NAFASI ZA KAZI 900 UTUMISHI WA UMMA
Kumb. Na EA.7/96/01/D/23
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI
Sekretariati
ya Ajira katika Utumishi wa Umma ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu
wa Sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 kama ilivyorekebishwa
na Sheria Na. 18 ya mwaka 2007 kifungu 29(1). Kwa mujibu wa Sheria
hiyo, chombo hiki, pamoja na kazi zingine kimepewa jukumu la kutangaza
nafasi wazi za kazi zinazotokea katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya
Waajiri (Taasisi za Umma).
Katibu
wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma anakaribisha maombi ya
Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi 944 za kazi kwa waajiri
mbalimbali kama ifuatavyo:
Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu
wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi na Ushirikiano wa Kimataifa, Afisa
Mtendaji Mkuu Wakala wa Vipimo, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo Jinsia na Watoto, Katibu Mkuu
Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu Wizara ya mifugo na Uvuvi, Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda
na Biashara, Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na Technolojia, Katibu Mkuu
Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Mkuu Wizara
ya Maji, Katibu Ofisi ya Rais Maadili, Katibu Tawala Mkoa Kagera,
Iringa, Ruvuma, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Manyara, Dar es Salaam,
Morogoro, Geita, Pwani, Mara, Kilimanjaro, Lindi, Singida, Tabora,
Tanga, Katavi na Arusha,Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza,
Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Iringa, Songea, Shinyanga,Morogoro,
Singida, Kigoma/Ujiji na Temeke, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya
Mufindi, Kyera, Rungwe, Mbeya, Chunya, Biharamulo, Bukoba, Muleba,
Namtumbo, Songea, Morogoro, Makete, Mkuranga, Mbinga, Tunduru, Ukerewe,
Sengerema, Ilemela, Busega, Maswa, Meatu, Shinyanga, Kishapu, Kilosa,
Msalala, Rufiji, Rorya, Ruangwa, Lushoto, Mkinga, Mpanda, Monduli,
Ngorongoro,Kigoma, Nachingwea, Rombo, Same, Singida, Urambo, Tabora,
Babati, Mbulu, Simanjiro, Kiteto, Handeni, Pangani, Kibondo, Chamwino,
Mtwara, Nanyumbu, Mpwapwa, Kongwa na Tandahimba. Mkurugenzi Halmashauri
ya Mji Njombe, Kibaha, Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) na TEMESA.
1.0 MCHAMBUZI MIFUMO YA KOMPYUTA DARAJA LA II – (NAFASI 10)
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Katibu Mkuu wizara
ya Kilimo na Chakula, Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Mkurugenzi
Halmashauri za Wilaya za Mufindi, Meatu, Rorya, Mbulu na Mtwara na
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Kibaha.
1.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuweka kumbukumbu za taratibu za kisasa na mbinu za kufanyia kazi.
· Kutekeleza chati za mtiririko wa mifumo ya nyendo za taarifa na uthibiti unaohusu Kompyuta.
· Kutoa msaada wa kiufundi kwa Wizara/Idara/Vituo mbalimbali vya kazi.
1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye Shahada/Stashahada ya Juu katika masomo ya Sayansi ya Kompyuta
kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
1.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D.
2.0 AFISA VIPIMO II – NAFASI 6
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Afisa Mtendaji Mkuu, Wakala wa Vipimo
2.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukagua, kuhakiki na kuvirekebisha vipimo vya wafanyabiashara;
· Kutunza, kuhifadhi vifaa vya kitaalam vitumikavyo katika utendaji wa kazi;
· Kutoa ushauri kuhusu masuala ya uhakiki na matumizi ya vipimo;
· Kufanya upelelezi kuhusu ukiukwaji wa Sheria ya Vipimo
· Kupokea na kufanyia kazi malalamiko ya wadau na waateja;
· Kufanya kazi nyingine kama atakavyopangiwa na kiongozi wake zinazohusiana na
· elimu na ujuzi wa kazi
2.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza katika fani ya “Legal Metrology” au “Legal and
· Industrial Metrology” toka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Au
· Kuajiriwa wenye Shahada ya kwanza ya Uhandisi/Sayansi ambao wamepata “Crash
· programme” ya “Legal and Industrial Metrology” isiyopungua miezi mnne (4) toka
· Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
· Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Uhandisi/Sayansi ambao wamehitimu
· Stashahada ya Uzamili (Postgraduate Diploma) katika fani ya vipimo katika Chuo
· kinachotambuliwa na Serikali.
· Kuajiriwa
wenye Stashahada ya juu katika fani ya “Legal Metrology” /Legal and
“Industrial Metrology” toka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
2.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani PTSS 13 -14 kwa mwezi.
3.0 MPIMA ARDHI DARAJA LA II (LAND SURVEYOR GRADE II) – (NAFASI 26)
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu
Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi, Katibu Tawala Mkoa wa Iringa,
Geita, Tabora, Kigoma na Mara, Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza,
Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Songea na Singida,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, Songea, Tunduru, Busega,
Shinyanga, Kishapu, Morogoro, Nachingwea, Rombo, Kongwa, Mkinga,
Nanyumbu na Rorya.
3.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Sehemu ya Upimaji Milki (Cadastral Survey)
- Kuingiza taarifa za Upimaji (alpha numeric data) kwenye kompyuta.
· Sehemu ya Topographic na Geodetic Surveys
- Kukagua kazi za upimaji na kuingiza taarifa za kazi zilizothibitishwa kwenye komputa.
· Sehemu ya Ramani
- Kufanya upimaji picha (aerial triangulation and block adjustment);
- Kuandaa vikosi kwa ajili ya kuhuisha ramani (map revision)
- Kutunza kumbukumbu za picha za anga.
· Sehemu ya Hydrographic Surveys
-Kusimamia na kuchukua vipimo vya tide gauges.
· Mpima Ardhi katika Serikali za Mitaa
- Kufanya kazi za nje ya Ofisi (field survey operations) chini ya usimamizi wa mpima aliyesajiliwa.
3.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Stastahada ya juu/Shahada kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi katika fani
ya Upimaji Ardhi au Taasisi yoyote inayotambuliwa na National Council
of Professional Surveyors (NCPS). Au
· Kuajiriwa
wenye cheti cha East African Land Survey (EALSC) au National Council of
Professional Surveyors Certificate (NCPSC) katika fani ya upimaji
ardhi.
3.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi.
4.0 MHANDISI DARAJA LA II – UFUNDI NA UMEME (MECHANICAL AND ELECTRICAL ENGINEER GRADE II) – NAFASI 9
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kyela, Msalala
na Pangani, Mkurugenzi ya Manispaa ya Singida na Morogoro na TEMESA.
4.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya
kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya Usajili wa
Wahandisi kama “Professional Enginner” ili kupata uzoefu unaotakiwa.
· Kufanya
kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi kupata
sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi
· Kukusanya
taarifa na takwimu kuhusu magari na mitambo mbalimbali, bei za magari
na mitambo na vifaa vya umeme ndani na nje ya nchi
· Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposal) mbalimbali ya ufundi na umeme yanayowasilishwa.
4.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Uhandisi Ufundi na Umeme.
4.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
5.0 AFISA MIPANGO MIJI DARAJA LA II (TOWN PLANNER) – NAFASI 13
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Tabora na Katavi,
Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya Singinda, Mkurugenzi Halmashauri ya
Wilaya ya Kyela, Tunduru, Kishapu, Rorya, Nachingwea, Urambo, Mbulu na
Kigoma.
5.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuandaa mipango ya maeneo yaliyoendelezwa kiholela.
· Kuandaa michoro ya Mipangomiji.
· Kupokea michoro ya Mipangomiji na taarifa za maeneo ya ardhi yanayopendekezwa kuiva kwa ajili ya uendelezaji kimji.
· Kuchambua takwimu na taarifa kwa ajili ya maandalizi ya mipango mipya ya makazi.
· Kupokea na kuweka kumbukumbu za maombi ya mabadiliko ya matumizi ya ardhi na umegaji wa viwanja.
· Kuhakikisha kuwa mabadiliko ya matumizi ya ardhi yanaingizwa katika michoro.
5.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
mwenye Stashahada ya juu/Shahada katika fani ya Mipangomiji kutoka Chuo
Kikuu cha Ardhi au Vyuo Vikuu au Taasisi nyingine zinazotambuliwa na
Serikali.
