Wednesday, August 21, 2013

CHADEMA YATAKA MAJI SAFI NA SALAMA YATAMBULIKE KIKATIBA KAMA HAKI YA KILA RAIA,

FREEMAN MBOWE NA TINDU LISU WAWASISITIZA WANANCHI KUTOA MAONI JUU YA RASIMU YA KATIBA MPYA  LEO KTK MJI WA NAMANYERE.

Viongozi wakuu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Watoa elimu kwa wananchi juu ya Rasimu ya katiba mpya hayoyamesemwa  na Mwenyekiti wa chama cha  CHADEMA TAIIFA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI, FREEMAN  MBOWE Akiwa na  Mwenzake  Mbunge wa Singida  Bwana TINDU LISSU, leo Tarehe 21-08-2013 ktk mji wa Namanyere.

Mh.MBOWE, Amewasisitiza wananchi kuendelea kutuma maoni yao juuu ya Rasimu ya katiba mpya kwa njia ya mtandao na simu za mkonono, lengo ni kutaka kuona wilaya gani inamahitaji ya msingi zaidi kikatiba kwa sababu kila wilaya inatofautiana kijiografia na mahitaji yao.
Mh. Mbowe alitoa mawasiliano haya ili kutuma maoni juu ya rsimu ya katiba mpya                                         Email:  chademamaoni@gmail.com,                                                                                                    Namba za simu  0789248224. Na pia unapotuma  maoni hayo lazima uandike majina yako matatu, kata unayoishi na  Wilaya yake.                                                                                                     

"Chadema Tulipigana Mpaka Mchakato wa Katiba Mpya ukaanza Hivyo Naomba Mtuamini kutupa Nafasi"  Haya yalisemwa  na Mh. Mbowe alipokuwa akihutubia mamia ya watu wa mji wa namanyere.  Pia ammeongelea  Matatizo Makubwa yanayoikumba Nchi hii ambayo ni MAJI. " Miaka 50 ya Uhuru Hadi sasa bado maeneo mengi ya nchi yetu yanshida ya maji Hivyo Tunataka katiba mpya itambue suala la maji iwe ni haki ya kikatiba  kwa kila Raia" hivyo serikali haina budi kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji safi na salama.

Naye Mbunge wa SINGIDA  Mh TINDU  LISSU Alianza hotuba yake kwa kutoa historia fupi ya katiba mpya toka enzi za ukoloni na akasema hakuna mtu wakati ule aliyeulizwa kuwa anataka katiba iweje?
Katiba ni utaratibu wa namana ya kujitawala na lengo la Rasimu ya katiba hii kutaka wananchi wapitie na kuona kama wanaweza kuongeza  mambo mengine ya msingi au kupunguza na baadae kuja kupigia kura ya NDIO au HAPANA.

Pia amezungumzia jinsi rasimu ilivyoongelea juu ya kupunguza madaraka ya Rais, na hapa tume ya Warioba imependekea mambo makuu 3.
1.Rais lazima ashauriwe
2.Rais akishauriwa lazima afuate ushauri nakama haufuati lazima atoe maelezo.
3.Kila mtu anayeteuliwa na Rais Lazima athibitishwe na Bunge.
Mambo mengine ni wanachi kuwa na nguvu ya kumuondoa Mbunge aliyeshindwa kutimiza ahadi zake.

Mh. LISSU  alihitimisha kwa kuwashukuru wananchi wa mji wa Namanyere kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo na  kuwaomba wananchi watoe maoni yao juu ya rasimu ya katiba mpya  ili tuweze kupata katiba iliyo bora zaidi na yenye manufaa kwa wananchi wote.

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa bwana Freeman Mbowe kulia na kushoto ni Mh. Tindu Lissu wakiwasili Mjini Namanyere

Freeman Mbowe akiwahutuba Wananchi wa Namanyere.
Mh Tindu Lissu akiwahutubia Wananchi.







Wananchi wa Mji wa Namanyere Wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA.











Aman E Mbwaga mmiliki wa blog hii akipata picha ya pamoja  na HELCOPTA iliyowaleta viongozi wa CHADEMA.
Rubani wa ndege akihaiki usalama wa viongozi wa chadema wakati wakiingia kwenye ndege tayari kwa safari ya kuelekea  mjini sumbawanga kwa ajili ya mkutano mwingine .

Ndege ikijiandaa kuondoka.

Ahsante kwa kusma habari hizi na karibu tena Nitaendelea kukuhabarisha Matukio mbalimbali yanayoendelea kutokea hapa nchini.
Kwa maoni, ushauri au zaidi tuma ktk Email yangu amanmbwaga@gmail.com, Facebook Aman Mbwaga, Tweeter @amanmbwaga, skype,  aman mbwaga.
  "MUNGU AKUBARIKI"







No comments:

Post a Comment