Tuesday, July 30, 2019
Friday, July 26, 2019
Thursday, July 25, 2019
Saturday, July 20, 2019
Thursday, July 18, 2019
Tuesday, July 16, 2019
Waziri Bashungwa Azindua ligi ya Mpira wa Miguu Karagwe
Na Amani Mbwaga, Karagwe
Waziri wa Viwanda na Biashara ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Karagwe Mkoani Kagera Mhe. Innocent Bashungwa Mapema Wikendi iliyopita amezindua rasmi Mashindano ya ligi ya mpira wa miguu ambayo hufanyika kila mwaka Jimboni kwake na ni maarufu kwa BASHUNGWA KARAGWE CUP.
Akiongea na Wananchi katika kijiji cha Nyakagoyagoye Wilayani Karagwe wakati wa uzinduzi wa ligi hiyo Waziri Bashungwa amesema wananchi wanapoendelea kuchapa kazi serikali nayo inaendelea kuleta huduma za jamii katika maeneo yote mijini na vijijini.
“Wana Karagwe Chapeni Kazi lakini sisi kwenye huduma za jamii suala la maji mlikuwa mkisikia nikiwa bungeni nazungumzia mradi wa maji mpaka koo linakauka, lakini huo mradi ndugu zangu ni mkubwa sana na uko katika hatua nzuri na hivi ninavyozungumza Waziri wa maji alikuwa hapa Karagwe jana kuhakikisha mradi huo unatekelezwa ipasavyo” alisema
Wakati huo huo Waziri Bashungwa amemshukuru Rais Magufuli kwa kupeleka miradi mingi na mikubwa Wilayani Karagwe ambapo hivi karibuni tu Zaidi ya Bilioni 70 zitapelekwa tena katika Wilaya hiyo kwa ajili ya kuchochea miradi mingine ya maendeleo.
Mkuu wa Wilaya Karagwe Mhe. Godfrey Mhehuka amempongeza waziri Bashungwa kwa kuchapa kazi na hatimae wana karagwe wanafurahia maendeleo yanayopatikana ktokana na juhudi zake.
“Niemona niseme pongezi zangu kwako, umati huu ni mkubwa sana na unaona ni kwa sababu wewe umeamua kufanya kitu.
Aidha. Mhe Mheuka ameendelea kusema rais hakukosea kumchagua kuwa waziri wa viwanda na biashara hivyo amemuomba akachape kazi na wao wako nyuma yake kuhakikisha anawatumikia vyema wananchi wa Karagwe na Taifa kwa ujumla.
“Niseme neno moja
tu, Mungu ametuona, nataka niwape siri hakika mungu amewaona DC Mwenye Waziri
Mkoa wa Kagera niko peke yangu ahsanteni sana”alisema Mhe. Mheuka
Kwa mujibu wa
mratibu wa mashindano ya BASHUNGWA KARAGWE CUP Bwana Majaliwa Said amesema Mashindano hayo yameanza tarehe
13 Julai 2019 yakihusisha timu kutoka kata zote 23 za Halmashauri ya Wilaya Karagwe.
HABARI PICHA
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Innocent Bashungwa (Kushoto) akifurahia jambo na Mkuu wa Wilaya Karagwe Mhe.Godgrey Mhehuka katikati ni Katibu wa CCM wilaya ya Karagwe Bi. Mary Kananda |
Pichani, Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa wa (tatu kushoto) akiwa pamoja na moja ya Timu iliyozindua mchezo wa kwanza wa ligi ya Bashungwa Karagwe Cup |
Waamuzi na Ma Kapteni wa Timu |
Baadhi ya Wananchi waliofika Kuhudhuria Uzinduzi wa Bashungwa Karagwe Cup Wkifuatilia kwa Makini Mchezo unaoendelea |
Mratibu wa Mashindano ya BASHUNGWA KARAGWE CUP Bwana Majaliwa Said akitoa Taarifa ya Mashindano kwa Waziri wa Viwanda na Biashara (Mbunge Karagwe) |
Thursday, July 11, 2019
Wednesday, July 10, 2019
Monday, July 8, 2019
Sunday, July 7, 2019
Friday, July 5, 2019
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Bashungwa Afanya ziara katika Viwanda vya nguo na Kutatua kero zao
Na
Amani Mbwaga, Dar es salaam
Waziri wa viwanda
na Biashara nchini Tanzania Mhe. Innocent Bashungwa Mapema leo hii amefanya
ziara katika viwanda vya nguo kikiwemo cha NIDA na kile cha NAMERA vya jijini Dar es salaam.
Akiongea mara baada
ya kutembelea viwanda hivyo Mhe. Bashungwa amesema lengo la ziara hiyo ni
kupita katika viwanda vyote vya nguo nchini kujua changamoto zao na kisha
serikali kuzifanyia kazi na hatimae kuwa na uzalishaji endelevu wa zao la pamba na kuwanufaisha wakulima.
“Mimi nimekuja hapa
kwa ziara mahususi, Wakulima wetu wa pamba wamehamasika sana kulima pamba,
Msimu huu wa mwaka 2019 tunategemea kuvuna
zaidi ya Tani Laki 4 za pamba kutoka tani Laki 220,000 za mwaka jana kwa
hiyo tuna pamba za kutosha” alisema Mhe.
Bashungwa.
Aidha amesisitiza
kwamba wakulima kwa upande wao wametimiza wajibu wao hivyo ni jukumu la
Serikali kupitia wizara ya viwanda na biashara kuwatafutia masoko yenye tija.
“Kwa muda mrefu
soko la pamba limekuwa likitegemea mlango mmoja tu, wakati wa enzi za Baba wa
Taifa Mwl. Julius Nyerere kulikuwa na viwanda vingi vya nguo na vilikuwa
vinafanya kazi ipasavyo na kama vyote vingekuwepo basi kusingekuwepo na
changamoto ya masoko katika zao la pamba hivyo ni wakati sasa wa viwanda vilivyopo na
vitakavyojengwa kuhakikisha vinafanya kazi ipasavyo na Kuongeza Uzalishaji mara mbili zaidi ili kuendana na kasi ya sasa
ya Tanzania ya Viwanda".
Nchi ikifanikiwa kuchakata
kila zao na kuliongezea thamani basi itakua ni chachu ya ongezeko la
ajira hapa nchini na hatimae kukuza uchumi wa
taifa na wananchi kwa ujumla.
Dira kuu ya Wizara ya Viwanda na Biashara
ni "Kuwa na msingi shindani wa viwanda, mazingira bora ya uwekezaji
na ukuaji wa biashara unaowezesha kukua kwa uchumi shirikishi na
endelevu."
Waziri Bashungwa
ataendelea na ziara hiyo nchi nzima baada ya Kuanza na Mkoa wa Kilimanjaro hapo
jana na leo hapa Jijini Dar es salaam.
MATUKIO KATIKA PICHA
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa akiangalia Bidhaa zinazotengenezwa na Kiwanda cha Nguo NIDA Wakati wa ziara yake.
|
Pamba ikiwa katika Hatua za awali za uchakataji |
Waziri wa Viwanda na Biashara (Katikati) akipokea maelezo ya namna Pamba inavyoanza kuchakatwa katika hatua za awali |
Shughuli za Uzalishaji Kiwandani zikiendelea |
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Innocent Bashungwa (Kulia) akimsikiliza kwa Makini Mkurugenzi Mkuu wa Kiwanda cha Nguo NIDA na NAMERA (Picha zote na Amani Mbwaga) |
Subscribe to:
Posts (Atom)