5.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
6.0 MHANDISI DARAJA LA II – UJENZI (ENGINEER GRADE II – CIVIL) – (NAFASI 16)
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu Wizara ya Maji,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya za Kyela, Mbulu na Ilemela, Mkurugenzi
Halmashauri ya manispaa ya Singida.
6.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Atafanya kazi chini ya uangalizi wa Mhandisi aliyesajiliwa
(Professional engineer) na bodi ya usajili ya Wahandisi ili kupata
uzoefu unaotakiwa.
·Kufanya ukaguzi wa Barabara, Madaraja na Majengo mbalimbali
·Kuchunguza vyanzo vya ajali barabarani
·Kufuatilia utekezaji wa Sheria, Kanuni za ujenzi wa Barabara na Majengo
·Kutayarisha bajeti ya mwaka ya Ujenzi na matengenezo ya Barabara, Madaraja na Majengo
·Kusimamia na kuratibu kazi za Barabara, Madaraja na Majengo zinazotolewa na makandarasi
6.3 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Uhandisi Ujenzi.
6.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
7.0 MHANDISI DARAJA LA
II MAJI (WATER ENGINEER GRADE II) – (NAFASI 13)
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Tawala Mkoa wa
Shinyanga na Geita, Mkurugenzi Halmashauri ya manispaa ya Temeke,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya za Rungwe, Busega na Chamwino.
7.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Ujenzi
na Usimamizi wa Vituo vya Hali ya Hewa, Vituo vya Upimaji wingi wa Maji
mitoni (Discharge Measurements) na Uchukuaji wa sampuli za mchanga
unaosafirishwa kwenye mito (sedment sampling) na kuzitafsiri.
· Ukusanyaji wa takwimu kwenye vituo vya hali ya hewa na upimaji wa wingi wa maji mitoni na kuzitafsri takwimu hizo.
· Kuandaa na kutayarisha Taarifa ya robo, nusu na mwaka mzima katika sehemu ya Haidrologia.
·Kutayarisha kielelezo cha mtiririko wa maji ( Rating Curve Eqution )
7.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·Kuajiriwa
mwenye Shahada ya Uhandisi wa Rasilimali za Maji kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
7.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
8.0 AFISA MISITU DARAJA LA II (FOREST OFFICER GRADE II) – NAFASI 7
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Katavi, Mkurugenzi
Halmashauri ya Wilaya za Muleba,Tunduru, Sengerema na Ilemela.
8.1MAJUKUMU YA KAZI
·Kusimamia upandaji na uhudumiaji wa miti na misitu.
·Kusimamia uendelezaji wa misitu ya kupandwa isiyozidi hekta 5,000 au ya asili isiyozidi hekta 10,000.
· Kufanya utafiti wa misitu.
· Kutekeleza Sera na Sheria za misitu.
· Kuendesha mafunzo ya Wasaidizi Misitu.
· Kukusanya takwimu za misitu.
· Kufanya ukaguzi wa misitu.
· Kupanga na kupima madaraja ya mbao.
· Kudhibiti leseni na uvunaji wa miti.
· Kutoa ushauri na mafunzo kwa wananchi juu ya uendelezaji na matumizi endelevu ya miti na misitu kwa wananchi.
· Kufanya ukadiriaji wa rasilimali za misitu.
· Kupima maeneo na kuchora ramani za misitu.
8.3 SIFA ZA MWOMBAJI
·Kuajiriwa wenye Shahada ya Misitu kutoka chuo Kikuu cha kilimo cha Sokoine au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
8.4MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi.
9.0AFISA WA SHERIA DARAJA LA II (LEGAL OFFICER GRADE II) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Ruvuma na Katavi na Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Makete.
9.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili
ni daraja la mafunzo katika kazi, hivyo Maafisa wa Sheria katika daraja
hili watafanya kazi za kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria
Waandamizi ikiwa ni pamoja na:
· Kutoa ushauri na kufanya utafiti wa kisheria pale anapohitajika kulingana na Wizara, Idara ya Serikali ama sehemu aliko.
· Kufanya mawasiliano na ofisi nyingine kuhusu masuala ya kisheria kwa maelekezo ya Maafisa wa Sheria walio katika ngazi za juu.
9.2SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye shahada ya kwanza ya Sheria kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali na waliomaliza mafunzo ya uwakili
yanayotambuliwa na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
9.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi
10.0 MTAKWIMU DARAJA LA II (STATISTICIAN GRADE II) – NAFASI 8
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Shinyanga na Mwanza,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Busega na Tunduru.
10.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kubuni na kuendeleza mfumo wa kitaifa wa kukusanya na kuratibu takwimu
· Kutengeneza utaratibu wa kukusanya takwimu pamoja na ule wa kuchukua takwimu za mfano/vielelezo (Sampling)
· Kukusanya, Kuchambua na kuwasilisha takwimu ngazi za juu.
10.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·Kuajiriwa
wenye shahada ya kwanza katika fani ya Takwimu au Hisabati au sifa
zinazolingana na hizo kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali na
wenye ujuzi wa kutumia Kompyuta.
10.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS D kwa mwezi.
11.0 MTHAMINI DARAJA LA II (VALUER GRADE II) – NAFASI 7
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Nachingwea, Sengerema na Tunduru.
11.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukusanya taarifa za utafiti na mwenendo wa soko la ardhi.
· Kuhakiki kumbukumbu za utafiti na kuziingiza kwenye kompyuta
11.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika fani ya Land
management and Valuation kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi au Taasisi nyingine
zinazotambuliwa na Serikali katika fani za Usimamizi Ardhi na
Uthamini. Au
·Kuajiriwa wenye cheti cha NCPS katika fani ya Usimamizi Ardhi na Uthamini.
11.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS E kwa mwezi.
12.0 MKADIRIAJI UJENZI DARAJA LA II (QUANTITY SURVEYOR GRADE II) – NAFASI 4
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Urambo na Sengerema.
12.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuandaa ratiba ya kazi, gharama za ujenzi (BOQ) na Hati za mikataba.
· Kuanda makisio ya gharama za miradi ya Ujenzi.
·Kukusanya takwimu na kufanya uchunguzi ( survey)ya ukarabati wa miradi ya Ujenzi
·Kuandaa bajeti ya miradi ya ujenzi
· Kuandaa taarifa za uthamini wa miradi ya ujenzi.
· Kwa kushirikiana na Mkadiriaji ujenzi kuandaa taarifa fupi za ujenzi wa miradi.
·Kushughulikia masuala yote ya utawala wa fedha za miradi, kuandaa hati / vibali maalumu vya ujenzi na mikataba.
· Kufanya kazi zingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
12.2 SIFA ZA MWOMBAJI
·Awe
na Shahada /Stashahada ya juu ya Uhandisi kutoka vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Ukadiriaji Ujenzi (quantity
Surveryor).
12.3 MSHAHARA.
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Serikali TGS E kwa mwezi
13.0 AFISA UFUGAJI NYUKI DARAJA LA II (BEEKEEPING OFFICER GRADE II) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela.
13.1 MAJUKUMU YA KAZI
·Kusimamia uanzishaji wa hifadhi za nyuki na manzuki.
·Kutangaza Sera na Sheria za ufugaji nyuki.
· Kufundisha masomo ya fani ya ufugaji nyuki.
· Kukusanya takwimu za rasilimali na ufugaji nyuki.
· Kupanga na kupima ubora wa mazao ya nyuki.
13.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Shahada katika fani ya Ufugaji Nyuki au Sayansi ya Elimu ya
Mimea, Elimu ya Wadudu au Elimu ya Wanyama kutoka Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam au Vyuo vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
13.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.D kwa mwezi
14.0 MHANDISI DARAJA LA II – NISHATI (ENERGY ENGINEER) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini na Katibu Tawala Mkoa wa Geita na Tanga.
14.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya
kazi chini ya uangalizi wa mhandisi aliyesajiliwa na bodi ya Usajili wa
Wahandisi kama “Professional Engineer” ili kupata uzoefu unaotakiwa.
· Kufanya
kazi kwa vitendo katika fanii zinazomhusu ili kumwezesha Mhandisi
kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi.
· Kufuatilia taarifa za upatikanaji, uzalishaji, ugavi na matumizi ya nishati.
· Kukusanya taarifa na takwimu kuhusu miradi mbalimbali kuhusu bei za nishati ndani na nje ya nchi.
· Kupitia mapendekezo ya miradi project proposals mbalimbali ya nishati yanayowasilishwa Wizarani.
· Kuhakiki maombi ya wawekezaji na mkandarasi kuhusu vivutio vya uwekezaji.
