Monday, May 28, 2018

Mapokezi ya Mwenge wa Uhuru 2018 yafana sana Halmashauri ya Mji Mafinga

 ·        Miradi ya Maendeleo yenye Thamani ya Zaidi ya Bilioni 1.7 Imezinduliwa, Kukaguliwa na Kuwekewa jiwe la Msingi.
Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William akipokea Mwenge wa Uhuru tayari kwa Kuukimbiza katika Halmashauri ya Mji Mafinga

Na Amani Mbwaga, Mafinga Iringa
 Jumla ya Miradi 08 imepitiwa na Mwenge wa Uhuru ikiwa ni utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Halmashauri ya Mji Mafinga, ikishirikiana na Wananchi pamoja na wadau mbalimbali wa Maendeleo.

Thamani ya miradi yote ni zaidi Tsh. Bilioni, 1.7, Mchanganuo wa gharama za miradi 08 ni kama ifuatavyo- ; Serikali Kuu imechangia Tsh Milioni 700.4, Halmashauri ya Mji Mafinga Tsh Milioni 47.2 Wahisani Tsh Milioni 38 na Wananchi wamechangia nguvu kazi na Fedha taslimu zenye thamani ya Tsh Milioni 954.5, miradi hii yote ipo katika sekta ya Elimu Afya, Maji,Kilimo, Mazingira na Ujenzi.

Katika Miradi hiyo Mwenge umefungua mradi wa ujenzi wa Daharia/Hosteli ya Wasichana Shule ya Sekondari Mnyigumba, umezindua mradi wa kusaidia kuhifadhi na kutunza kumazingira wa WF Renuable Resources Limited uliopo katika Kijiji cha Rungemba, Umezindua ujenzi wa Tanki la Maji mtaa wa Tanganyika, Umezindua Klabu ya Wapinga Rushwa Shule ya Sekondari JJ Mungai, Umezindua Mnara wa Kumbukumbu ya Kuuenzi Mwenge wa Uhuru mwaka 2018, Umezindua Zahanati ya Nipende katika mtaa wa Amani.   

Aidha Umeweka Jiwe la Msingi katika Ujenzi wa vyumba 02 vya Madarasa Shule ya Sekondari Ihongole, Pia umekagua mradi wa kilimo    cha zao la Parachichi mtaa wa Ndolezi na Mwisho kukagua  mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Changarawe Matanana-Kisada yenye Urefu wa Kilometa 15 Katika mradi huu Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho ametoa maelekezo ya kurudia kupima kwa ufanisi kama mkandarasi ametekeleza viwango vilivyowekwa katika mkataba ikiwa ni kwa lengo la kusimamia ubora wa barabara.

Akitoa Ujumbe wa Mwenge  Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho aliwahamsisha Wananchi Kuwekeza Katika Elimu chini ya Ujumbe Mkuu wa Mbio za Mwenge 2018 “ELimu ni Ufunguo wa Maisha Wekeza Sasa kwa Maendeleo ya Taifa letu”

Pia aliendelea Kuhamasisha Kuhusu Mapambano dhidi ya Rushwa, Mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI, Mapambano dhidi ya Madawa ya Kulevya na Mapambano dhidi ya Malaria.

Aidha alisistiza kwa viongozi wa serikali kufuatilia kwa makini miradi inayojengwa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi ijengwe kwa ubora unaotakiwa ili thamani ya pesa inayotumika ionekane “Watumishi wote mnatakiwa kutimiza  wajibu wenu katika kulitumikia Taifa letu”alisema Kabeho    

Kwa Upande Wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe Jamhuri William Kupitia Risala ya Utii wa Mwenge wa Uhuru 2018 Halmashauri ya Wilaya Mufindi Kwa Mheshimiwa Rais Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Kuhusu Utekekelezwaji wa Maagizo ya Serikali katika Sekta Mbalimbali, Ikiwemo Uanzishwaji wa Viwanda, Usimamizi wa Mbolea ya Ruzuku, Kuokoa Mifumo ya Kiikoljia ya Bonde la Mto Ruaha Mkuu na Waalimu Kutojihusisha na Michango ya Wazazi Mashuleni .

