Lionel Messi, ambaye alipoteza fursa ya kutwaa kombe la dunia aliambulia tuzo la mchezaji bora katika mchuano huo uliokamilika kwa ushindi wa Ujerumani huko Brazil.
Messi ambaye amesifiwa kwa miondoko yake na uwezo wake mbele ya lango huko Barcelona alitawazwa kuwa mchezaji bora katika mechi nne tofauti.
Messi alifunga mabao manne katika kipute hicho mbili nyuma ya mshambulizi wa Colombia James Rodriguez aliyetuzwa kuwa mfungaji mabao mengi mwaka huu.
Kipa wa ugerumani alikuwa na bahati ya kutwaa nishani ya dhahabu , kombe la dunia na pia tuzo la kipa nambari moja katika kipute hicho.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 28 na ambaye anayeilindia lango mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich aliwapiku mlinda lango wa Argentina Sergio Romero na Keylor Navas kutoka Costa Rica.
Neuer alifungwa jumla ya mabao 4 pekee katika mchuano huu huko Brazil.
Nuer anachukua wadhfa aliokuwa nao kipa wa Uhispania Iker Casillas.
Mshambulizi wa Colombia James Rodriguez alitawazwa mshindi wa Golden Boot baada ya kuongoza katika orodha ya wafungaji mabao mengi katika mchuano wa mwaka huu wa kombe la dunia .
Rodriguez alifunga mabao sita akifuatwa kwa karibu na Mshambulizi wa wa Ujerumani Thomas Mueller akiwa na jumla ya mabao 5.
Licha ya kuwa Colombia iliondolewa katika hatua ya robo fainali Hakuna mshambulizi aliyeweza kumpiku Rodriguez .
Lionel Messi, Neymar ana Robin van Persie, wote walifunga mabao manne kila mmoja.
Paul Pogba wa Ufaransa alituzwa kuwa mchezaji anayeinukia bora .
Timu ya Colombia ilituzwa kwa kuwa timu yenye nidhamu katika mashindano haya
Source: BBC.