14.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
mwenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za Uhandisi wa
Nishati (Renewable Energy, Mechanical Engineering or Elecrical
Engineering)
14.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
15. MSANIFU MAJENGO (ARCHITECT) DARAJA LA II – (NAFASI 3)
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Jiji la Mwanza,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma na Mkurugenzi Halmashauri ya
Manispaa ya Singida.
15.1 MAJUKUMU YA KAZI
·
Kufanya kazi chini ya uangalizi wa Msanifu majengo aliyesajiliwa na
Bodi ya Usajili husika kama “Proffessional Archtect” ili kupata uzoefu
unaotakiwa
·
Kufanya kazi kwa vitendo katika fani zinazomhusu ili kumwezesha kupata
sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili inayowahusu Wasanifu
majengo
·Kufuatilia upatikanaji wa taarifa za taaluma ya usanifu wa majengo
·Kupitia mapendekezo ya miradi (Project Proposals) mbalimbali ya majengo yanayowasilishwa.
15.3 Sifa za mwombaji
Kuajiriwa
wenye Shahada/ Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka vyuo vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika fani ya Wasanifu Majengo
15.3 Mshahara
Kwa kuzingatia viwango vya mishahara vya Serikali yaani TGS E.
16.0 MJIOLOJIA DARAJA LA II (GEOLOGIST GRADE II) – NAFASI 7
Nafasi hizi ni kwa kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.
16.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kupokea
na kufuatilia upatikanaji wa taarifa za utafiti wa mistari ya uchungi
na mitetemo katika utafutaji wa madini au petroli;
· Kukusanya na kuchambua taarifa za mitetemo, mienendo na mabadiliko ya miamba ardhini;
· Kutunza kumbukumbu za miamba, madini au petroli;
· Kutayarisha rasimu za taarifa za kitaalam na kuziwasilisha kunakohusika;
· Kusimamia matumizi ya vifaa vya kitaalam na utunzaji wake; na
· Anaweza kuongoza timu ya mafundi sanifu wanapokuwa katika shughuli za utafutaji wa madini au petroli.
16.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Shahada ya Sayansi katika fani ya Jiolojia (pamoja na fani za
Jiofizikia au Jiokemia) au sifa nyingine zinazolingana na hizo kutoka
vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali,
16.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
17.0 FUNDISANIFU DARAJA LA II (UJENZI) – (CIVIL TECHNICIAN GRADE II) – NAFASI 26
Nafasi
hizi ni kwa kwa ajili ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida na Morogoro,
Mkurugerugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Mpanda, Mbulu,
Meatu, Ilemela, Sengerema, Tunduru, Bukoba Ngorongoro na Kyela na
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe.
17.1 MAJUKUMU YA KAZI
Mafundi
sanifu watapangiwa kazi na Mamlaka zinazohusika katika fani zao
kutegemea cheo, ujuzi, uzoefu na uwezo wao na utendaji mzuri wa kazi
kama ifuatavyo:-
· Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba;
· Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”;
· Kufanya kazi za upimaji (survey) wa barabara, majengo na mifereji kama atakavyoelekezwa;
· Kuwapangia kazi Mafundi sanifu wasaidizi na kuhakikisha wanamaliza kama ilivyopangwa.
17.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
· Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani za ufundi.
· Waliohitimu
kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya
Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za ufundi,
· Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
· Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
17.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
18.0 MVUVI MSAIDIZI DARAJA LA II (FISHERIES ASSISTANT II) – NAFASI 8
Nafasi
hizi ni kwa kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi,
Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Tunduru, Nachingwea, Pangani na Same,
Mkurugenzi Halmashauri ya Mji Njombe.
18.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutengeneza, Kushona, Kutunza na Kukarabati zana za uvuvi.
· Kutunza na kuangalia mabwawa ya samaki.
· Kutega mitego Ziwani au Baharini.
· Kutengeneza nyavu ndogo ndogo.
· Kuwapa chakula samaki katika mabwawa.
· Kuvua samaki katika mabwawa.
· Kutoa ushauri kwa wavuvi kuhusu mbinu mbalimbali za uvuvi.
· Kukusanya takwimu za uvuvi kutoka kwenye vituo vya kupokelea samaki.
· Kutoa ushauri juu ya uhifadhi wa samaki na mbinu za usambazaji na uuzaji wa mazao yatokanayo na samaki.
· Kuwaelimisha wananchi juu ya ufugaji wa samaki na mambo muhimu ya kuzingatia.
18.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye stashahada (Diploma) ya
Uvuvi au Uhifadhi wa Samaki na Masoko (Fish Processing & Marketing)
kutoka vyuo vya uvuvi vya Mbegani, Kunduchi au vyuo vingine
vinavyotambuliwa na Serikali.
18.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS C kwa mwezi
19.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) (ASISTANT TECHNICIAN – WATER) NAFASI 19
Nafasi
hizi ni kwa kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na
Ushirika, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya
Rugwe na Busega na Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
19.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kupima uwingi wa maji mtoni
· Kusoma kituo cha hali ya hewa
· Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
19.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha VI waliohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka
mmoja kutoka kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali ambao wana cheti cha ufundi Daraja la III katika fani ya maji.
19.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
20.0 NAHODHA DARAJA LA II – NAFASI 6 (SKIPPER GRADE II)
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Chunya.
20.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kubuni na kuunda zana za kuvulia samaki (Fishing Gears).
· Kutunza na kutengeneza zana za kuvulia samaki.
· Kuongoza na kuendesha meli/boti ndogo za futi 40 zenye uzito wa kuandikishwa wa tani 50-200 (GRT).
· Kuendesha shughuli za uvuvi katika meli/boti.
20.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha sita (VI) wenye Stashahada (Diploma) ya Unahodha
na Uvuvi (Master Fisherman) kutoka Chuo cha Uvuvi Mbegani au vyuo
vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
20.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.C kwa mwezi.
21.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – HAIDROLOJIA – (TECHNICIAN GRADE II – HYDROLOGY) – NAFASI 6
Nafasi hii ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Songea
21.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Ukusanyaji na ukaguaji wa takwimu za maji
· Kutunza takwimu za maji
· Kuingiza takwimu za maji kwenye fomu Na: H: 12 tayari kwa kutumiwa kwenye michoro
· Kuchora hydrograph za maji
· Utengenezaji visima vya rekoda, stendi za winchi, sinia za maji ‘cable way post” n.k.
· Kufanya matengenezo ya vifaa vyote vya kupimia maji na hali ya hewa
· Kuingiza takwimu kwenye kompyuta
· Kufundisha wasoma vipimo
21.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana
cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Rasilimali za Maji na wenye
ujuzi wa kutumia kompyuta.
21.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
22.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – HAIDROJIOLOJIA (TECHNICIAN GRADE II – HYDROGEOLOGIST) – NAFASI 6
Nafasi
hizi ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Katibu Tawala Mkoa wa
Mwanza na Geita, Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Songea.
22.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuhakiki nuwezo wa kisima kutoa maji (Pump test)
· Kuchora ramani za eawali za kiufundi
· Kuhifadhi taarifa za kikazi (Field Data) zipatikanazo wakati wa utafiti wa maji chini ya ardhi.
22.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
Wahitimu wa vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali ambao wana
cheti cha ufundi ( FTC) au Stashahada ya Kawaida ya Rasilimali za Maji
na wenye ujuzi wa kutumia kompyuta.
22.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
23.0 MSAIDIZI MISITU DARAJA LA II (FORESTRY ASSISTANT GRADE II) – NAFASI 7
Nafasi hizi ni kwaajili ya Mkurugenzi Halmashauri Wilaya ya Tunduru, Busega, Meatu, Urambo na Chamwino.
23.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukusanya mbegu
· Kuhudumia na kutunza bustani za miti.
· Kutunza na kuhudumia miti na misitu.
· Kufanya doria.
· Kusimamia ukusanyaji mbegu na bustani za miti.
· Kukusanya takwimu za misitu.
· Kusimamia kazi za upandaji, utunzaji na uvunaji wa miti/misitu.
· Kukusanya maduhuli.
· Kupima mazao ya misitu.
· Kufanya doria.
23.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha Nne au Sita wenye Astashahada (Cheti) au
Stashahada (Diploma) ya Misitu kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
23.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B/C kwa mwezi
24.0 FUNDI SANIFU DARAJA II – RAMANI (TECHNICIAN GRADE II – (MAPPING) – NAFASI 6
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Ilemela, Busega, Kishapu, Morogoro na Nachingwea.
