Tuesday, December 31, 2019
Wednesday, September 11, 2019
Friday, September 6, 2019
Thursday, September 5, 2019
Tuesday, September 3, 2019
Monday, September 2, 2019
Thursday, August 29, 2019
Wednesday, August 28, 2019
Tuesday, August 27, 2019
Monday, August 26, 2019
Friday, August 23, 2019
Tuesday, August 20, 2019
Thursday, August 8, 2019
Tuesday, August 6, 2019
Saturday, August 3, 2019
Thursday, August 1, 2019
Tuesday, July 30, 2019
Friday, July 26, 2019
Thursday, July 25, 2019
Saturday, July 20, 2019
Thursday, July 18, 2019
Tuesday, July 16, 2019
Waziri Bashungwa Azindua ligi ya Mpira wa Miguu Karagwe
Na Amani Mbwaga, Karagwe
Waziri wa Viwanda na Biashara ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mkoani Kagera Mhe. Innocent Bashungwa Mapema Wikendi iliyopita amezindua rasmi Mashindano ya ligi ya mpira wa miguu ambayo hufanyika kila mwaka Jimboni kwake na ni maarufu kwa BASHUNGWA KARAGWE CUP.
Akiongea na Wananchi katika kijiji cha Nyakagoyagoye Wilayani Karagwe wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo Waziri Bashungwa amesema wananchi wanapoendelea kuchapa kazi serikali nayo inaendelea kuleta huduma za jamii katika maeneo yote mijini na vijijini.
“Wana Karagwe Chapeni Kazi lakini sisi kwenye huduma za jamii suala la maji mlikuwa mkisikia nikiwa bungeni nazungumzia mradi wa maji mpaka koo linakauka, lakini huo mradi ndugu zangu ni mkubwa sana na uko katika hatua nzuri na hivi ninavyozungumza Waziri wa maji alikuwa hapa Karagwe jana kuhakikisha mradi huo unatekelezwa ipasavyo” alisema
Wakati huo huo Waziri Bashungwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kupeleka miradi mingi na mikubwa Wilayani Karagwe ambapo hivi karibuni tu Zaidi ya Bilioni 70 zitapelekwa tena katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kuchochea miradi mingine ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya Karagwe Mhe. Godfrey Mhehuka amempongeza waziri Bashungwa kwa kuchapa kazi na hatimae wana karagwe wanafurahia maendeleo yanayopatikana ktokana na juhudi zake.
“Niemona niseme pongezi zangu kwako, umati huu ni mkubwa sana na unaona ni kwa sababu wewe umeamua kufanya kitu.
Aidha. Mhe Mheuka ameendelea kusema rais hakukosea kumchagua kuwa waziri wa viwanda na biashara hivyo amemuomba akachape kazi na wao wako nyuma yake kuhakikisha anawatumikia vyema wananchi wa Karagwe na Taifa kwa ujumla.
“Niseme neno moja
tu, Mungu ametuona, nataka niwape siri hakika mungu amewaona DC Mwenye Waziri
Mkoa wa Kagera niko peke yangu ahsanteni sana”alisema Mhe. Mheuka
Kwa mujibu wa
mratibu wa mashindano ya BASHUNGWA KARAGWE CUP Bwana Majaliwa Said amesema Mashindano hayo yameanza tarehe
