Thursday, November 15, 2018

TFS Saohill Yatembelewa na Wahasibu wa Kanda

Wahasibu Tfs Kanda  na Watumishi wa Shamba Sao Hill Wakifurahia Asali
Kwa Hisani ya Afisa Habari TFS - Sao Hill
Shamba la Miti Saohill Chini ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS mapema wiki hii imetembelewa na Wahasibu kutoka katika ofisi mbalimbali za Kanda (TFS) kwa lengo la kukagua, kujifunza na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na shamba la miti Sao Hill.

Wahasibu hao wamejifunza jinsi shamba linavyofaya kazi ikiwa ni pamoja na kufahamu changamoto za kila siku katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali kama vile ukusanyaji wa mapato na kuona namna malipo yanavyofanyika. 

Ugeni huo umetembelea maeneo mbalimbali ya shamba ikiwemo sehemu ya kuchakatia asali, Manzuki, bustani ya miti, (Miche) minara ya mawasiliano ya moto kuangalia zoezi la uvunaji wa miti na majaribio yanayoendelea ya uvunaji wa utomvu kutoka kwenye miti na maeneo mengine yenye vivutio vya utalii ndani ya shamba.

Shamba la miti Sao Hill ni la kwanza kwa ukubwa kati ya mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya Taifa. Kwa sehemu kubwa Shamba hili lipo katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na eneo dogo lipo katika mkoa wa Morogoro.

Shamba hili lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi 1951 na upandaji kwa kiwango kikubwa ulianza rasmi mwaka 1960 hadi 1980
                        HABARI PICHA
Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Herberth Haule aliyesimama akiongea na Wahasibu kutoka Kanda mabalimbali za TFS a baadhi ya watumishi wa Shamba hilo katika ukumbi wa mikutano uliopo makao makuu ya shamba Sao Hill










Meneja Tarafa ya kwanza  Irundi Bi Glory (aliyenyoosha mkono)  akionesha wageni  jinsi shamba linavyoonekana  katika moja ya mnara wa asili wa Mawasiliano (Watch Tower) kwa ajili ya ulinzi wa msitu endapo utavamiwa na moto sehemu yoyote ili ili kuchukua hatua yankudhibiti mapema 



Baadhi ya Mizinga ya Nyuki






Mmoja wa Wageni akichuguza kwa makini (Packaging)ya Asali ya Saohill



Mmoja wa Wa wageni akionja Asali tamu ya Saohill

Wahasibu wakiwa katika chumba cha kuchakatia Asali  ambapo wamepata maelezo kuhusu zoezi zima la uchakataji

Wageni mbalimbali na Watumishi  wa Shamba la Miti SaoHilll wakiongozwa na Afisa Nyuki wa Shamba hilo Bwana Said Aboubakar  wa kwanza kushoto waliochuchumaa wakifurahia Asali ya Saohill Honey yenye ubora wa kiwango cha juu (Picha zote na Afisa Habari TFS Sao Hill Mwanaisha Luhaga)

Wednesday, November 14, 2018

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Aoongoza Songambele ya Ukarabati wa Madarasa Shule ya Msingi Mamba na Kuokoa zaidi ya Milioni 4.


Na Amani Mbwaga, Mafinga.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga leo ameongoza wananchi katika shughuli za maendeleo ya kijiji cha Isalavanu katika ukarabati wa Shule ya Msingi Mamba iliyoko katika Kata ya Isalavanu Halmashauri ya Mji Mafinga M`koani Iringa.

Zaidi ya Milioni 4 zimeokolewa kwa siku moja kutokana na nguvu za Wananchi, Mchango wa Mhe Charles Makoga akishusha Mifuko 60 ya Cement yenye thamani ya Tsh 900,000/= na Mdau wa Maendeleo ambae ni Mkurugenzi wa Kituo cha Afya Tumain Jipya Dkt. Basil Tweve ambae amechangia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Milioni 4.

Mhe Makoga amewapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi hilo ambapo zaidi ya wananchi 300 wa kijiji cha Isalavanu wameshiriki katika ujenzi huo na kumtaka Afisa mtendaji wakijiji kuthaminisha nguvu ya wananchi kama Rais Dkt John Pombe Magufuli anavyotaka nguvu ya wananchi ithaminishwe na isomwe kwenye taarifa za mapato na matumizi ya kijiji na Shule hii ndio aliyoisoma Mhe Makoga.

“Wananchi ninawapongeza kwa mwitilio wenu na mmejenga wenyewe kwa nguvu zenu, naomba tumalizie jengo hili na tutahakikisha majengo yote yanapakwa rangi na tayari nimeshamwagiza Afisa Mipango Miji aje afanye tathimini hapa ya kazi iliyobakia ili serikali iweze kuwaletea fedha kama Milioni 10 hivi kwa sababau tayari mmeonesha nia” alisema Mhe Makoga  

Akisoma taarifa ya utekelezaji wa ujenzi huo kwa wananchi Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Isalavanu Bwana Noel Kabinda alisema wanachi wamejitokeza kwa wingi kutokana na uhamasishaji uliofanywa na Mhe Mwenyekiti wa Halmashauri yaMji Mafinga ambae ndie diwani wa kata hiyo ya Isalavanu, kutokanana na Mahafali ya darasa la saba lilipoibuka suala la ukarabati wa shule hiyo kupitia kwa aliyekuwa mgeni rasmi Dkt Basil Tweve.

