Monday, February 25, 2019
Saturday, February 23, 2019
Sunday, February 17, 2019
Mbunge Chumi Akabidhi Magari 02 Bure kwa Idara ya Elimu Mafinga
Na
Amani Mbwaga, Mafinga.
Mbunge wa Jimbo la
Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi Mapema wiki hii amekabidhi Magari idadi mawili
kwa Idara ya elimu katika Halmashauri ya Mji Mafinga kwa lengo la kuongeza
nguvu ya ufuatiliaji wa masuala ya elimu ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi
na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa Jimbo la Mafinga Mjini na Taifa kwa ujumla.
Hafla ya
makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Teachers Resource Centre (TRC
Mafinga) wakati wa mkutano wa tathimini ya Elimu kwa Halmashauri ya Mji Mafinga
ambapo umewakutanisha takribani waalimu wakuu wa shule zote za Sekondari na Msingi,
Maafisa Elmu kata, Wilaya na Wataalamu wengine wote wa Sekta ya Elimu Mjini
Mafinga.
Akiongea na
Wataalamu hao wa elimu Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi
ameelezea hisia zake juu ya umuhimu wa elimu kwa wananchi wa Jimbo lake na taifa
kwa ujumla.
“Mimi
naamini kwamba elimu ndio kila kitu bila elimu tusingekuwa hapa kwa hiyo
tunapokaa kufanya tathimini ya elimu tunapanga ili kuboresha elimu ya watoto
wetu” alisema
Aidha ameeleza kuwa
Halmashauri ya mji mafinga bado ni changa na ilianzishwa hivi karibuni kwa hiyo
idara nyingi zina uhaba wa magari kwa hiyo yeye kama mbunge ameamua kujiongeza
kutafuta wadau wakamsaidia magari hayo mawili ambayo ameyakabidhi kwa idara ya
elimu Msingi na Sekondari.
Kwa Mujibu wa Mhe.
Chumi amesema kwamba magari hayo amepewa na Kamishina wa Ushuru na Forodha wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kumsumbua sana ili amsaidie magari kwa ajili
ya idara za halmashauri yake na ndipo kamishina huyo akampatia magari hayo na
leo ameikabidhi Halmshauri Kupitia Mkuu wa Wilaya Mufindi na baade kumkabidhi
Mwenyekiti wa Halmashari ya Mji Mafinga tayari kwa matumizi ya kiserikali
hususani idara ya elimu.
Akitoa shukrani kwa
Mbunge huyo Mgeni wa rasmi wa hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri
William amempongeza Mhe. Chumi kwa kulipigania jimbo la Mafinga mjini katika
kuhakikisha maendleo yanapatikana kwani amekuwa msaada mkubwa sana.
“Leo
hii tumepokea magari mazuri halafu mapya kabisa yaliyotokana na jitihada za
mbunge wetu Chumi, mimi kipekee nakushukuru sana naomba upeleke shukrani na
salamu zetu kama Wilaya kwa wadau wote waliojitolea upatikanaji wa magari haya”
alisema
Mhe. William
amemhakikishia Mhe. Mbunge Chumi kuwa magari hayo yatatunzwa kwa kuzingatia
kanuni na taratibu zote za utunzaji wa magari ya serikali na kutumika kwa shughuli
za serikali hususani shughuli za elimu tu.
Hapo awali kulikuwa
kunachangamoto ya shule nyingi kutofanyiwa ukaguzi na idara ya udhibiti
ubora elimu kutokana na ukosefu na uhaba
wa usafiri sasa kupatikana kwa magari haya ni wakati muafaka wa kuhakikisha
hakuna tena tatizo la ufuatiliaji wa elimu Mafinga Mjini.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe. Charles Makoga amesema Mhe.
Mbunge Chumi amekuwa akisaidia sana katika upatikanaji wa vifaa mbalimbali toka
ameingia ubunge kwa muda mfupi amechangia upatikanaji wa magari ya kubebea Wagonjwa
(Ambulance) takribani manne sasa katika Halmshauri hiyo lakini pia alipigani
pia kupatikana kwa gari la TASAF na la udhibiti ubora yote mapya ambayo
yamepatikana pia hivi karibuni.
“Mhe
Mbunge mimi nikushukuru sana na mungu akubariki sana kwa upendo wako mkubwa kwa
wananchi wa Mafinga kama Mungu hua anapunguza miaka basi kwangu apunguze miwili
tu akuongezee wewe” alisema Mhe. Makoga.