24.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kushughulikia madaai/malalamiko ya hati za viwanja, kuweka na kutunza kumbukumbu zake
· Kutunza kumbukumbu za “cadastrals surveys” na mahesabu yake
· Kuandaa nakala za “cadastral site plans”
· Kutunza miongozo ya ramani (maping guides) na viwanja
24.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye wahitimu wa kidato cha nne au sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Ramani (Mapping)
24.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.
25.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – (TECHNICIAN GRADE II – COMMUNITY DEVELOPMENT) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwaajili ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida na Mkurugenzi Halmashuri ya Wilaya ya Ilemela.
25.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufundisha wanavijiji teknolojia na ufundi
· Ujenzi wa nyumba bora za gharama nafuu
· Kusimamia utengenezaji wa majiko bora , ufinyanzi, uhunzi na useremla
· Utengenezaji
wa nyenzo za usafiri kama mikokoteni, uchimbaji wa visima, ujenzi wa
vyoo bora, ujenzi wa mabanda na usimikaji wa mashine za kusaga
· Kusaidia, kuanzisha na kutoa ushauri wa kiufundi kwa vikundi vya ujenzi
· Kuratibu shghuli za ufundi na teknolojia katika ngazi ya kata
· Kutoa ushauri kuhusu miradi ya ujenzi, ufundi na teknolojia
· Kufuatilia utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya ujenzi, ufundi na teknolojia
· Kuandaa taarifa ya mwezi, robo mwaka, nusu mwaka na mwaka mzima kuhusu shughuli zote za ujenzi, ufundi na teknolojia.
25.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
· Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya fundi sanifu maendeleo ya
jamii
· Waliohitimu
kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi sanifu maendeleo ya jamii ya
miaka mitatu kutoka Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika
fani ya fundi sanifu maendeleo ya jamii
· Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
· Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi sanifu maendeleo ya jamii kutika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
25.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
26.0 DEREVA MITAMBO DARAJA LA II (PLANT OPERATOR GRADE II) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Meatu
26.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuendesha mitambo chini ya usimamizi wa Dereva Mitambo mwenye uzoefu.
26.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye cheti cha Kidato cha IV ambao wana leseni Daraja la “G” ya
kuendesha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo
hiyo, wenye uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu
(300) au miezi mitatu (3) bila kusababisha ajali.
26.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi
27.0 MPIGA CHAPA MSAIDIZI (ASSISTANT PRINTER) – NAFASI 5
Nafasi hizi ni Kwaajili ya Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu.
27.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukunja
karatasi ngumu na kutengeneza ‘covers’ za vitabu, majarida, madaftari
katika mahitaji mbalimbali kwa kugandisha, kuweka pamoja au kushona
katika hali mbalimbali za ubora.
· Kukarabati
vitabu, kumbukumbu mbalimbali au majarida kwa kuyawekea gamba jipya, au
kurudisha katika hali yake ya mwanzo kutegemea na kifaa hicho
kilivyoharibika.
· Kupanga vifaa vilivyotengenezwa katika makasha kwa vipimo vyake au katika seti.
· Kuendesha
mashine za kukata karatasi/kupiga Chapa/Mashine za Composing, kushona
au kugandisha vitabu, majarida, madaftari na vifaa vingine vinavyokuwa
vimetakiwa kwa mtindo na ubora wake.
· Kupanga
karatasi zitakazochapwa kwa hesabu ya kila kitabu, jarida, daftari na
vinginevyo kwa kushonwa au kugandishwa pamoja.
27.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha IV au VI katika masomo ya Sayansi, au Sanaa,
wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Daraja la I (Trade Test Grade I)
katika Lithography/Composing/Binding/Machine Minding, au waliohitimu
mafunzo ya miaka miwili ya Kupiga Chapa.
27.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi
28.0 OPERATA WA KOMPYUTA MSAIDIZI (ASSISTANT COMPUTER OPERATOR) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni Kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
28.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuhifadhi data.
· Kutunza kumbukumbu za shughuli za kila siku.
· Kugundua na kusahihisha makosa yanayotokea katika data.
· Kufanya kazi za Kompyuta.
· Kuchapa orodha ya makosa.
· Kufanya programu ya matumizi.
· Kuchapa taarifa za mwisho.
· Kufanya kazi chini ya usimamizi wa Opereta wa Kompyuta Daraja la II.
28.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye cheti cha masomo ya Kompyuta (Certificate in Computer Science in
Information Technology) kutoka kwenye Taasisi/Chuo kinachotambuliwa na
Serikali.
28.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.B kwa mwezi.
29.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – MIGODI (MINING TECHNICIAN GRADE II) – NAFASI 9
Nafasi hizi ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini.
29.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kukagua na kupima viwanja kwa ajili ya waombaji wadogo wadogo
· Kusimamia wapimaji na kuhakikisha wanapima kwa kiwango kinachotakiwa
· Kuandaa “action plan” na kuhakikisha inafuatwa
29.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
· Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani za ufundi.
· Waliohitimu
kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya
Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za ufundi,
· Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
· Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi kutika Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
29.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
30.0 POLISI MSAIDIZI (AUXILIALRY POLICE) – NAFASI 5
Nafasi hii ni kwaajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke.
30.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuwa mlinzi wa Usalama wa watu na mali zao katika halmashauri
· Kuhifadhi maisha na mali za halmashauri
· Kuhifadhi maisha na mali za mtu yeyote katika maeneno maalum
· Kulisaidia Jeshi la Polisi kuhifadhi Sheria na utengamano katika maeneno maalum
· Kusaidia
Halmashauri katika masuala ya kuhifadhi Sheria katika kutekeleza
masuala/kazi kama ilivyoainishwa katika Sheria za Nchi
· Kuendesha shughuli za uhifadhi wa Sheria kama itakavyokuwa imeelekezwa na Inspekta Jenerali wa Polisi
· Kufanya kazi zingine kama atakavyopata maelekezo ya utendaji kutoka ngazi za juu za uongozi wa Polisi na Halmashauri.
30.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au
Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
· Kuajiriwa wenye sifa njema na asiwe na makosa ya Jinai
· Awe anajua kusoma na kuandika Kiswahili na Kiingereza
30.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TPSW 1 kwa mwezi.
31.0 MPOKEZI (RECEPTIONIST) – NAFASI 1
Nafasi hii ni Kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi.
31.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kupokea wageni na kuwasaili shida zao.
· Kutunza
rejesta ya wageni wa ofisi na kufanya uchambuzi wa wageni wanaoingia
ili kutoa ushauri juu ya utaratibu bora wa kupokea wageni.
· Kupokea na kusambaza maombi ya simu za ndani.
· Kutunza na kudumisha usafi wa “Switchboard” na ofisi zake.
· Kuwaelekeza wageni wa ofisi kwa maafisa/ofisi watakakopewa huduma.
· Kuhakikisha kwamba wageni wanaoingia ndani wanamiadi (Appointment) au wamepata idhni ya maafisa husika.
· Kupokea simu kutoka nje na kuzisambaza kwa maofisa mbalimbali ofisini.
· Kupokea simu kutoka “Extension” za ndani na kupiga nje ya ofisi.
· Kutunza rejesta ya simu zinazopokelewa kutoka nje ya ofisi na zinazopigwa kwenda nje.
31.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha IV waliofaulu masomo ya Kiingereza, Kiswahili na
Hisabati na kufuzu mafunzo ya Mapokezi na Upokeaji Simu kutoka vyuo
vinavyotambuliwa na Serikali.
31.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
32.0 KATIBU MAHSUSI DARAJA LA III (PERSONAL SECRETARY GRADE III) – NAFASI 10
Nafasi hizi ni kwaajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Handeni na Pangani.
32.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida.
· Kusaidia kupokea wageni na kuwasaili shida zao, na kuwaelekeza sehemu wanapoweza kushughulikiwa.
· Kusaidia
kutunza taarifa/kumbukumbu za matukio, miadi, wageni, tarehe za vikao,
safari za Mkuu wake na ratiba ya kazi zingine zilizopangwa wakati
unaohitajika.
· Kusaidia
kutafuta na kumpatia Mkuu wake majadala, nyaraka au kitu chochote
kinachohitajika katika shughuli za kazi hapo ofisini.
· Kusaidia
kufikisha maelekezo ya Mkuu wake wa kazi kwa wasaidizi wake na pia
kumuarifu kuhusu taarifa zozote anazokuwa amepewa na wasaidizi hao.
