Sunday, July 6, 2014

WATU ZAIDI YA 50 WAUAWA UGANDA


Watu wasiopungua 50 wameuawa baada ya watu wenye silaha kushambulia vituo vya polisi na kambi za jeshi nchini Uganda, kwa mujibu wa jeshi.
Miongoni mwa waliokufa ni washambuliaji 41 na polisi pamoja na raia 17.
Mashambulio hayo yametokea magharibi mwa Uganda, karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.
Mashambulio hayo yamelenga majeshi katika wilaya za Kasese, Ntoroko na Bundibugyo.
Msemaji wa jeshi amesema mashambulio hayo hayana uhusiano wowote na kundi la waasi la ADF, ambalo lilikuwa likifanya shughuli zake katika eneo hilo zaidi ya muongo mmoja uliopita.
"Tunachofahamu ni kuwa wanamgambo hawa hawana uhusiano na ADF-NALU, lakini tunachunguza kuona sababu hasa na nani wanawaunga mkono," amesema Paddy Ankunda, msemaji wa jeshi akizungumza na shirika la habari la Reuters.
Watu 17 walikamatwa na wanahojiwa kwa mujibu wa polisi.
LikeSource: kikeke S.

No comments:

Post a Comment