahili (Masters) katika chuo kuu cha kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro akijikita kwenye (Management of Natural Resources For Sustainable Agriculture). Mwaka 1997 -2000 alisoma na kuhitimu Shahada ya kwanza ya taaluma ya Misitu katika chuo kikuu cha kilimo cha Sokoine  (SUA) Morogoro’
Aidha, 1994 – 1996 kidato cha 5 -6 Shule ya Sekondari SAME
1990 -1993: Kidato cha nne LWANDAME Sekondari
1983 – 1989: NGWERO Shule ya Msingi .
HABARI PICHA
Aliyekuwa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya Mufindi Prof. Riziki Shemdoe akiongea na Watumishi waliokuwa wakikshuhudia Makabidhiano ya Ofisi (Hawapo Pichani)

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Mhe Festo Mgina nae akisaini nyaraka za Makabidhiano ya Ofisi ya Mkurugenzi Mufindi (Picha zote na Ofisi ya Habari Mawasiliano naUhusiano).