13 Julai 2019 yakihusisha timu kutoka kata zote 23 za Halmashauri ya Wilaya Karagwe.
HABARI PICHA
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (Kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya Karagwe Mhe.Godgrey Mhehuka katikati ni Katibu wa CCM wilaya ya Karagwe Bi. Mary Kananda |
Pichani, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa wa (tatu kushoto) akiwa pamoja na moja ya Timu iliyozindua mchezo wa kwanza wa ligi ya Bashungwa Karagwe Cup |
Waamuzi na Ma Kapteni wa Timu |
Baadhi ya Wananchi waliofika Kuhudhuria Uzinduzi wa Bashungwa Karagwe Cup Wkifuatilia kwa Makini Mchezo unaoendelea |
Mratibu wa Mashindano ya BASHUNGWA KARAGWE CUP Bwana Majaliwa Said akitoa Taarifa ya Mashindano kwa Waziri wa Viwanda na Biashara (Mbunge Karagwe) |
Thursday, July 11, 2019
Wednesday, July 10, 2019
Monday, July 8, 2019
Sunday, July 7, 2019
Friday, July 5, 2019
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Bashungwa Afanya ziara katika Viwanda vya nguo na Kutatua kero zao
Na
Amani Mbwaga, Dar es salaam
Waziri wa viwanda
na Biashara nchini Tanzania Mhe. Innocent Bashungwa Mapema leo hii amefanya
ziara katika viwanda vya nguo kikiwemo cha NIDA na kile cha NAMERA vya jijini Dar es salaam.
Akiongea mara baada
ya kutembelea viwanda hivyo Mhe. Bashungwa amesema lengo la ziara hiyo ni
kupita katika viwanda vyote vya nguo nchini kujua changamoto zao na kisha
serikali kuzifanyia kazi na hatimae kuwa na uzalishaji endelevu wa zao la pamba na kuwanufaisha wakulima.
“Mimi nimekuja hapa
kwa ziara mahususi, Wakulima wetu wa pamba wamehamasika sana kulima pamba,
Msimu huu wa mwaka 2019 tunategemea kuvuna
zaidi ya Tani Laki 4 za pamba kutoka tani Laki 220,000 za mwaka jana kwa
hiyo tuna pamba za kutosha” alisema Mhe.
Bashungwa.
Aidha amesisitiza
kwamba wakulima kwa upande wao wametimiza wajibu wao hivyo ni jukumu la
Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara kuwatafutia masoko yenye tija.
“Kwa muda mrefu
soko la pamba limekuwa likitegemea mlango mmoja tu, wakati wa enzi za Baba wa
Taifa Mwl. Julius Nyerere kulikuwa na viwanda vingi vya nguo na vilikuwa
vinafanya kazi ipasavyo na kama vyote vingekuwepo basi kusingekuwepo na
changamoto ya masoko katika zao la pamba hivyo ni wakati sasa wa viwanda vilivyopo na
vitakavyojengwa kuhakikisha vinafanya kazi ipasavyo na Kuongeza Uzalishaji mara mbili zaidi ili kuendana na kasi ya sasa
ya Tanzania ya Viwanda".
Nchi ikifanikiwa kuchakata
kila zao na kuliongezea thamani basi itakua ni chachu ya ongezeko la
ajira hapa nchini na hatimae kukuza uchumi wa
taifa na wananchi kwa ujumla.
Dira kuu ya Wizara ya Viwanda na Biashara
ni "Kuwa na msingi shindani wa viwanda, mazingira bora ya uwekezaji
na ukuaji wa biashara unaowezesha kukua kwa uchumi shirikishi na
endelevu."
Waziri Bashungwa
ataendelea na ziara hiyo nchi nzima baada ya Kuanza na Mkoa wa Kilimanjaro hapo
jana na leo hapa Jijini Dar es salaam.
MATUKIO KATIKA PICHA
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akiangalia Bidhaa zinazotengenezwa na Kiwanda cha Nguo NIDA Wakati wa ziara yake.
|
Pamba ikiwa katika Hatua za awali za uchakataji |
Waziri wa Viwanda na Biashara (Katikati) akipokea maelezo ya namna Pamba inavyoanza kuchakatwa katika hatua za awali |
Shughuli za Uzalishaji Kiwandani zikiendelea |
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (Kulia) akimsikiliza kwa Makini Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Nguo NIDA na NAMERA (Picha zote na Amani Mbwaga) |
Monday, July 1, 2019
Sunday, June 30, 2019
Bodi ya Ushauri ya Wizara kwa TFS Yapongeza Juhudi za Uendelezaji Shamba la Miti Sao Hill Mafinga
Na Amani Mbwaga, Mafinga
Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imefanya ziara hivi karibuni katika Shamba la Miti Sao Hill ikiwa ni lengo la kujitambulisha kwa wajumbe wa bodi hiyo lakini pia kuona shughuli mbalimbali zinazosimamiwa na Wakala.