Mwenge wa Uhuru Uliwashwa Rasmi na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Tarehe 02 Aprili 2018 Katika Mkoa wa Geita na Unatarajiwa kumaliza Mbio zake Katika Siku ya Kumbukumbu ya Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Wiki ya Vijana Kitaifa tarehe 14 Oktoba 2018 Mkoani Tanga.

                              HABARI KATIKA PICHA

Mkuu wa Wilaya Iringa Mhe Richard Kasesela aliyevaa trakisuti akimkabidhi Mwenge wa Uhuru 2018 Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William tayari kwa kuukimbiza katika Halmashauri ya Mji Mafinga
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho ajisalimiana na Mhe Mkuu wa Wilaya Mufindi Mhe Jamhuri David William
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Saada Mwaruka akisalimiana na Mmoja wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa 2018 wakati wa Makabidhiano.


Mmoja wa wazee wa zamani waliowahi Kukimbiza Mwenge wa Uhuru miaka 50 iliyopita akiwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Kabeho wakati wa Makabidhiano ya Mwenge baina ya Manispaa Iringa na Halmshauri ya Mji wa Mafinga katika viwanja vya Shule ya Sekondari Mnyigumba

Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya Mji Mafinga akisoma Taarifa ya Ujenzi wa Hostel ya Wasichana katika Shule ya Sekondari Mnyigumba
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Kabeho akikagua Ujenzi wa Hosteli na Vitanda vyake


Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga Bi Saada Mwaruka akitoa maelezo ya Mradi wa Ujenzi wa Hosteli ya Wasichana Kwa kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Francis Kabeho katika Shule ya Sekondari Mnyigumba

Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa akiweka jiwe la Uzinduzi wa Hosteli ya Wasichana Shule ya Sekondari Mnyigumba


Kiongozi wa Mbio za Mwenge ndugu Kabeho ajitoa Ujumbe wa Mbio za Mwenge 2018 mara baada ya Kuzindua Hosteli ya Shule ya Sekondari Mnyigumba







Kiongozi waMbio za Mwenge Kitaifa akikata Utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa kiwanda cha kutengeneza Mkaa kwa kutumia Mabaki ya vumbi za Mbao (Sawdust)

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji Mafinga  Bi Saada Mwaruka akisalimiana na Msoma Taarifa ya Kiwanda cha Mkaa wakati Mwenge wa Uhuru ukizindua 

Kiongozi wa Mbio za Mwenge akikagua Mradi wa Kiwanda cha Mkaa na Hatua zake jinsi kinavyozalisha Mkaa huo unaolinda kuhifadhi na Kutunza Mazingira



Huu ndio Mkaa unaozalishwa na Kiwanda hiki baada ya kupitia hatu mbalimbali za Uzalishaji




Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2018 akizindua Mradi wa Ujenzi wa Tanki la Maji lenye ujazo wa lita 500,000 liliopo katika mtaa wa Tanganyika, Mjini Mafinga


Ukaguzi wa Tanki Ukifanyika





Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ndugu Charles Kabeho akimtwisha ndoo ya Maji Mama aliyechota Maji kutoka kwenye bomba linaotoa maji kwenye Tanki mpya liliozinduliwa na Mwenge 2018




Baadhi ya Wananchi waliohudhuria Uzinduzi wa Tanki la Maji Uliofanywa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2018


Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa ndugu Charles Kabeho akizindua akiweka jiwe la msingi la Ukaguzi wa Mradi wa Kilimo cha Parachichi Unaomilikiwa na Mr& Mrs Mkisi mtaa wa Ndolezi




Kiongozi wa Mbio za Mwenge 2018 akiweka Jiwe la Msingi Mradi wa Ujenzi wa Vyumba 02 vya  Madarasa  Shule ya Sekondari Ihongole






Kiongozi wa Mbio za  Mwenge akioonge na Wananchi na Wanfunzi wa Shule ya Sekondari JJ Mungai Wakati wa Uzinduzi wa Klabu ya Wapinga Rushwa  


Akiwauliza maswali ya Ufahamu  wanafunzi wa JJ Mungai na Wanachama wa Kklabu ya Wapinga Rushwa juu  ya ulewa wa Kupinga Rushwa





Picha zote na Amani Mbwaga

Wasiliana nasi;
Mob:+255 656 632 566
Email:Prof.mbwaga@gmail.com
Twitter:@amanimbwaga

No comments:

Post a Comment