Jumla ya vyumba 02 vya madarasa ofisi 01 ya waalimu, Jiko la Muda la Kupikia chakula cha wanafunzi shuleni, ujenzi wa vyoo vya wanafunzi vyenye matundu 14 vimekarabatiwa kwa siku moja, aidha oparesheni ondoa nyasi kwenye nyumba za waalimu imefanyika ili kuweka mazingira mazuri ya kuishi kwa waalimu wa shule hiyo.

Akitoa shukrani za pongezi kwa niaba ya Wananchi Mmoja wa wakazi wa kijiji cha Isalavanu ambae pia ni katibu wa Chama cha demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika Kata hiyo Bwana Fulgence Kadinde ambae pia alisoma shule hiyo toka mwaka 1981 hadi mwaka 1987 ameishukuru serikali chini ya Mhe Makoga kwa kushirikiana  kuhamasisha wananchi katika shughuli hizo za maendeleo.

“Maendeleo hayana chama  kwani leo wote tupo hapa bila kujali vyama vyetu katika shughuli za kuleta maendeleo yetu hasa katika ujenzi wa shule yetu hii ya msingi Mamba, nakupongeza kwa kutafuta wadau lakini pia ongeza badii ya kiutendaji na katika hili tunakusifu na tunakupenda sana maneno ya kisiasa tuyafunike endelea kupiga kazi” alisema Ndugu Kadinde

Kwa upande wake mmoja wa waalimu wakongwe na waanzilishi wa shule hiyo toka inafunguliwa rasmi mwaka 1977 akiwa Mwalimu Mkuu Msaidizi Mwl. Leonya Victory Kalinga amesema toka shule hiyo inaanzishwa hajawahi kuona mwitikio mkubwa wa wananchi katika shughuli za maendeleo ya ujenzi wa shule hiyo imekuwa historia kubwa katika kijiji hicho kuwahi kutokea.

Shule ya Msingi Mamba ilianzishwa rasmi mnamo tarehe 07 Novemba 1977 chini ya Mwalimu Mkuu wa Kwanza Mwl. Joseph Mbishi na inamilikiwa na Halmashauri ya Mji Mafinga Mkoani Iringa na ndio shule aliyoisoma Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe. Charles Makoga toka darasa la kwanza hadi hadi la saba.

HABARI PICHA








































Sunday, November 11, 2018

IHALIMBA MISITU FC NA IHEFU MISITU FC ZATINGA FAINALI

Na Amani Mbwaga, Mafinga,

Ihalimba Misitu FC
Ni katika mashindano ya Misitu Sports Bonanza yanayodhaminiwa na Wakala wa huduma za Misitu Tanzania (TFS) Shamba la miti Sao Hill ambayo yalifikiwa hatua ya nusu fainali iliyopigwa jana jumapili baada ya kuzikutanisha timu za Tarafa ya Kwanza hadi ya nne ambazo ni Ihalimba Misitu FC Vs Villa FC na Ihefu Misitu Vs Sawala FC.Katika mtanange wa kwanza ulizikutanisha Ihalimba Misitu Fc dhidi ya Villa Fc Ihalimba iliweza kuichabanga Villa Fc Mabao 4-1 Magoi yaliyofungwa na Zackaria, Melick, Issa na Stanley Wakati bao la kufutia machozi la Villa FC likifungwa na Joshua Kadinda.


Mchezo wa Pili ulizikutanisha timu za Ihefu Misitu Fc dhidi ya Sawala Fc mchezo huu uligubikwa na bonge la mvua mwanza wa mchezo hadi mwisho lakini pira uliendelea mpaka kipyenga cha mwisho kinapigwa Ihefu Misitu FC iliweza kuchomoza na ushindi wa mabao 2-0 amaao sawala hawakupata kitu mbali ya hapo waliambulia kadi nyekundu kwa beki wao mahili ajulikanae kwa jina la Tenende.
Hivyo basi kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Mshindano hayo ya Misitu Bonanza Shamba la Miti Sao Hill Bwana Saidi Aboubakar Amethibitisha kwamba Fainali ya mashindano hayo itapigwa siku ya Jumamosi ya Tarehe 17 Novema 2018 katika viwanja vya Misitu Makao makuu ya Shamba la Miti Sao Hill ambapo itazikutanisha timu za IHEFU MISITU FC kutoka Tarafa ya II Ihefu dhidi ya IHALIMBA FC kutoka Tarafa ya III na Mshindi atajinyakulia zawadi nono sana!
Aidha Bwana Said amewaomba wananchi wengi na wapenzi wa michezo kuweza kujitokeza kwa wingi kuja kushuhudia mtanange huo wa kukata na shoka, kwani siku hiyo mtoto hatumwi dukani.
Mashindano haya yamekuja kwa lengo la kuendelea kutoa elimu juu ya matumizi sahii ya moto dhidi ya mazingira na athari za uchomaji misitu, lakinin pia kuendelea kujenga mahusiano mazuri baina ya Shamba la Mti Sao Hill na Wananchi wanaolizunguka sanjari na Kurudisha shukrani kwa jamii (Corporate Social Responsibility)

HABARI PICHA
Ihalimba Misitu FC
Ihefu Misitu FC
Sawala FC





Villa FC



Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill wa Pili Kushoto  Bwana Haule akifuatilia kwa makini mtanange wa nusu fainali wa Misitu Sports Bonanza wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo na Afisa Nyuki wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Said Aboubakar wakiwa na viongozi wengine wa TFS Sao Hill



Mechi kati ya Ihefu Fc na Sawala Fc ikiendelea wakati mvua inanyesha

Ihefu Fc
Sawala Fc

Picha zote na Amani Mbwaga
Kwa Maoni au ushauri wasiliana nasi;
Mob:+255 656 632 566
E-mail:prof.mbwaga@gmail.com