Akiongoza wajumbe wa Bodi hiyo Bi. Piencia Kiure mara baada ya kupokea taarifa ya utendaji kazi Shamba la Miti Sao Hill na kutembelea baadhi ya miradi na amepongeza juhudi hizo na kusema toka ameanza ziara hiyo katika maeneo mbalimbali ya Nyanda za Juu Kusini lakini Shamba la Miti Sao Hill ni mfano wa kuigwa kwa utendaji bora na uliotukuka.
“Nimefurahi sana taarifa zenu ni nzuri sana na pia nimeona jinsi mnavyotekeleza suala la wajibu kwa jamii yaani Corporate Social Responsibility (CSR) ikiwepo kutenga fedha kwenye bajeti yenu katika miradi ya maendeleo vijijini hapa mmenikuna zaidi kwani na mie ni mdau mkubwa sana wa (CSR) Na kwa kufanya hivyo kunasaidia sana kuwa na mahusiano mazuri baina yenu na jamii inayozunguka shamba hongereni sana”.
Kwa upande mwingine Bi. Kiure ameitaka Shamba la Miti Sao Hill Kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Kuendelea na juhudi za Ujenzi wa Viwanda hasa vya mazao ya nyuki kwani shamba hilo limefanikiwa sana katika shughuli za ufugaji nyuki na kuwa na vifaa vya kisasa vya ufugaji nyuki na vile vya kuchakatia mazao hayo.
“Sisi kama bodi tunaona Sao Hill mna uwezo huo na tunasisitiza zaidi kuwa na viwanda hivyo kwani nia mnayo uwezo mnao na nguvu mnazo za kutekeleza agizo hilo mkisaidiana na viongozi wenu kutoka TFS Makao makuu hili litasaidia sana hata wale wafugaji wadogo wadogo kuinuka na hatimae kuwa na kipato cha kutosha kisha kuchangia uchumi wa Taifa”.
Aidha amewataka watumishi wote wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kuongeza kuboresha utendaji kazi zaidi ili kuongeza mapato na kusaidia kukua kwa uchumi wa nchi na hii inatokana na kipindi kilichopo ambapo nchi imeamua kuja na mpango wa kujitegemea zaidi na kupunguza misaada kutoka nje kutoka asilimia 42% hadi sasa kufikia asilimia 8% ili kuweza kujiendesha wenyewe kwa mapato ya ndani.
Mkurugenzi wa Usimamizi Rasilimali za Misitu na Nyuki TFS Bw. Zawadi Mbwambo amewataka watumishi wote kuendelea na juhudi kufanya kazi kwa bidii na kuendeleza misitu kwa faida ya kizazi cha sasa na vizazi vijavyo.
“Nashukuku Sao Hill na TFS kwa ujumla tunaenda vizuri na ndio maana hata bungeni kwa kipindi hiki hakuna maswali mengi bungeni tayari tumeshawarahisishia kazi mawaziri wetu zaidi tunaendelea kupokea pongezi hivyo tusibweteke na sifa hizo bali tuongeze bidii za kufanya kazi kwa Uhodari ushirikiano na kwa weledi wa hali ya juu kwa manufaa ya Taifa letu”
Kwa Upande wake Meneja Shamba la Miti Sao Hill Bw. Heriberth Haulle amesema uwepo wa Shamba la Miti Sao Hill umekuwa mkombozi mkubwa kwa uchumi wa wilaya ya Mufindi na Mkoa wa Iringa kwa ujumla na kumekuwa na mahusiano mazuri baina ya shamba na wananchi wanaozunguka shamba.