· Kusaidia
kupokea majalada, kuyagawa kwa Maofisa walio katika sehemu alipo, na
kuyakusanya, kuyatunza na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
· Kutekeleza kazi zozote atakazokuwa amepangiwa na Msimamizi wake wa kazi.
32.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha IV waliohudhuria Mafunzo ya Uhazili na kufaulu
mtihani wa Hatua ya Tatu. Wawe wamefaulu somo la Hatimkato ya Kiswahili
na Kiingereza maneno 80 kwa dakika moja na wawe wamepata mafunzo ya
Kompyuta kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali na kupata
cheti katika programu za Window, Microstoft Office, Internet, E-mail na
Publisher.
32.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi.
33.0 MLINZI (SECURITY GUARD) – NAFASI 100
Nafasi
hizi ni kwaajili ya katibu Mkuu Wizara ya Fedha,Katibu Mkuu Wizara ya
Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, katibu Mkuu Wizara ya Nishati na
Madini, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Katibu Mkuu
Wizara ya Kazi, Katibu Tawala Mkoa wa Iringa, Kagera, Mwanza, Morogoro,
Geita, Kilimanjaro, Lindi, Tabora na Katavi, Mkurugenzi Halmashauri ya
Jiji Mwanza, Mkurugenzi Manispaa ya Shinyanga, Mkurugenzi Halmashauri ya
Wilaya Kyela, Biharamulo, Bukoba, Songea, Mbinga, Tunduru, Busega,
Meatu, Ruangwa, Nachingwea, Same, Urambo, Chamwino na Nanyumbu.
33.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuhakikisha kwamba mali yoyote ya ofisi inayotolewa langoni (nje ya ofisi) ina hati ya idhini.
· Kuhahikisha kuwa mali yote inayoingizwa langoni inazo hati za uhalali wake.
· Kulinda usalama wa majengo, ofisi na mali za ofisi mchana na usiku.
· Kuhakikisha kwamba milango na madirisha yote yamefungwa ipasavyo mwisho wa saa za kazi.
· Kuhakikisha kwamba wageni wote wanaoingia katika eneo la ofisi wana idhini ya kufanya hivyo.
· Kupambana
na majanga yoyote yatakayotokea katika sehemu ya kazi kama vile, moto,
mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika kama vile,
moto, mafuriko n.k na kutoa taarifa katika vyombo vinavyohusika.
· Kutoa ushauri wa jinsi ya kuboresha huduma ya ulinzi mahali pa kazi.
33.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mgambo/polisi/JKT au
Mafunzo ya Zimamoto kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Serikali.
33.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya mshahara TGOS.A kwa mwezi.
34.0 DEREVA DARAJA LA II (DRIVER II) – NAFASI 178
Nafasi
hizi ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Kazi na Ajira, Katibu Mkuu
Wizara ya Viwanda na Biashara, Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi na
Teknolojia, Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini, Katibu Mkuu Wizara
ya Kilimo Chakula na Ushirika, Katibu
Mkuu
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu Wizara
ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, na Katibu Mkuu Wizara ya Mamba ya Ndani
ya Nchi, Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Katibu Tawala Mkoa wa Geita,
Katibu Tawala Mkoa wa Pwani, Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Katibu Tawala
Mkoa wa Lindi, Katibu Tawala Mkoa wa Manyara, Katibu Tawala Mkoa wa Dar
es Salaam, Mkurugenzi Jiji la Mwanza, Mkurugenzi Halmashauri Manispaa ya
Singida na Mkurugenzi Halmashauri Wilaya Biharamulo, Namtumbo,
Sengerema, Kilosa, Rorya, Ruangwa, Mbulu, Chamwino, Pangani na Nanyumbu.
34.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuendesha magari ya abiria, magari madogo na malori
· Kuhakikisha
gari na vyombo vyake vipo katika hali nzuri wakati wote, na kufanya
uchunguzi wa gari kabla na baada ya safari ili kugundua ubovu unaohitaji
matengenezo,
· Kufanya matengenezo madogo madogo katika gari,
· Kutunza na kuandika daftari la safari “Log-book” kwa safari zote.
34.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye Cheti cha Mtihani wa Kidato cha IV, Wenye Leseni daraja la “C” ya
uendeshaji pamoja na uzoefu wa kuendesha magari kwa muda usiopungua
miaka mitatu bila kusababisha ajali na wenye Cheti cha Majaribio ya
ufundi Daraja la II.
34.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
35.0 MSAIDIZI WA OFISI (OFFICE ASSISTANT) – NAFASI 30.
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya
Viwanda na Biashra, Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Manyara na Lindi, Mkurugenzi Halmashauri ya
Wilaya Kyera, Bukoba, Songea, Mbinga, Tunduma, Busega, Singida,
Nachingwea, Monduli na Ngorongoro.
35.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya
usafi wa ofisi na mazingira ya nje na ndani ikiwa ni pamoja na kufagia,
kufuta vumbi, kupiga deki, kukata majani, kupalilia bustani, kumwagilia
maji bustani, kupanda maua au miti na kusafisha vyoo.
· Kuchukua na kupeleka majalada na hati nyingine kwa maofsa waoaohusika na kuyarudisha sehemu zinazohusika.
· Kusambaza barua za Ofisi kama jinsi atakavyoelekezwa.
· Kutayarisha chai ya ofisi.
· Kupeleka mfuko wa posta na kuchukua barua kutoka Posta.
· Kuhakikisha kwamba vifaa vya ofisi vinaweka sehemu zinazostahili.
· Kufungua Milango na Madirisha ya Ofisi wakati wa Asubuhi na Jioni kuyafunga baada ya Saa za Kazi.
· Kudurufu barua au machapisho kwenye mashine za kudurufia.
· Kuweka katika majalada nakala za barua zilizochapwa katika ofisi walizomo.
· Kutunza vifaa vya ofisi na kutoa ripoti kila vinapoharibika.
35.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliofaulu vizuri katika masomo ya Kiingereza, Kiswahili na Hisabati.
35.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
36.0 AFISA KUMBUKUMBU DARAJA LA II (RECORDS OFFICER GRADE II) – NAFASI 1.
Nafasi hii ni kwa ajili ya Katibu Ofisi ya Rais Maadili ya Viongozi.
36.1 MAJUKUMU YA KAZI
Hili
ni daraja la mafunzo katika kazi hivyo atafanya kazi kwa maelekezo ya
Maafisa Kumbukumbu walio juu yake kwa cheo. Kazi atakazojifunza na
kufanya ni zile zifanywazo na Afisa Kumbukumbu Daraja la I:-
· Kudhibiti mifumo ya kumbukumbu, kutunza, na kusimamia matumizi ya kumbukumbu.
· Kutambua na kutafuta kumbukumbu katika masjala.
· Kudhibiti mfumo wa kumbukumbu zinazozalishwa na kompyuta, kutunza na kusimamia matumizi yake.
36.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
mwenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Utunzaji na Uhifadhi wa
Kumbukumbu (Records management & Archieves), Upimaji na Ramani na
nyingine zinazolingana nayo kutoka katika Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na
Serikali. Aidha wawe na ujuzi wa kutumia kompyuta.
36.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
37.0 MWENYEKITI WA MABARAZA YA ARDHI NA NYUMBA YA WILAYA(CHAIRPERSON) – NAFASI 5.
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Makazi.
37.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kusikiliza,
kuamua migogoro yote ya Ardhi na Nyumba kwa mujibu wa Sheria Na 2 ya
mwaka 2002 inayohu Mabaraza ya Ardhi na Nyumba ya Wilaya
· Kusikiliza na kutoa uamuzi wa Rufaa kutoka Mabaraza ya Kata
· Kufanya marejeo kwa mashauri yaliyosikilizwa na mabaraza ya Kata.
· Kusimamia utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Ardhi na Nyumba la wilaya na Mabaraza ya Kata katika eneo husika.
37.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Shahada ya Sheria na kuendelea kutoka Chuo kikuu kinachotambulika
na serikali na kumaliza mafunzo ya kazini (internship)
· Awe na uzoefu wa miaka mitano (5) katika masuala ya Sheria na Kutolea uamuzi
· Awe mwadilifu na asiye na historia ya makosa ya jinai
· Awe na umri usiopungua miaka 35
37.3 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.J kwa mwezi.
38.0 AFISA MTENDAJI WA KATA DARAJA LA III (WARD EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 10.
Nafasi hizi ni kwaajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya Bukoba, Mbinga, Tunduru, Msalala, Mpanda, Pangani na Nanyumbu.
