Na Amani Mbwaga, Mafinga
Kamati ya bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii jana wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kukagua shughuli za utendaji kazi katika shamba la Misitu Sao Hill imeupongeza uongozi wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Shamba la miti Sao Hill kwa uzalendo wanaoonesha katika kulitumikia Taifa kwa maeneo yote walioyopangiwa kwani wanayasimamia kwa weledi wa hali ya juu.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Nape Nnauye alisema kamati yake imeridhishwa sana na kazi zinazofanywa na Wakala wa Huduma za misitu Tanzania kupitia Shamba la Miti Sao Hill ambao wanafanya kazi kwa viwango vya hali ya juu kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
“Kiukweli nikupongeze Menejea kwa namna mlivyojipanga, ukisoma taarifa na jinsi mlivyojipanga inaonekana nyinyi ni wazalendo haswaa na mnafanya kazi nzuri sana, kwa niaba ya kamati tunawatia moyo kwa hiyo muendelee na msimamo huo kulitumikia Taifa letu katika maeneo yote mliyopewa sisi tuna imani na nyie” Alisema Mhe. Nnauye.
Aidha Mhe. Nnauye alimhakikishia Mhe. Naibu Waziri kwamba kamati yake itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha kuhakikisha wizara inatimiza majukumu yake ipasavyo.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Constantine Kanyasu ameiagiza Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS kuongeza kitengo cha Intelejensia ambacho watakisambaza katika maeneo yote ya Hifadhi za Misitu ambayo yanapakana na wananchi ili kupata taarifa za kina kutoka kwa wananchi juu ya nini wanawaza kuhusu mashamba hayo, lengo kuu ni kuondoa kabisa tatizo la uchomaji moto katika mashamba ya miti ya serikali ambayo wakati mwingine inasababishwa na hujuma tu za mtu lakini pia kuongeza ulinzi wa rasilimali hizo muhimu kwa Taifa kwa kuishirikisha jamii ipasavyo ili waione kama mali yao.
“Niseme tu bila kuwepo TFS sasa hivi tungekuwa tunazungumzia habari nyingine kwa upande wa Misitu” Alisema Mhe. Kanyasu
Hata hivyo Mtendaji Mkuu wa wakala wa huduma za Misitu Tanzania TFS Profesa Dos Santos Silayo alisema kwa sasa serikali kupitia TFS ina mashamba makubwa ya kupandwa 23 na mwaka huu 2019 litafunguliwa shamba lingine la 24 katika eneo la kisiwani katika Mkoa wa Mtwara Wilaya ya Mikindani .
“Tunapanua wigo katika maeneo mbalimbali na iwe kama darasa kwani tunawafundisha wananchi kwamba miti inaweza ikapandwa, ikalelewa na kuwa zao la kiuchumi kwa Taifa na Dunia kwa ujumla” Alisema Profesa Silayo.
Akieleza Mchango wa shamba kwa jamii na uchumi wa Taifa Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Heriberth Haule alisema Shamba hilo limekusanya zaidi ya Bilioni 319 kama maduhuli ya serikali kuu kwa kipindi cha miaka 10 na Tsh Bilioni 6 kama CESS Kwa Halmashauri za Wilaya Mufindi, Mji Mafinga na Kilombero.
Aidha Shamba huchangia pia katika kurudisha shukrani kwa jamii inayolizunguka yaani Corporate Social Responsibility (CSR) kwa kila mwaka, kupitia michezo, ujenzi wa barabara, madawati na kuchangia huduma nyingine nyingi za jamii.
Shamba la Miti Sao Hill ni Miongoni mwa Mashamba 23 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Shamba hili kwa sehemu kubwa lipo katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na Kwa sehemu ndogo Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro.
|
Kushoto ni Mlurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Saada Mwaruka akiwa na Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Mufindi Bwana Mchina wakifuatilia kwa makini taarifa ya meneja wa shamba la miti Sao Hill mbele ya kamati ya Bunge |
|
Baadhi ya Watendaji wa TFS Sao Hill Wakiwa katika Picha ya pamoja |
|
Baadhi ya Watendaji wa TFS Shamba la Miti Sao Hill wa kwanza kushoto i Meneja wa Shamba hilo Bwana Herberth Haule |
|
Baadhi ya Miti ya Mikaratusi Inayolimwa na Shamba la Miti Sao Hill |
|
Kamati ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii wakipata maelezo ya Shamba la Miti aina ya Mikaratusi iliyoboreshwa na inayokuwa kwa muda mfupi katika Tarafa ya Tatu Ihalimba ya Shamba hilo |
|
Kushoto ni Mbunge na Mjumbe wa Kamati Mhe Magdalena Sakaya akiuliza swali |
|
Meneja wa Tarafa ya Tatu Ihalimba Shamba la Miti Sao Hill Bwana Mshana akitoa maelezo ya Shamba kwa kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii |
|
Mmoja wa Wajumbe wa Kamati ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii akiuliza swali ili kupata ufafanuzi wa aina ya miti iliyopandwa katika shamba la miti Sao Hill |
|
Mtendaji Mkuu TFS Prof. Silayo pembeni yake ni Meneja wa Shamba la Miti Sao Hill wakisikiliza maoni ya Kamati ya Bunge |
|
Mwenyekiti wa Kamti ya Bunge Ardhi Maliasili nna Utalii Mhe Nape akiangalia jinsi Utomvu Unavyovunwa katika Miti ya Shamba la miti Sao Hill ikiwa bado katika majaribio |
|
Mtendaji Mkuu Prof. Silayo Akitoa maelezo ya jinsi Miti inavyovunwa Utomvu katika shamba la Miti Sao Hill |
|
Mjumbe wa Kamati hiyo na Mbunge wa Iringa Mjini Mhe. Mchungaji Peter Msigwa akiangalia kwa makini jinsi Utomvu unavyovunwa katika shamba la Miti Sao hill |
|
Miti inayovunwa utomvu kwa majaribio katika Shamba la Miti SaoHill |
|
Mkurugenzi wa Misitu na Nyuki TFS Dkt Mwakalukwa akiwa katika shamba linaovunwa Utomvu Sao Hill wakati kamati ya Bunge ilipotembelea shamba hilo |
|
Menyekiti wa Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii Mhe Nape Nnauye akisalimiana na AfisaNyuki wa Shamba la Miti Sao hill Bwana Saidi Aboubakar wakati wa Kutembelea Shughuli za Ufugaji Nyukin katk Shamba hilo. |
|
Afisa Nyuki Bwana Said Aboubaka akitoa Maelezo Ndani ya Kiwanda kidogo cha kuchakata Asali mbeleya Kamati ya Bunge |
|
Mwenyekiti Kamati ya Bunge Mhe. Nape na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Kanyasu wakiwa katika Picha ya Pamoja na Wadau wa Mazao ya Misitu na Walinzi wa Shamba la Miti Sao Hill |
|
Picha ya Pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya Mufindi |
|
Picha ya Pamoja Kamati ya Bunge Ardhi Maliasili na Utalii na Watendaji wa TFS Shamba la Miti Sao Hill (Picha zote na Amani Mbwaga) |