Aidha shamba limekuwa likichangia sana katika shughuli za maendeleo katika vijiji vyote vinavyozunguka shamba mfano kupitia ukatishaji wa leseni za kufanya shughuli za uchakataji mazao ya misitu kwa umoja wa wadau wa mazao hayo wamekuwa wakichangia 2% ya leseni hizo na mapato yanayopatika hupelekwa katika Halmashauri zinazozungukwa na msitu ili kuchochea shughuli za maendeleo vijijini kulingana na vipaumbele vyao.
“Mpaka kufikia mwezi mei mwaka huu 2019 tumekusanya zaidi ya Milioni 315 kama mpango wa wavunaji kuchangia shughuli za maendeleo vijijini na tayari fedha hizo zilishapelekwa katika Halmashauri zinazozungukwa na shamba letu”
Mbali na hilo pia Shamba la Miti Sao Hill katika Bajeti ya mwaka 2019/2020 imetenga zaidi ya milioni 172 kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii hususani kujenga mabweni 02 ya Wasichana katika shule za sekondari na huu pia ni mchango wa shamba kwa jamii.
Akitoa neno la shukrani Kaimu Meneja wa TFS Nyanda za juu Kusini Bw. Ebrantino Mginje amesema maelekezo na ushauri uliotolewa na bodi kwa ziara nzima umechukuliwa na tayari hatua za utekelezaji zinaanza mara moja ili kuwa na misitu endelevu kwa faida ya sasa na baadae.
Bodi hii ya Ushauri ya Wizara kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS ilizinduliwa rasmi machi 9 mwaka 2019 Jijini Mwanza na Waziri wa Maliasili na Utalii nchini Tanzania Dkt. Hamisi Kigwangalla na inaongozwa na Mwenyekiti wake Brigedia Jenerali Mbaraka Mkeremy.
MATUKIO KATIKA PICHA
Mjumbe wa Bodi ya Ushauri ya Wizara Kwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS Bi. Piencia Kiure akitoa maelekezo kwa Watumishi wa TFS Shamba la Miti Sao Hill (Hawapo pichani) |
Meneja Tarafa ya I Irundi Shamba la Miti Sao Hill Bi. Glory Fortunatus akitoa maelezo ya Bustani ya Miche Irundi wakati Bodi ya Ushauri ilipotembelea eneo hilo |
(Picha zote na Amani Mbwaga) |
Wednesday, June 26, 2019
Sunday, June 23, 2019
Thursday, June 20, 2019
Tuesday, June 18, 2019
Tuesday, June 11, 2019
Monday, June 10, 2019
Sunday, June 9, 2019
Friday, June 7, 2019
Friday, May 24, 2019
Thursday, May 23, 2019
Friday, May 17, 2019
Thursday, May 16, 2019
Friday, May 10, 2019
Thursday, May 9, 2019
Tuesday, May 7, 2019
Monday, May 6, 2019
Sunday, May 5, 2019
Friday, May 3, 2019
Tuesday, April 30, 2019
Thursday, April 25, 2019
Wednesday, April 24, 2019
Monday, April 22, 2019
Sunday, April 21, 2019
Friday, April 19, 2019
Wednesday, April 17, 2019
Tuesday, April 16, 2019
Monday, April 15, 2019
Sunday, April 14, 2019
Saturday, April 13, 2019
Friday, April 12, 2019
Thursday, April 11, 2019
Wednesday, April 10, 2019
Monday, April 8, 2019
Wednesday, April 3, 2019
Tuesday, April 2, 2019
Monday, April 1, 2019
Sunday, March 31, 2019
Saturday, March 30, 2019
Monday, March 25, 2019
Friday, March 22, 2019
Thursday, March 21, 2019
Shamba la Miti Sao Hill Laadhimisha Siku ya Kimataifa ya Misitu Duniani na Kugawa Miche ya Miti Takribani Milioni 1 Kwa Wananchi Buree.
Na Amani Mbwaga, Mafinga.
Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) Shamba la miti Sao Hill limeungana na taasisi nyingine
duniani katika kuadhimisha siku ya misitu duniani ambayo hufanyika Tarehe 21
Machi ya kila mwaka.