38.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Kata na kiungo cha Uongozi kwa Idara zote katika kata na atashughulikia masuala yote ya kata
· Atakuwa Mhamasishaji mkuu wa Umma katika mikakati mbalimbali ya uzalishaji, mali, kuondoa njaa na Umasikini.
· Atakuwa ni Katibu wa kamati ya maendeleo ya kata.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa shughuli za maendeleo ya kata, vijiji na vitongoji.
· Atatafsiri
sera na kusimamia utekelezaji wa sheria ndogondogo katika Kata
yake.Atamsaidia Mkurugenzi Kuratibuna kusimamia shughuli za Uchaguzi
katika Kata.
· Kumsaidia na kumwakilisha Mkurugenzi katika kusimamia maendeleo ya eneo lake.
· Kusimamia utendaji kazi wa wataalamu na watendaji wengine katika ngazi ya Kata.
· Kuratibu na kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha kwa mkurugenzi na nakala kwa Katibu Tarafa.
· Atakuwa mwenyekiti katika vikao vya vinavyowahusisha wataalamu na watendaji wa vjiji, na NGO’S katika kata yake.
· Atakuwa Msimamizi na mratibu wa takwimu zote zinazokusanywa katika vijiji, vitongoji, na kata yake.
38.3 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa
waliohitimu kidato cha nne au sita na kuhudhuria mafunzo ya Stashahada
yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences) Utawala, (Public
Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya Sheria au Sifa
nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na
Serikali.
38.4 MSHAHARA
· Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.
39.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA II (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER GRADE II) – NAFASI 6.
Nafasi hizi ni kwaajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Maswa na Mtwara.
39.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa
Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika
Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya kijiji
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.
· Ataratibu
na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata .
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.
39.3 SIFA ZA MWOMBAJI.
· Kuajiriwa
wenye elimu ya kidato cha IV na VI waliohitimu Stashahada ya kawaida
katika fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii (Social Sciences)
Utawala, (Public Administration and Local Gorvernment), Stashahada ya
Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo kutoka Chuo chochote
kinachotambuliwa na Serikali.
39.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS C kwa mwezi.
40.0 AFISA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA III (VILLAGE EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 232.
Nafasi
hizi ni kwaajili ya Mkurugunzi Halmashauri ya Wilaya Rungwe, Tunduru,
Mbeya, Muleba, Mbinga, Msalala, Nachingwea, Chamwino, Nanyumbu,
Sengerema, Shinyanga, Kishapu, Mkuranga, Ngorongoro, Simanjiro, Mpanda,
Mtwara na Tandahimba.
40.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa
Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Kijiji na Kamati zake katika
Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya kijiji
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Kijiji.
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya kijiji
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Kijiji.
· Ataratibu
na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Kijiji na baadae kwenye kata.
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Kijiji.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika kijiji.
40.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada
(Certificate) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii
(Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local
Gorvernment), Astashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na
hizo kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
40.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.
41.0 AFISA MTENDAJI MTAA DARAJA LA III (MTAA EXECUTIVE OFFICER GRADE III) – NAFASI 3.
Nafasi hizi ni kwaajili ya Mkurugenzi Halmashauri Manispaa Kigoma/Ujiji.
41.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Atakuwa
Mtendaji na Mshauri Mkuu wa Serikali ya Mtaa na Kamati zake katika
Mipango ya Maendeleo ya kijamii na Utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo.
· Atakuwa Afisa Mhasibu wa Serikali ya Mtaa na atasimamia mapato na matumizi ya Serikali ya Mtaa
· Atakuwa Mlinzi wa Amani na Msimamizi wa Utawala Bora katika Mtaa
· Ataratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa Mipango ya Maendeleo ya Mtaa
· Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Mtaa.
· Atatafsiri Sera, ataratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogondogo za Halmashauri ya Mtaa
· Ataratibu
na kuandaa taarifa ya utekelezaji wa kazi katika eneo lake na
kuziwasilisha kwenye Halimashauri ya Mtaa na baadae kwenye Kata.
· Ataongoza vikao vya maendeleo ya Mtaa vitavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake.
· Atahamasisha wananchi katika kampeni za kuondoa njaa, umasikini, na kuongeza uzalishaji mali.
· Atasimamia matumizi bora ya Nguvu kazi.
· Atakuwa Kiongozi wa Wakuu wa Vitengo vya Kitaalamu Katika Mtaa.
· Atasimamia ukusanyaji wa kumbukumbu za walipa kodi, wataalamu mbalimbali na NGO waliopo katika Mtaa.
41.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
wenye Elimu ya Kidato cha Nne au cha sita waliohitimu Astashahada
(Certificate) katika Fani yoyote yenye mwelekeo wa Sayansi ya Jamii
(Social Sciences) Utawala, (Public Administration and Local
Gorvernment), Atashahada ya Sheria au Sifa nyingine inayolingana na hizo
kutoka Chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
41.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali ngazi ya Mshahara TGS B kwa mwezi.
42.0 AFISA LISHE II (NUTRITON OFFICEER II) – NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe, Chunya na Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga.
42.1 Majukumu ya Kazi
· Kukusanya
taarifa na takwimu za lishe kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali na
kutoa ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi ya wilaya.
· Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa ya watoto na makundi mengine yenye lishe duni.
· Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya lishe katika ngazi ya wialaya.
· Kutoa taarifa za mara kwa mara za hali ya lishe katika ngazi ya wilaya.
· Kusimamia kazi za lishe katika wilaya
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
42.2 Sifa za mwombaji
Kuajriwa
wenye Shahada ya kwanza ya Lishe, Sayansi Kimu na Lishe au Sayansi na
Chakula na Teknolojia ya Chakula (BSc – Nutrition, Home Economics and
Nutrition, Food Science and Technology Food Science) au Stashahada ya
juu ya Lishe (Higher Diploma in Nutrition) kutoka chuo kinachotambuliwa
na Serikali.
42.3 Mshahara
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali TGS D kwa mwezi.
43.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – UFUNDI NA UMEME (TECHNICIAN GRADE II MECHANICS & ELECTRICAL) – NAFASI 12
Nafasi
hizi ni kwa ajili ya, Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika,
Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na Kishapu Halamshauri za Manispaa ya
Morogoro na Songea na Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu.
43.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya ukaguzi wa ubora wa magari ya Serikali na kurekebisha ipasavyo.
· Kufanya upimaji wa Mitambo na Umeme kufuatana na Maelekezo ya Mhandisi.
· Kufanya kazi za kutengeneza mitambo, magari,na vifaa vya Umeme
· Kufanya usanifu wa miradi midogo midogo ya umeme
· Kusimamia jinsi ya kufunga mashine mpya zinazowekwa kwenye karakana za ufundi na Umeme.
43.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
· Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika moja ya fani za ufundi.
· Waliohitimu
kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka Vyuo vya
Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za ufundi,
· Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
· Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
43.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
44.0 AFISA BIASHARA MSAIDIZI (ASSISTANT TRADE OFFICER II) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwaajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
44.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuandaa Takwimu za Mahitaji kutokana na bidhaa zinazowasilishwa hapa nchini.
· Kuandaa takwimu zinazoonyesha tofauti kati ya mahitaji na uzalishaji.
· Kukusanya na kuunganisha (compile) nyaraka za Sera za Biashara na Sheria za Biashara.
· Kuandaa
sifa ya Biashara na huduma ambazo zinauzwa nchi za nje kwa kila sekta
kama vile Kilimo, Madini, Nguo na kadhalika na kuandaa sifa za kampuni
zinazouza nje.
· Kukusanya takwimu za biashara kutoka kila wilaya, kuzichambua na kutathmini mwenendo wa biashara kwa kila wilaya.
· Kukusanya
takwimu kutoka kwa wafanya biashara ambao wanauza na kununua kutoka
masoko ya nje kama vile SADC, EAC, EU, U.S.A
44.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye Stashahada ya Biashara kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali au sifa inayo lingana na hiyo.
44.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS B kwa mwezi
45.0 MCHAPA HATI DARAJA LA II – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwaajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
45.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuchapa taarifa za Uthamini na Hati za fidia
· Kuchapa Nyaraka na Hati za kumiliki ardhi
45.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa Kidato cha Nne au cha Sita waliofaulu mtihani wa Uhazili
Hatua ya II kutoka Chuo cha Watumishi wa Umma na ujuzi wa Kompyuta Hatua
ya I na II kutoka Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
45.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B
46.0 MHANDISI DARAJA LA II – BAHARINI (MARINE ENGINEER) – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya TEMESA.
46.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kusimamia ufungaji wa mitambo katika vyombo vya uvuvi.