Akieleza lengo la
tathimini ya elimu ya mwaka 2018 hasa katika matokeo ya mitihani ya kitaifa
Kaimu Mkurugenzi na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bwana
Voster Mgina amesema tathimini hiyo itachangia kupanga mipango madhubuti ya
mwaka 2019.
Matokeo ya mitihani
ya Taifa kwa mwaka 2018 Halmashauri ya Mji Mafinga ilifanya vizuri sana katika
mitihani yote.
Mtihani wa darasa la
saba Halmashauri ya Mji Mafinga iliweza kufaulisha kwa kiwango cha asilimia
92.86%
Mtihani wa Kidato
cha pili ufaulu ulikuwa wa kiwango cha asilimia 96% na kidato cha nne ufaulu
ulikuwa wa kiwango cha asilimia 87 wakati huo mwaka jana ufaulu ulikuwa
asilimia 73% lakini mwaka huu shule zote zimepandisha ufaulu na zimeweza kupunguza daraja 0 kutoka 350
hadi 176.
Aidha kidato cha
sita kwa matokeo ya mwaka 2018 Halmashauri ya Mji Mafinga iliweza kufaulisha
kwa kiwango cha asilimia 100% na hakukua na mwanafunzi aliyepata daraja la 0
wala daraja la IV kwa shule zote za serikali
na binafsi.
HABARI PICHA
Magari aliyoyatoa Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe Cosato Chumi kwa Idara za Elimu Mafinga Mji |
Mhe. Charles Makoga akitoa Shukrani |
Thursday, February 14, 2019
Zaidi ya Bilioni 25 .2 za Bajeti ya 2019/2020 zapitishwa na Baraza la Madiwani Halmashauri ya Mji Mafinga
Mkutano maalumu wa
baraza la madiwani la Halmashauri ya Mji
Mafinga leo limepitisha rasimu ya mpango wa bajeti ya kipindi cha mwaka wa
fedha 2019/2020 na kuidhinisha kukusanya
na kutumia zaidi ya Bilioni 25.2 kwa ajili ya matumizi ya
mishahara, mengineyo na miradi ya maendeleo.
Akisoma rasimu hiyo
kwa niaba ya Mkurugenzi, Afisa Mipango wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bwana
Andambikye Kyomo amesema zaidi ya Bilioni 3.9 zinakadiriwa kukusanywa kutokana
na vyanzo mbalimbali vya mapato ndani ya Halmashauri.
Makisio hayo ni zaidi
ya milioni 648.8 ambayo ni asilimia 20% ukilinganisha na makisio ya mwaka
2018/2019 ya zaidi ya Tsh Bilioni 3.3, aidha katika mapato hayo kiasi cha zaidi
ya Tsh milioni 602.8 ni mapato ya vyanzo fungiwa katika idara ya afya na elimu
sekondari hivyo kufikia mapato halisi kuwa zaidi ya Bilioni 3.3.
Baraza hilo
limeridhia pia matumizi ya kawaida kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo zaidi ya
Bilioni 17.8 zimeidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kawaida na mishahara ,
kati ya fedha hizo kiasi cha zaidi ya Tsh Bilioni 13.8 ni kwa ajili ya mishahara, na
zaidi ya Bilioni 4 ni kwa ajili ya
matumizi mengineyo.
Aidha baraza hilo
limeidhinisha pia kukusanya na kutumia zaidi ya Bilioni 7.3 kwa ajili ya
kutekeleza miradi ya maendeleo kutoka vyanzo mbalimbali vya mapato kati ya
fedha hizo zaidi ya bilioni 4.7 ni kutoka ruzuku ya serikali kuu, wahisani zaidi
ya milioni 490, Halmashauri inatarajia kuchangia zaidi ya Bilioni 1.3 sawa na
asilimia 40% ya mapato halisi ya ndani ya Halmashauro na nguvu ya wananchi wanatarajia
kuchangia zaidi ya milioni 768.
Akieleza matarajio
ya utekelezaji wa rasimu ya bajeti hiyo ya 2019/2020 Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Mji Mafinga Bwana Voster Mgina ametanabaisha kwamba bajeti hiyo italenga
kuimarisha mifumo ya ukusanyaji na kuongeza mapato ya ndani, kuongeza viwanda
na fursa za uwekezaji, kuboresha huduma za usafi katika mji, kuboresha makazi
na mipango miji sanjari na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi na vitendea
kazi na hatimae kukamilisha miradi viporo iliyoanzishwa siku nyingi katika
sekta ya afya, elimu utawala na ujenzi.
