Tuesday, July 31, 2018

“Serikali Kuajiri Waalimu 2000 wa Sayansi” Naibu Waziri (OR- TAMISEMI) Mhe Kakunda

Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe Joseph Kakunda akiongea na Wananchi wa Mdabulo (Picha na Amani Mbwaga)

Na Amani Mbwaga, Mafinga- Iringa
Naibu Waziri ofisi ya Rais (OR-TAMISEMI) Mhe Joseph Kakunda amesema serikali iko katika mchakato wa kuajiri waalimu 2000 wa masomo ya sayansi.

Ameyasema hayo alipokuwa katika ziara ya kikazi na kuoongea na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya Mufindi Kata ya Mdabulo katika viwanja vya shule ya Sekondari Mdabulo mara baada ya Mkuu wa shule kutoa changamoto ya uhaba wa waalimu wa sayansi katika shule hiyo.

Mhe Kakunda amewahakikishia Wazazi Waalimu na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mdabulo kuwa “Serikali kwa mwaka huu inaendelea na mchakato wa kuajiri waalimu wa sayansi wapatao 2000 hivyo taarifa yenu naichukua mwenyewe na kuipeleka kwa Mhe Waziri Jafo kumkumbusha,  kwa hiyo hao waalimu wawili 02 watapatikana tu hili nalibeba kwa ajili ya utekelezaji”

Aidha Mhe Kakunda ameridhishwa na miundo mbinu ya Shule hiyo ilivyojengwa kwa kuzingatia maelekezo ya kitaifa kwani kuna madarasa na mabweni mazuri hivyo amesisitiza utaratibu uliotumika wa kujenga kwa njia ya Force Account uendeleee hivyo hivyo hata wakati wa mradi wa ujenzi wa Bwalo la chakula utakavyoaanza ambapo serikali tayari imetenga Jumla ya Tsh Milioni 100 kwa shule ya Sekondari Mdabulo.

Kwa mujibu wa mkuu wa shule ya Sekondari Mdabulo Mwalimu George Mgomba, ameipongeza serikali ya awamu ya tano kwa kuwapatia Tsh milioni 259 kwa ajili ya upanuzi wa miundo mbinu ikiwemo ujenzi wa madarasa vyumba 04 kwa gharama ya Tsh milioni 80, ujenzi wa mabweni 02 yaliyogharimu Tsh milioni 150, Ujenzi wa vyoo Tsh milioni 11 na kuimarisha maabara kwa gharama ya Tsh Milioni 18.

Pamoja na fedha hizo Mwalimu Mgomba alisema anatumia fursa ile  kuwashukuru wachangiaji waliosaidia kukamilisha ujenzi kwa wakati, kwanza ni Halmashauri ya Wilaya Mufindi ambayo ilichangia msitu kwa ajili ya mbao, Rural Development Organization (O.R.D) ambao walitoa mashine za kuchanganyia zege kwa siku 30 bila malipo na kampuni ya china Civil Engineering Construction Cooperation (CCECC) walitoa malori amabayo yalibeba tripu 12 za mchanga bila malipo,  majengo hayo kwa sasa yanatumika toka Agosti 2017.

Shule ya Sekondari Mdabulo ilianzishwa rasmi mwaka 1984 ikiwa ni moja kati ya shule za wananchi wa Wilaya Mufindi, mwaka 1986 ilisajiliwa ikiwa miongoni mwa shule zinazomilikiwa na Mufindi Education Trust (MET)

Shule ya Sekondari Mdabulo ipo katika Wilaya ya Mufindi, Tarafa ya Ifwagi, Kata ya Mdabulo katika Kijiji cha Kidete umbali wa kilometa 45 kutoka makao makuu ya Wilaya Mufindi.

Shule hii ilikabidhiwa rasmi Serikalini mwaka 2003 kufuatia sera ya serikali ya kila Kata kuwa na Shule ya Sekondari, tangu mwaka huo mpaka sasa Shule imeendelea kujengwa na wananchi, wadau mbalimbali, Halmashauri ya Wilaya na Serikali kuu.


HABARI PICHA

Naibu Waziri Kakunda akisalimiana na Wazee waKijiji cha Mdabulo alipowasili Kijijini hapo katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mdabulo


Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mdabulo Wakimpokea Mhe Naibu Waziri Kakunda

Haya ni Madarasa yaliyojengwa zamani sana wakati shule ya sekondari Mdabulo ikianzishwa



Haya ni Madarasa Mapya yaliyojengwa hivi sasa kutoka fedha serikalini na kutumia mfumo wa "Force Account"





Naibu Waziri Kakunda akiongozwa na Mkuu wa Shule Mdabulo kuelekea Kukagua Maabara za Shule hiyo




Mmoja wa Wanafunzi wa Mdabulo Sekondari akitoa Maelezo kwa Naibu Waziri Kakunda Jinsi Mfumo wa umeme unavyofanya kazi katika Maabara ya Fizikia


Naibu Waziri Kakunda akipata maelezo kutoka kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mdabulo ndani ya Maabra ya Kemia.


Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Mdabulo akionesha mwili wa binadamu na sehemu zake katika Maabaya ya Baiolojia






Moja ya jengo jipya la Hosteli ya Wasichana iliyojengwa katika Shule ya Sekondari Mdabulo  kutoka fedha serikalini



Baadhi ya Wananchi wa Mdabulo waliohudhuria kumsikiliza Mhe Naibu Waziri Kakunda

Mkuu wa Shule ya Sekondari Mdabulo Mwalimu George Mgomba akisoma taarifa ya Shule kwa Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mh Kakunda

Mkuu wa Wilaya Mufindi Mh Jamhuri David William akiwasalimia Wananchi wa Mdabulo


Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini Mhe Menrad Kigola askiaslimia Wananchi wa Mdabulo


Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kaskazini Mh Mahamoud Mgimwa akisalimia Wananchi wa Jimbo lake Mdabulo nakueleza shida zao kwa Naibu Waziri  Mhe Kakunda

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEM Mhe Joseph Kakunda akiongea na Wanachi wa Mdabulo Wilayani Mufidi

Mwanafunzi Sarah Kangalawe akiimbisha wimbo wa Shule




Naibu Waziri Kakunda akiagana na aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mufindi Prof. Riziki S. Shemdoe ambaye sasa ni Katibu Tawala Mkoa Wa Ruvuma.

Naibu Waziri OR TAMISEMI Mhe Kakunda akiagana na Katibu Tawala Wilaya ya Mufindi Ndugu Benard Mwala




Naibu Waziri Kakunda akiagana na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mdabulo mara baada ya Kumaliza Ziara yake Shuleni hapo (Picha zote na Amani Mbwaga)

No comments:

Post a Comment