· Kushauri juu ya aina za vyombo/mitambo inayoendeleza uvuvi.
· Kusimamia matengenezo ya vyombo vya uvuvi
· Kusimamia uendeshaji wa mitambo ya vyombo vya baharini
46.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye Shahada/Stashahada ya Juu ya Uhandisi kutoka Vyuo Vikuu
vinavyotambuliwa na Serikali katika mojwapo ya fani ya Uhandisi wa
Baharini.
46.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS E kwa mwezi.
47.0 DEREVA MITAMBO DARAJA LA II – (NAFASI 1)
Nafasi hii ni kwa ajili ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza
47.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuendesha mitambo chini ya usimaizi wa dereva mitambo mwenye uzoefu.
47.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye cheti cha Kidato cha IV ambao wana leseni Daraja la “G” ya
kuendesha mitambo na ujuzi wa kutunza vyombo mbalimbali vya mitambo
hiyo, wenye uzoefu wa kuendesha mitambo kwa muda usiopungua saa mia tatu
(300) au miezi mitatu (3) bila kusababisha ajali.
47.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS. A kwa mwezi.
48.0 DEREVA WA VIVUKO DARAJA LA II – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili ya TEMESA
48.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufunga na kufungua kamba za kivuko.
· Kuchunga usalama nwa abiria na magari yaliyomo ndani ya kivuko.
· Kupanga abiria au magari kwenye kivuko.
· Kuendesha na kuongoza kivuko.
· Kutunza daftari za safari ya kivuko.
· Kuhakikisha kwamba injini za kivuko zipo katika hali nzuri ya kufanya kazi.
· Kuangalia mafuta na vyombo vingine vya kufanyia kazi.
48.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
waliohitimu Mtihani wa Kidato cha IV, wenye Ujuzi wa kuendesha na
kutunza Mashua/Kivuko uliothibitishwa na Chuo cha Dar es Salaam Marine
Institute au Chuo kingine chochote kinachotambuliwa na Serikali kwa muda
usiopungua miaka miwili; na waliofuzu mafunzo ya miezi sita ya uokoaji
wa maisha majini, kuogelea na kupanga watu na magari kwenye
mashua/vivuko.
48.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGOS.A kwa mwezi.
49.0 MKUFUNZI MWANDAMIZI DARAJA II – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwa ajili ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA)
49.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufundisha wanafunzi wa mwaka 3 (NTA level 6)
· Kusimamia mitihani ya wanafunzi wa mwaka wa 3
· Kutayarisha na kuhuisha Mitaala ya chuo
· Kusimamia mafunzo ya vitendo
· Kusimamia wanafunzi walioko chini yake
· Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa Idara
49.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Shahada ya Uzamili katika fani Sanaa za Ufundi na Sanaa za Maonyesho (Muziki)
· Awe amesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Vyuo vya Ufundi (NACTE) mwenye uzoefu wa kazi wa miaka mitatu (3).
49.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani PTSS 13 -14 kwa mwezi.
50.0 MKUFUNZI DARAJA II – NAFASI 2
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TASUBA)
50.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufundisha wanafunzi wa mwaka wa 3 (NTA evel 6)
· Kusimamia mitihani ya wanafunzi wa mwaka wa 3
· Kuendesha, kusaidia utafiti na kazi za ushauri
· Kutayarisha nyenzo za kufundishia
· Kusimamia mafunzo ya vitendo
· Kusimamia wakufunzi walioko chini yake
· Kufanya kazi nyingine atakazopewa na mkuu wake wa Idara
50.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Awe
na Shahada ya kwanza katika fani ya Sanaa za Ufundi na Sanaa za
Maonyesho (Muziki) kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali mwenye
uzoefu wa kazi wa miaka mitatu (3).
50.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani PTSS 10-11 kwa mwezi
51.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (BOMBA) – (ASISTANT TECHNICIAN – PLUMBING) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
51.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kazi atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
51.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
waliomaliza kidato cha VI katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya
mwaka mmoja katika ya fani za Ufundi Bomba kutoka Chuo kinachotambuliwa
na Serikali. AU
· Kuajiriwa
waliomaliza kidato cha IV wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Hatua ya
II kutoka chuocha ufundi katika mojawapo ya fani za ufundi Bomba.
51.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
52.0 FUNDI SANIFU MSAIDIZI (UMEME) – (ASISTANT TECHNICIAN – ELECTRICAL) – NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
52.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya marekebisho madogo madogo ya umeme katika ofisi na nyumba za serikali.
· Kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
52.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
waliomaliza kidato cha VI katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya
mwaka mmoja katika ya fani za Ufundi Umeme kutoka Chuo kinachotambuliwa
na Serikali. AU
· Kuajiriwa
waliomaliza kidato cha IV wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi Hatua ya
II kutoka chuocha ufundi katika mojawapo ya fani za ufundi umeme.
52.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS A kwa mwezi.
53.0 MKUFUNZI DARAJA II (TUTOR GRADE II) – NAFASI 3
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi (Chuo Cha Ardhi Tabora)
NAFASI 1 – Usimamizi na Uthamini wa Ardhi (Land Management and Valuation) NAFASI 1 – Mipangomiji (Town Planing)
NAFASI 1 – Teknolojia ya Uchapaji (Printing Technology)
53.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufundisha
· Kutoa ushauri kwa wanachuo katika kazi maalum (projects).
· Kusimamia na kuongoza wanachuo katika kazi za darasani na nje.
· Kutoa ushauri wa kiufundi na kitaalam.
· Kuendesha tafiti na ushauri.
· Kuandaa taarifa za tathmini na mapendekezo ya mitaala ya masomo.
53.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
mwenye Shahada/Stashahada ya Juu katika mojawapo ya fani za Mipangomiji
(Town Planing), Usimamizi na Uthamini wa Ardhi (Land Management and
Valuation) na Teknolojia ya Uchapaji (Printing Technology) kutoka Chuo
Kikuu cha Ardhi au Vyuo Vikuu vingine vinavyotambuliwa na Serikali.
53.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS.E kwa mwezi
54.0 MKUFUNZI DARAJA LA II (TUTOR II) - JIOLOJIA – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini (Chuo cha Madini Dodoma)
54.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kutafsiri mihutasari ya mafunzo kwenye masomo
· Kuandaa mtiririko wa kila somo (lesson plan) kwa upande wa nadhari na vitendo
· Kufundisha kozi za stashahada na astashahada kwa upande wa nadharia na vitendo
· Kuandaa na kupanga somo la vitendo na kusimamia wanachuo wakati wa kujifunza
· Kupima maendeleo ya wanachuo kwenye mitihani kwa kipindi chote kinachohusika na kutunza alama zao
· Kupima
maendeleo ya wanachuo kwa kushirikiana na wahandisi wa
uchenjuaji/jiologia na wahandisi migodi wa viwandani wa mafunzo kwa
vitendo (Field Practicals)
· Kufanya kazi nyingine kulingana na kiwango cha elimu na fani yake kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi
54.3 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wenye Shahada ya Kwanza katika fani ya Sayansi ya Uhandisi wa
Uchenjuaji Madini,Jiolojia au Uhandisi Migodi kutoka chuo
kinachotambuliwa na Serikali na wenye uzoefu wa kazi usiopungua miaka
mitatu
54.3 MSHAHARA - TGS E
55.0 MKUFUNZI MSAIDIZI (TUTORIAL ASSISTANTS) – JIOLOJIA – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini (Chuo cha Madini Dodoma)
55.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuandaa mtiririko (lesson plan) wa somo.
· Kufundisha Kozi ya astashahada ya uchenjuaji madini,jiolojia na utafutaji wa madini na uhandisi migodi
· Kusimamia masomo ya vitendo chini ya usimamizi wa Mkufuniz Mkuu wa somo
· Kuandaa na kupanga vifaa kwa ajili ya somo la vitendo
· Kuwapima wanachuo wakati wa mazoezi ya somo la vitendo
· Anaweza kuteuliwa kuwa Mkuu wa Kitengo (maabara,karakana na “museum” n.k)
· Kufanya kazi nyingine kulingana na kiwango cha elimu na fani yake kadri atakavyopangiwa na mkuu wake wa kazi.
