Saturday, September 21, 2013

Kama ubaya, ubaya tu England







KWA UFUPI
Manchester, England. Mashabiki wa Manchester United wamefanikiwa kumpata Marouane Fellaini na kiungo huyo wa Ubelgiji ameonyesha kiwango cha juu kwa kutoa pasi nzuri na kunyang’anya mpira wakielekea katika mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu wao City.

Viungo Yaya Toure wa City ataonyeshana ufundi na Marouane Fellaini wa United kesho kwenye uwanja wa Etihad.
Manchester, England. Mashabiki wa Manchester United wamefanikiwa kumpata Marouane Fellaini na kiungo huyo wa Ubelgiji ameonyesha kiwango cha juu kwa kutoa pasi nzuri na kunyang’anya mpira wakielekea katika mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu wao City.
Mabingwa wa msimu uliopita na washindi wa pili wanakutana kwenye Uwanja wa Etihad, wakiwa na rekodi ya ushindi waliopata katikati ya wiki katika Ligi ya Mabingwa.
Mshambuliaji wa Wayne Rooney amerudi kwenye kiwango chake na Jumanne alifunga mabao mawili wakishinda 4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen, lakini uwepo wa Fellaini katika nafasi ya kiungo aliyeonyesha uwezo mzuri wa kumiliki mpira umeongeza ladha ya mchezo wa kesho.
Wapinzani wao City baada ya kupoteza dira katika ligi katikati ya wiki walishinda 3-0 dhidi ya Viktoria Plzen katika Ligi ya Mabingwa, ushindi unaomfanya kocha Manuel Pellegrini kuamini kwamba umerudisha kujiamini kwa wachezaji wake.
“Tuna mechi ngumu Jumapili na ushindi wa ugenini katika Ligi ya Mabingwa tena wa mabao matatu, nafikiri umerudisha kujiamini kwa wachezaji.”
Kiungo wa City,Yaya Toure, ambaye ni kama Fellaini ameonyesha kiwango cha juu, cha kutengeneza magoli na uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, pia alifunga bao moja dhidi ya Plzen na kesho inategemewa itakuwa ni vita kubwa kati ya viungo hao wawili.
Hii ni mechi ya kwanza ya miamba ya Manchester kukutana wakati timu zote zikiwa na makocha wapya ambao wanajua kuwa City imekusanya pointi 10 kutoka kwa United katika michezo saba ya ligi waliokutana katika misimu mitatu iliyopita.


No comments:

Post a Comment