Katika madhimisho
ya mwaka huu shamba la miti Sao Hill limewapatia wananchi na Taasisi mbalimbali
za serikali na binafsi Miche takribani Milioni Moja ya miti aina ya Msindano
(Pine) kwa lengo la kuongeza kasi ya upandaji wa miti kila mwaka ili kurahisisha
upatikanaji wa malighafi ya mazao ya misitu viwandani kwa dhumuni la kuunga
mkono serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dkt John Magufuli ya kuwa
na Tanzania ya Viwanda na kufikia uchumi wa kati ifikapo 2025.
Meneja Shamba la
Miti Sao Hill Bwana Herberth Haulle akiongea na waandishi wa habari ofsini
kwake ameeleza namna sekta ya misitu nchini inavyochangia katika kutoa
malighafi ya viwanda vya Karatasi, Mbao, Nguzo, viberiti, chai (Kukaushia-chai)
nk.
Viwanda vipatavyo
elfu saba huwasilisha uhitaji wa malighafi katika mashamba ya miti
yanayomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, 81.2% ya viwanda hivi
vinaonesha uhitaji wa malighafi kutoka eneo tengefu la Saohill.
Saohill inahudumia
71% ya viwanda vinavyohudimiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia
mashamba ya miti.
Viwanda hivi
vilionesha kuhitaji jumla ya meta za ujazo milioni 22,439, 489 kwa Sao hill
pekee viwanda vilionesha uhitaji wa meta za ujazo milioni 18 hii ni asilimia
84.3%, Ambapo malighafi iliyotolewa
(uwezo wa mashamba) ni asilimia 5 tu ya malighafi iliyohitajika kwa viwanda.
Uwezo wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kutoa malighafi kwa viwanda ni mita za ujazo millioni moja kwa mwaka ambapo Saohill hutoa 83.8% ya malighafi husika.
Chanzo cha mapato ya serikali (TFS) kwa zaidi ya nusu ya makusanyo yanayo fanywa na TFS ni makusanyo kutoka Shamba la Miti Sao hill.
Misitu huchangia pia katika upatikanaji wa hali nzuri ya hewa na utunzaji wa vyanzo vya maji ya kutumia binadamu na mengine kwa ajili ya kuzalisha nishati ya umeme, mfano bwawa la Kihansi na Mto Ruaha unaopeleka maji yake katika mradi mpya wa umeme Rufiji (Stigler’s Gorge).
Aidha bwana Haulle ameeleza pia namna sekta ya misitu kupitia shamba la miti Sao Hill linavyochangia katika uchumi wa wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, Taifa na dunia kwa ujumla.
“Shamba limekua likichangia asilimia tano 5% ya mrabaha wa mauzo ya miti (CESS) kwa mujibu wa sheria kwa Halmashauri zinazozungukwa na Shamba la Miti Sao Hill ambazo ni Mufindi, Kilombero na Halmashauri ya Mji Mafinga ambapo kwa kipindi cha mwaka 2010/2011 hadi disemba 2018 kiasi cha Zaidi ya Bilioni 6 kilikusanywa kama CESS na kukabidhiwa kwa halmashauri husikakwa ajili ya shughuli za maendeleo” alisema.
Aidha shamba la miti Sao Hill huajiri vibarua wa kutwa Zaidi ya Elfu tatu 3000 kwa mwaka katika kazi mbalimbali za shamba na wengi wao ni wakazi wanaozungukwa na shamba hilo.
Akiongea katika Kipindi maalumu cha utoaji elimu kwa umma leo hii kuhusu siku ya Kimataifa ya Misitu duniani katika kituo cha redio Ebony fm MKoani Iringa Meneja Msaidizi Mipango na Matumizi wa Shamba la Miti Sao Hill Bwana Ignas Lupala ameeleza chimbuko kubwa la misitu Tanzania na hatimae hadi kuanzishwa kwa shamba la miti Sao Hill.