55.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne (IV)au sita (VI) waliofuzu mafunzo ya
Stashahada ya Uhandisi wa Uchenjuaji Madini,Jiolojia au Uhandisi Migodi
kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
55.3 MSHAHARA - TGS D
56.0 FUNDI SANIFU DARAJA II – UBUNIFU MIPANGO MIJI – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwaajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Rombo
56.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kumsaidia Afisa Mipangomiji katika kukusanya kumbukumbu za shughuli za mipango miji
· Kumsaidia kuhamasisha na kusimamia utekelezaji wa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na kata.
· Kumsaidia Afisa Mipangomiji katika kuandaa mipango ya matumizi ya ardhi ya vijiji na kata.
56.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya mipangomiji kutoka kwenye vyuo
vinavyotambuliwa na serikali.
56.3 MSHAHARA - TGS C
57.0 FUNDI SANIFU DARAJA II- URASIMU RAMANI (CARTOGRAPHY) – NAFASI 5
Nafasi
hizi ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya
Makazi, Katibu Tawala Mkoa wa Geita na Halmashauri ya Wilaya ya Pangani
57.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya maandalizi ya Uchoraji wa ramani za miji kadiri ya uwiano unaohitajika
· Kutunza kumbukumbu za ramani na plan
· Kuchora plani za hati miliki, upimaji, mashamba na vijiji
· Kutoa nakala za plani za hati za viwanja, mashamba na vijiji
57.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Urasimu Ramani (Cartography)
kutoka kwenye vyovinavyotambuliwa na serikali.
57.3 MSHAHARA– TGS C
58.0 FUNDI SANIFU DARAJA II- UCHAPAJI RAMANI (PHOTOLITHOGRAPHY) –
NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi
58.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuandaa vifaa vya uchapaji wa ramani,vitabu,vipeperushi n.k
· Kutoa nakala za picha za anga katika uwiano mbalimbali
· Kupanya maandalizi yanayohusu upigaji wa ramani na picha za anga.
· Kuchapa ramani.
·
58.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha nne au cha sita wenye cheti cha mafunzo ya
ufundi ya miaka miwili katika fani ya Uchapaji Ramani (photolithography)
kutoka kwenye vyuo vinavyotambuliwa na serikali.
58.3 MSHAHARA – TGS C
59.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II – MAABARA (LABORATORY TECHNICIAN II)
– NAFASI 13
Nafasi hizi ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.
59.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya mchanganuo (analysis) kikemikali ili kuthibitisha/kutathmini vielelezo (samples) vinavyohusika kwenye maabara.
· Kutunza vyombo vya maabara
· Kutayarisha vitendea kazi vya maabala kwenye masomo ya sayansi kwa vitendo
· Kutambua, Kuthibitisha na kuweka kumbukumbu za takwimu za vielelezo mbalimbali
· Kusaidia kazi za watafiti
59.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa
wahitimu wa kidato cha sita (vi) waliofuzu mojawapo ya mafunzo ya miaka
miwili (2) ya stashahada (Diploma) ya ufundi sanifu wa Maabara au sifa
zinazolingana na hizo kutoka katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.
59.3 MSHAHARA – TGS C
60.0 FUNDISANIFU MSAIDIZI ( UJENZI – CIVIL TECHNICIAN ) – NAFASI 1
Nafasi hii ni kwaajili ya Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu
60.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi za ujenzi wa kuta za nyumba na kupaka rangi na kufunga mabomba,
· Kuchonga vifaa vya nyumba za serikali ikiwa ni pamoja na samani “furniture”,
· Kufanya kazi za upimaji ( Survey ) wa barabara,majengo na mifereji kama atakavyoelekezwa,
60.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
waliomaliza kidato cha IV katika masomo ya Sayansi na kufuzu mafunzo ya
mwaka mmoja katika Fani ya Ufundi wa Ujenzi kutoka katika chuo
kinachotambuliwa na serikali,
Au
· Kuajiriwa
waliomaliza kidato cha IV wenye cheti cha Majaribio ya ufundi hatua ya
II kutoka chuo cha ufundi katika mojawapo ya fani ya ufundi wa Ujenzi.
60.4 MSHAHARA – TGS A
61.0 FUNDI SANIFU DARAJA LA II - (TECHNICIAN GRADE II – PLUMBING) – NAFASI 4
Nafasi hizi ni kwa ajili ya Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya ya Pangani.
61.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kufanya kazi za ufundi bomba atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
61.2 SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
· Waliohitimu
kidato cha VI na kufuzu mafunzo ya ufundi ya miaka miwili kutoka Chuo
kinachotambuliwa na Serikali katika fani ya fundi bomba (Plumbing)
· Waliohitimu
kidato cha IV na kufuzu kozi ya ufundi bomba ya miaka mitatu kutoka
Vyuo vya Ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za
ufundi Bomba,
· Wenye Cheti cha Majaribio ya Ufundi hatua ya I kutoka Chuo cha Ufundi kinachotambuliwa na Serikali
· Wenye Stashahada ya Kawaida katika fani za ufundi bomba kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
61.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
62.0 WAKUFUNZI WASAIDIZI (TUTORIAL ASSISTANTS) – NAFASI 54
Nafasi hizi ni kwaajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto
62.1 KITUO CHA KAZI
Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi.
62.2 MAJUKUMU YA KAZI
· Ukufunzi wa Masomo ya Ufundi kwenye Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi
62.3 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa waliohitimu kidato IV au VI na kufuzu mafunzo ya Stashahada zifuatazo:-
Ujenzi,Ushonaji,
Ufundi na Umeme, Kompyuta, Ufundi Magari, Uchomeleaji, Useremala na
Chakula na Lishe (Food and Nutrition). Kutoka katika vyuo vinavyo
tambuliwa na Serikali.
62.4 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi
63.0 BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA)
Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na 27 ya mwaka 1967.
63.1 MHASIBU MKUU DARAJA II
66.1.1 MAJUKUMU YA KAZI
· Kuratibu kazi ya kujibu hoja za ukaguzi.
· Kuandaa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha.
· Kuandaa na kuoanisha taarifa za mwezi za Benki.
· Kuandaa taarifa za ukaguzi wa fedha za mwaka.
· Kusimamia, kuthibitisha na kuidhinisha malipo.
· Kufanya kazi zingine kama atakavyoagizwa na msimamizi wake wa kazi.
66.1.2 SIFA ZA MWOMBAJI
· Kuajiriwa
mwenye Shahada ya Uzamili ya Uhasibu/ Biashara yenye mwelekeo wa
Uhasibu kutoka Chuo/Taasisi yoyote inayotambuliwa na Serikali.
· Awe na CPA (T).
· Mwenye uwezo wa kutumia mifumo ya kompyuta ya kiuhasibu.
· Awe na uzoefu wa kazi usiopungua miaka nane (8) mfululizo katika fani ya uhasibu.
66.1.3 MSHAHARA - PGSS 17
Do not send money to potential employers for interviews.
Where money is requested or you are in doubt please contact
us for clarification
MASHARITI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji
ambao tayari ni watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia
katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya
nafasi za kazi kwa waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi
ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji
waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye
anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini
(referees)
watatu wa kuaminika.
vi.
Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti
vya kidato cha nne na kidato cha sita kwawale waliofikia kiwango hicho
na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi
husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa
kudondoka kupotea.
- Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Computer Certificate
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.
viii. “Transcripts”,
“Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati
matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS)
HAVITAKUBALIWA.
ix. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
x. Waombaji
waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa
kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
xi. Waombaji
kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko
katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo
yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. WAAJIRI WOTE WALIOPO NJE YA DAR ES SALAAM WANAOMBWA KUSAMBAZA MATANGAZO HAYA KWENYE MBAO ZA MATANGAZO NA MAENEO MENGINE.
xiii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 9 Aprili, 2013
xiv. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya ajira HAURUHUSIWI.
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo.
Katibu,
|
AU
|
Secretary,
|
Sekretariati ya Ajira katika
|
Public Service Recruitment
| |
Utumishi wa Umma,
|
Secretariat,
| |
SLP.63100,
|
P.O.Box 63100
| |
Dar es Salaam.
|
Dar es Salaam.
|
- Posted by: HR MANAGER
- Company: SEKRETARIATI YA AJIRA
- State: Tanzania
- Location: Dar es Salaam, Dar es Salaam, Tanzania
- Job type: Full-Time
- Salary:
- Job category: Others
- Tags: nafasi za kazi utumishi wa umma
- Job expires in: 11 days
Subscribe to:
Posts (Atom)
No comments:
Post a Comment