KWA
UFUPI
Manchester, England.
Mashabiki wa Manchester United wamefanikiwa kumpata Marouane Fellaini na kiungo
huyo wa Ubelgiji ameonyesha kiwango cha juu kwa kutoa pasi nzuri na
kunyang’anya mpira wakielekea katika mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu wao
City.
Viungo Yaya Toure wa
City ataonyeshana ufundi na Marouane Fellaini wa United kesho kwenye uwanja wa
Etihad.
Manchester, England.
Mashabiki wa Manchester United wamefanikiwa kumpata Marouane Fellaini na kiungo
huyo wa Ubelgiji ameonyesha kiwango cha juu kwa kutoa pasi nzuri na
kunyang’anya mpira wakielekea katika mchezo wa kesho dhidi ya mahasimu wao
City.
Mabingwa wa msimu
uliopita na washindi wa pili wanakutana kwenye Uwanja wa Etihad, wakiwa na
rekodi ya ushindi waliopata katikati ya wiki katika Ligi ya Mabingwa.
Mshambuliaji wa Wayne
Rooney amerudi kwenye kiwango chake na Jumanne alifunga mabao mawili wakishinda
4-2 dhidi ya Bayer Leverkusen, lakini uwepo wa Fellaini katika nafasi ya kiungo
aliyeonyesha uwezo mzuri wa kumiliki mpira umeongeza ladha ya mchezo wa kesho.
Wapinzani wao City
baada ya kupoteza dira katika ligi katikati ya wiki walishinda 3-0 dhidi ya
Viktoria Plzen katika Ligi ya Mabingwa, ushindi unaomfanya kocha Manuel
Pellegrini kuamini kwamba umerudisha kujiamini kwa wachezaji wake.
“Tuna mechi ngumu
Jumapili na ushindi wa ugenini katika Ligi ya Mabingwa tena wa mabao matatu,
nafikiri umerudisha kujiamini kwa wachezaji.”
Kiungo wa City,Yaya
Toure, ambaye ni kama Fellaini ameonyesha kiwango cha juu, cha kutengeneza
magoli na uwezo mkubwa wa kusoma mchezo, pia alifunga bao moja dhidi ya Plzen
na kesho inategemewa itakuwa ni vita kubwa kati ya viungo hao wawili.
Hii ni mechi ya kwanza ya miamba ya Manchester
kukutana wakati timu zote zikiwa na makocha wapya ambao wanajua kuwa City
imekusanya pointi 10 kutoka kwa United katika michezo saba ya ligi waliokutana
katika misimu mitatu iliyopita.