Kwa kuzingatia taarifa ya tathimini ya rasilimali ya misitu iliyofanyika nchini kati mwaka 2010 – 2013, inaonesha kuwa misitu inakadiriwa kufikia eneo la hekta milioni 48.1, sawa na asilimia 55 ya eneo la ardhi la Tanzania Bara lenye hekta millioni 88 (TFS, 2015).
Kati ya eneo hilo, asilimia 93 ni misitu ya mataji wazi (woodlands), wakati sehemu inayobaki inajumuisha misitu ya lindimaji, mikoko, misitu ya pwani (coastal forests), na mashamba ya miti.
Misitu ya kupandwa ni hekta 572,000 ambayo inajumuisha yale yanayomilikiwa na serikali, watu na makampuni binafsi.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, mahitaji ya mazao ya misitu yalikadiriwa kuwa ni meta za ujazo milioni 62.3 kwa mwaka huku wakati uwezo wa misitu kutoa mahitahiji hayo kwa njia endelevu ukiwa meta za ujazo milioni 42.8.
Hivyo, kuwepo na upungufu wa meta za ujazo milioni 19.5 kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama nishati (kuni na mkaa), nguzo za umeme pamoja na mbao kwa ajili ya ujenzi.
Upungufu huo umekuwa kichocheo cha uvunaji haramu katika misitu ya asili ambao husababisha uharibifu na upotevu wa misitu hiyo.
Katika jitihada za kuongeza upatikanaji wa Malighafi ya miti Ili kukabiliana na upungufu wa malighafi/ mazao ya misitu, serikali ilianzisha mashamba ya miti (forest plantations) katika maeneo mbalimbali.
Lengo ni kupunguza utegemezi wa mazao ya misitu kutoka katika misitu ya asili ili kuhifadhi mazingira na baionuai.
Kwa sasa serikali inamiliki mashamba 24 yanayopatikana maeneo mbalimbali nchini.
Mashamba hayo yana jumla hekta 306,980.20 na kusimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).
Kati ya hekta hizo, jumla ya hekta 105,583.56 sawa na asilimia 34 ya eneo la mashamba hayo zimepandwa miti.
Maeneo mengine yamehifadhiwa kwa ajili ya vyanzo vya maji na mengine yanaendelea kupandwa kulinganga na mipango ya usimamizi wa mashamba husika.
Shamba la Miti Sao Hill ni miongoni mwa mashamba 24 ya miti ya kupandwa ya serikali ambayo yanasimamiwa na Wizara ya Maliasili na Utalii Kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)
Shamba hili kwa sehemu kubwa lipo katika wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa na eneo dogo lipo katika Wilaya ya Kilombero Mkoani Morogoro
Shamba hili lilianzishwa kwa majaribio mnamo mwaka 1939 hadi 1951 na upandaji wa miti kwa kiwango kikubwa ulianza rasmi kuanzia miaka ya 1960 hadi 1980.
Aidha shamba hili ndilo shamba kubwa kuliko mashamba yote 24 ya serikali ambapo kwa sasa lina ukubwa wa hekta laki moja na thelathini na tano elfu mia tisa na tatu 135,903.
Katika kuadhimisha siku ya kimataifa ya misitu duniani kila mwaka, nchi mbalimbali duniani zinahamasishwa kuendeleza juhudi za kitaifa na kimataifa ili kuandaa na kushiriki katika shughuli zinazohusika na misitu pamoja na miti, kama vile kampeni ya kupanda miti pamoja na midahalo kuhusu misitu.
Siku hii huadhimishwa kwa ajili ya kuwafanya watu waelewe umuhimu wa aina zote za misitu duniani, ikiwemo jukumu lake katika mabadiliko ya tabia nchi.
Siku hii ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2012 na siku hiyo ilisherehekewa kwa mara ya kwanza Machi 21, 2013.