Akiongoza baraza
hilo Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe. Charles Makoga amewahakikishia
wananchi wa Mafinga kwamba bajeti hiyo iliyoidhinishwa leo hii itaenda kutekelezwa
ipasavyo na imelenga kutatua kero za wananchi.
“Sisi
kama watekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi wote kwa pamoja kwa
kushirikiana na madiwani wa chadema kwa pamoja tunashirikiana kuhakikisha
bajeti hii inaenda kutekelezwa katika kata zetu zote kama iliyopangwa bila
kujali vyama vyetu kwani maendeleo hayana chama”
Alisema
Aidha ameeleza
kwamba katika kuendelea kuunga mkono juhudi za Mhe. Rais Dkt John Magufuli za kuleta
elimu bure na matokeo chanya yanayotokea ya ongezeko la wanafunzi, Halmashauri
yake imejiandaa kuongeza kujenga shule mbili za Sekondari mpya ikiwemo ya
vipaji maalumu na nyingine ya Wasichana itakayojulikana kwa jina la Mafinga
Girls hii ni kutokana na ongezeko la ufaulu wa mtihani wa darasa la saba ambapo
halmashauri hiyo imefikia asilimia 92.86% ya ufaulu kwa mwaka 2018 na kushika
nafasi ya kwanza katika mkoa wa Iringa.
Kwa upande wake mwakilishi
wa Mkuu wa Wilaya Mufindi Kaimu Katibu Tawala (DAS) Bwana Joseph Mchina
ameipongeza Halmashauri ya mji wa Mafinga kwa kuwa na usimamizi mzuri wa
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
“Waheshimiwa
Madiwani endeleeni kushirikiana na wataalamu hawa wa Halmashauri na wananchi
kwa ujumla katika kufanikisha utekelezaji wa miradi yetu kwa viwango vyenye
ubora unaotakiwa ambavyo thamani yake ya fedha inaonekana ili kuchochea
maendeleo ya wananchi na kufikia kipato cha kati kwa manufaa ya sasa na ya kizazi
kijacho” Alisema.
Mapendekezo ya
Bajeti ya mwaka 2019/2020 yameandaliwa kwa kuzingatia mambo yafuatayo, Muongozo
wa Bajeti wa 2019/2020, Ilani ya Uchaguzi ya chama Tawala –Ccm ya 2015/2016
-2019/2020, Malengo ya Maendeleo endelevu (SDGs), Dira ya Taifa ya maendeleo
2025, Maelekezo ya Ki- Sekta na Mpango wa maendeleo wa miaka mitano na mpango
mkakati wa Halmashauri pamoja na vipaumbele vya Taifa kama vilivyofafanuliwa na
Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa
kufunga bunge la 11 Mjini Dodoma.
Vilevile umezingatia mwongozo wa Serikali wa kuandaa mipango na Bajeti wa mwaka 2019/2020 uliotolewa na Wizara ya Fedha na Mipango mwezi Disemba 2018 ikiwa ni utekelezaji wa sheria ya Bajeti Namba 11 ya mwaka 2015 sehemu ya 21 na 22.
HABARI PICHA
Tuesday, February 12, 2019
Friday, February 8, 2019
Wednesday, February 6, 2019
Saturday, February 2, 2019
Friday, February 1, 2019
Halmashauri ya Mji Mafinga Yazindua Kampeni ya Upandaji Miti Katika Vyanzo vya Maji.
Na
Amani Mbwaga, Mafinga.
Halmshauri
ya Mji Mafinga jana imezindua kampeni ya upandaji miti aina ya Mivengi katika
chanzo cha maji eneo la Makamadolesi kata ya Changarawe Wilayani Mufindi Mkoani
Iringa, uzinduzi huo umeoongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Mhe. Charles
Makoga akimwakilisha Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri William.
Kwa kuzingatia
mabadiliko ya tabia ya nchi yanayosababaishwa na shughuli za kibinadamu za
uvunnaji wa mazao ya misitu na kilimo kisichofuata hifadhi ya mazingira na
vyanzo vya maji serikali iliamua kutenga tarehe mosi Aprili ya kila mwaka kuwa
siku maalumu ya upandaji miti kitaifa.
Kampeni hiyo mwaka
huu inaenda na kaulimbiu ya “Panda miti
hifadhi Mazingira na Vyazo vya maji kwa vizazi vya sasa na vya baadae”
Hata hivyo kwa
kuzingatia tofauti ya majira ya misimu ya mvua kuanza na kuisha katika maeneo
haya, Mkoa wa Iringa ulipanga uzinduzi wa upandaji wa miti katika maeneo yote ya
mkoa kufanyika mwezi Januari kila mwaka.
