Saturday, January 18, 2020

CGI Asikitishwa na Kifo cha Naibu Kamishna wa Uhamiaji

Dar es salaam.
Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania  (Air Tanzania)
Iliyotumika kusafirisha mwili wa Marehemu
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala amesikitishwa na kifo cha Naibu  Kamishna wa Uhamiaji (Mstaafu) DCI  Mwanakhamis Sheha aliyefariki mapema leo hii katika Hospitali kuu ya Taifa Muhimbili Jijini Dar ses salaam.

Dkt. Makakala akiwa na Maafisa Askari, Watumishi ndugu na jamaa wa Marehemu wameuaga mwili wa marehemu katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere( JNIA) tayari kwa kusafirishwa kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mazishi ambayo yatafanyika hapo kesho kuanzia muda wa saa 10:00 Asubuhi.

Aidha Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Makakala amekabidhi rambirambi ya Tsh. Milioni Moja na elfu hamsini kwa ndugu wa marehemu ikiwa ni ishara ya pole na kuthamini mchango mkubwa wakati wa uhai wake.

Akitoa neno wakati wa kuaga mwili wa marehemu, Dkt. Makakala alisema Taifa limepoteza mtu muhimu na makini sana kwani wakati wa uhai wake na kabla ya kustaafu kazi  marehemu alitekeleza majukumu yake ya Idara ya uhamiaji kwa weledi, uzalendo  na uhodari wa hali ya juu.

Bwana ametoa na Bwana Ametwaa Jina Lake Lihimidiwe

Ameni.

HABARI PICHA
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dtk. Anna Peter Makakala wa Kwanza (Kulia) akiwaongoza maafisa askari, watumishi wa umma, ndugu na jamaa kuaga mwili wa marehemu DCI  (Mstaafu) Mwanakhamis Sheha aliyefariki leo hii jijini Dar es salaam na mwili wake kusafirishwa Zanzibar kwa ajili ya Mazishi



Mwili wa Marehemu DCI Mstaafu Mwanakhamisi Sheha ukishushwa katika gari maalumu la kubebea maiti tayari kwa kuagwa na kusafirishwa na ndege kuelekea Zanzibar kwa ajili ya mazishi
Kamishna Jenerali Dkt. Anna Peter Makakala Kushoto akikabidhi Rambirambi kwa Wafiwa









Baadhi ya wanaosindikiza mwili wa marehemu wakiagana na CGI Dkt. Anna Peter Makakala katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa  Mwalimu Julius Nyerere (JNIA) (Picha zote na Kitengo cha Uhusiano Uhamiaji Makao Makuu)




No comments:

Post a Comment