Makala hii Maalumu Imeandaliwa na Amani Mbwaga kwa kushirikiana na Kitengo cha Uenezi na Ugani katika Ofisi ya Habari na Mawasiliano TFS- Shamba la Miti Sao Hill
Tarehe 21 Machi 2019.
Mob+255 656 632 566
E-mail:prof.mbwaga@gmail.com
HABARI PICHA
Meneja Shamba la Miti Sao Hill Bwana Heriberth Haulle |
Baadhi ya Miche ya Miti ya Msindano (Pines) Iliyopandwa Msimu huu katika Shamba la Miti Sao Hill na Mingine Kugawiwa kwa Wananchi bure |
Daniel Silima Meneja Msaidizi Rasilimali za Misitu Shamba la Miti Sao Hill |
Ignas Lupala Meneja Msaidizi Mipango na Matumizi Shamba la Miti Sao Hill Mapema Leo hii akitoa Elimu kwa umma kwa njia ya Redio kuhusu chimbuko la Misitu Nchini na Faida za uwepo wa Shamba la Miti Sao Hill katika kituo cha EBONY FM RADIO Mapema leo wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Misitu Duniani (Picha na Amani Mbwaga) |
(Picha zote na Amani Mbwaga) |
Friday, March 15, 2019
Tuesday, March 5, 2019
Monday, February 25, 2019
Saturday, February 23, 2019
Sunday, February 17, 2019
Mbunge Chumi Akabidhi Magari 02 Bure kwa Idara ya Elimu Mafinga
Na
Amani Mbwaga, Mafinga.
Mbunge wa Jimbo la
Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi Mapema wiki hii amekabidhi Magari idadi mawili
kwa Idara ya elimu katika Halmashauri ya Mji Mafinga kwa lengo la kuongeza
nguvu ya ufuatiliaji wa masuala ya elimu ili kuongeza ufanisi wa utendaji kazi
na kuongeza ufaulu kwa wanafunzi wa Jimbo la Mafinga Mjini na Taifa kwa ujumla.
Hafla ya
makabidhiano hayo imefanyika katika viwanja vya Teachers Resource Centre (TRC
Mafinga) wakati wa mkutano wa tathimini ya Elimu kwa Halmashauri ya Mji Mafinga
ambapo umewakutanisha takribani waalimu wakuu wa shule zote za Sekondari na Msingi,
Maafisa Elmu kata, Wilaya na Wataalamu wengine wote wa Sekta ya Elimu Mjini
Mafinga.
Akiongea na
Wataalamu hao wa elimu Mbunge wa Jimbo la Mafinga Mjini Mhe. Cosato Chumi
ameelezea hisia zake juu ya umuhimu wa elimu kwa wananchi wa Jimbo lake na taifa
kwa ujumla.
“Mimi
naamini kwamba elimu ndio kila kitu bila elimu tusingekuwa hapa kwa hiyo
tunapokaa kufanya tathimini ya elimu tunapanga ili kuboresha elimu ya watoto
wetu” alisema
Aidha ameeleza kuwa
Halmashauri ya mji mafinga bado ni changa na ilianzishwa hivi karibuni kwa hiyo
idara nyingi zina uhaba wa magari kwa hiyo yeye kama mbunge ameamua kujiongeza
kutafuta wadau wakamsaidia magari hayo mawili ambayo ameyakabidhi kwa idara ya
elimu Msingi na Sekondari.
Kwa Mujibu wa Mhe.
Chumi amesema kwamba magari hayo amepewa na Kamishina wa Ushuru na Forodha wa Mamlaka
ya Mapato Tanzania (TRA) baada ya kumsumbua sana ili amsaidie magari kwa ajili
ya idara za halmashauri yake na ndipo kamishina huyo akampatia magari hayo na
leo ameikabidhi Halmshauri Kupitia Mkuu wa Wilaya Mufindi na baade kumkabidhi
Mwenyekiti wa Halmashari ya Mji Mafinga tayari kwa matumizi ya kiserikali
hususani idara ya elimu.