“Leo
hii ni siku muhimu kwetu kwani inaelenga kukumbushana na kuelimishana juu ya
umuhimu wa kuhifadhi na kutunza mazingira kwa manufaa ya sasa na vizazi vijavyo”
alisema
Mhe. Makoga.
Ameendelea
kusisitiza kwamba uhaba wa upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi wa
mijini na vijijini aidha uharibifu wa vyanzo vya maji ni kero kubwa, na mfumo
wa maji ni miongoni mwa changamoto za
mazingira zinazoendelea kulikumba taifa .
Pamoja na juhudi
zinazochukuliwa na serikali katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira ni
muhimu ifahamike kwamba mazingira ni sehemu ya maisha ya binadamu na ndio uhai
wa viumbe, Maisha ya binadamu yanategemea ardhi, maji, mimea na hewa.
“Takwimu
za hivi karibuni za sensa ya miti zinaonesha wazi kwamba idadi inapungua sana
takribani hekta zaidi ya 270,000 hadi 300,000 zinapungua kutokana na ukataji miti
hovyo na uchomaji mkaa” alisema.
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi. Saada Mwaruka alisema Halmashauri
yake imeandaa jumla ya miche 15,039 ambapo miche 5,000 ni pine na miche 5200 ni
miti rafiki na maji (Mivengi), miche ya matunda parachichi 1,118, miche ya
mapambo na vivuli 1400.
“Lengo
la kupanda miche ya aina hii ni kwa ajili ya kuhifadhi mazingira kupendezesha maeneo
ya wazi kuhifadhi vyanzo vya maji na kuimarisha mipaka ya maeneo mbalimbali”
alisema.
Akisoma taarifa ya
uzinduzi kwa mgeni rasmi Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bwana
Charles Tuyi alisema halmashauri hiyo imefanikiwa sana kwa upandaji wa miti
kutokana na kuwa katika ukanda unaokubali mazao ya kilimo cha miti wananchi
wake wanazidi kuhamasika kwani kila mwaka kwani takwimu za upandaji zimekuwa
zikizidi kuongezeka.
Licha ya mafanikio
hayo Halmashauri hiyo bado inakumbwa na changamoto lukuki katika uhifadhi wa
mazingira ikiwemo kuendelea kutokea kwa matukio ya moto kichaa unaoathiri
misitu ya asili na ile ya kupandwa, uvamizi wa misitu na vyanzo vya maji
kutokana na shughuli za kibinadamu, kukosekana takwimu halisi za miti
iliyovunwa hasa miti michanga, uhaba wa wataalamu na vijiji vingi kutokuwa na
mipango ya matumizi bora ya ardhi inayopelekea migogoro ya ardhi kutokea.
Bwana Tuyi ameeleza
kwamba kutokana na changamoto hizo Halmashauri ya Mji Mafinga imeendelea
kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kuwa na kampeni ya utoaji elimu juu ya
udhibiti mioto jamii kwa kushirikiana na wakala wa huduma za misitu Tanzania
TFS-Shamba la Miti Sao Hill ambapo kila mwaka elimu hiyo hutolea na kuunda
vikosi maalumu vya kudhibiti moto.
Mbali na hayo Halmashauri
imeendelea kusimamia sheria ndogo za mazingira, kushawishi wizara ya maliasili
na utalii kuimarisha na kusimamia matumizi ya mfumo wa viwango (Standards)
sahihi katika biashara ya mazao ya misitu ili kudhibiti uvunaji holela wa miti
michanga.
Kwa upande wake
Afisa Misitu wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bwana Peter Kibona amesema lengo kuu
la halmashauri hiyo kwa mwaka 2019 ni kuotesha miche Milioni 1 na laki tano,
hadi sasa zaidi ya miche milioni 1
imepandwa katika maeneo mbalimbali na upandaji bado unaendeelea.
Kwa kipindi cha
mwaka 2016 hadi sasa Halmashauri ya Mji Mafinga imepanda zaidi ya hekta 8,652.1
za miti.
Aidha Halmashauri
hiyo imeanzisha vitalu vya miti ya aina mbalimbali ili kuweza kuhudumia
wananchi kwa kuwagawia miti bure ili kuwapatia motisha katika upandaji miti na uendelezaji wa miti hiyo kwa ajili ya
mazao ya misitu kwa faida ya vizazi vya
sasa na baadae.
Subscribe to:
Posts (Atom)