Akitoa shukrani kwa
Mbunge huyo Mgeni wa rasmi wa hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe. Jamhuri
William amempongeza Mhe. Chumi kwa kulipigania jimbo la Mafinga mjini katika
kuhakikisha maendleo yanapatikana kwani amekuwa msaada mkubwa sana.
“Leo
hii tumepokea magari mazuri halafu mapya kabisa yaliyotokana na jitihada za
mbunge wetu Chumi, mimi kipekee nakushukuru sana naomba upeleke shukrani na
salamu zetu kama Wilaya kwa wadau wote waliojitolea upatikanaji wa magari haya”
alisema
Mhe. William
amemhakikishia Mhe. Mbunge Chumi kuwa magari hayo yatatunzwa kwa kuzingatia
kanuni na taratibu zote za utunzaji wa magari ya serikali na kutumika kwa shughuli
za serikali hususani shughuli za elimu tu.
Hapo awali kulikuwa
kunachangamoto ya shule nyingi kutofanyiwa ukaguzi na idara ya udhibiti
ubora elimu kutokana na ukosefu na uhaba
wa usafiri sasa kupatikana kwa magari haya ni wakati muafaka wa kuhakikisha
hakuna tena tatizo la ufuatiliaji wa elimu Mafinga Mjini.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe. Charles Makoga amesema Mhe.
Mbunge Chumi amekuwa akisaidia sana katika upatikanaji wa vifaa mbalimbali toka
ameingia ubunge kwa muda mfupi amechangia upatikanaji wa magari ya kubebea Wagonjwa
(Ambulance) takribani manne sasa katika Halmshauri hiyo lakini pia alipigani
pia kupatikana kwa gari la TASAF na la udhibiti ubora yote mapya ambayo
yamepatikana pia hivi karibuni.
“Mhe
Mbunge mimi nikushukuru sana na mungu akubariki sana kwa upendo wako mkubwa kwa
wananchi wa Mafinga kama Mungu hua anapunguza miaka basi kwangu apunguze miwili
tu akuongezee wewe” alisema Mhe. Makoga.
Akieleza lengo la
tathimini ya elimu ya mwaka 2018 hasa katika matokeo ya mitihani ya kitaifa
Kaimu Mkurugenzi na Afisa Elimu Sekondari wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bwana
Voster Mgina amesema tathimini hiyo itachangia kupanga mipango madhubuti ya
mwaka 2019.
Matokeo ya mitihani
ya Taifa kwa mwaka 2018 Halmashauri ya Mji Mafinga ilifanya vizuri sana katika
mitihani yote.
Mtihani wa darasa la
saba Halmashauri ya Mji Mafinga iliweza kufaulisha kwa kiwango cha asilimia
92.86%
Mtihani wa Kidato
cha pili ufaulu ulikuwa wa kiwango cha asilimia 96% na kidato cha nne ufaulu
ulikuwa wa kiwango cha asilimia 87 wakati huo mwaka jana ufaulu ulikuwa
asilimia 73% lakini mwaka huu shule zote zimepandisha ufaulu na zimeweza kupunguza daraja 0 kutoka 350
hadi 176.
Aidha kidato cha
sita kwa matokeo ya mwaka 2018 Halmashauri ya Mji Mafinga iliweza kufaulisha
kwa kiwango cha asilimia 100% na hakukua na mwanafunzi aliyepata daraja la 0
wala daraja la IV kwa shule zote za serikali
na binafsi.
HABARI PICHA
Magari aliyoyatoa Mbunge wa Mafinga Mjini Mhe Cosato Chumi kwa Idara za Elimu Mafinga Mji |
Mhe. Charles Makoga akitoa Shukrani |
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mafinga Mhe Charles Makoga akimkabidhi Fungua Kaimu Mkurugenzi na Afisa Elimu Sekondari Bwana Voster Mgina mara baada ya kukabidhiwa na Mbunge Cosato Chumi (Picha zote na Amani Mbwaga) |
Subscribe to:
Posts (Atom)