Saturday, August 31, 2013
Wednesday, August 21, 2013
CHADEMA YATAKA MAJI SAFI NA SALAMA YATAMBULIKE KIKATIBA KAMA HAKI YA KILA RAIA,
FREEMAN MBOWE NA TINDU LISU WAWASISITIZA WANANCHI KUTOA MAONI JUU YA RASIMU YA KATIBA MPYA LEO KTK MJI WA NAMANYERE.
Viongozi wakuu wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Watoa elimu kwa wananchi juu ya Rasimu ya katiba mpya hayoyamesemwa na Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA TAIIFA NA KIONGOZI WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI, FREEMAN MBOWE Akiwa na Mwenzake Mbunge wa Singida Bwana TINDU LISSU, leo Tarehe 21-08-2013 ktk mji wa Namanyere.
Mh.MBOWE, Amewasisitiza wananchi kuendelea kutuma maoni yao juuu ya Rasimu ya katiba mpya kwa njia ya mtandao na simu za mkonono, lengo ni kutaka kuona wilaya gani inamahitaji ya msingi zaidi kikatiba kwa sababu kila wilaya inatofautiana kijiografia na mahitaji yao.
Mh. Mbowe alitoa mawasiliano haya ili kutuma maoni juu ya rsimu ya katiba mpya Email: chademamaoni@gmail.com, Namba za simu 0789248224. Na pia unapotuma maoni hayo lazima uandike majina yako matatu, kata unayoishi na Wilaya yake.
"Chadema Tulipigana Mpaka Mchakato wa Katiba Mpya ukaanza Hivyo Naomba Mtuamini kutupa Nafasi" Haya yalisemwa na Mh. Mbowe alipokuwa akihutubia mamia ya watu wa mji wa namanyere. Pia ammeongelea Matatizo Makubwa yanayoikumba Nchi hii ambayo ni MAJI. " Miaka 50 ya Uhuru Hadi sasa bado maeneo mengi ya nchi yetu yanshida ya maji Hivyo Tunataka katiba mpya itambue suala la maji iwe ni haki ya kikatiba kwa kila Raia" hivyo serikali haina budi kuhakikisha kwamba wananchi wanapata maji safi na salama.
Naye Mbunge wa SINGIDA Mh TINDU LISSU Alianza hotuba yake kwa kutoa historia fupi ya katiba mpya toka enzi za ukoloni na akasema hakuna mtu wakati ule aliyeulizwa kuwa anataka katiba iweje?
Katiba ni utaratibu wa namana ya kujitawala na lengo la Rasimu ya katiba hii kutaka wananchi wapitie na kuona kama wanaweza kuongeza mambo mengine ya msingi au kupunguza na baadae kuja kupigia kura ya NDIO au HAPANA.
Pia amezungumzia jinsi rasimu ilivyoongelea juu ya kupunguza madaraka ya Rais, na hapa tume ya Warioba imependekea mambo makuu 3.
1.Rais lazima ashauriwe
2.Rais akishauriwa lazima afuate ushauri nakama haufuati lazima atoe maelezo.
3.Kila mtu anayeteuliwa na Rais Lazima athibitishwe na Bunge.
Mambo mengine ni wanachi kuwa na nguvu ya kumuondoa Mbunge aliyeshindwa kutimiza ahadi zake.
Mh. LISSU alihitimisha kwa kuwashukuru wananchi wa mji wa Namanyere kwa kujitokeza kwa wingi kwenye mkutano huo na kuwaomba wananchi watoe maoni yao juu ya rasimu ya katiba mpya ili tuweze kupata katiba iliyo bora zaidi na yenye manufaa kwa wananchi wote.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa bwana Freeman Mbowe kulia na kushoto ni Mh. Tindu Lissu wakiwasili Mjini Namanyere |
Freeman Mbowe akiwahutuba Wananchi wa Namanyere. |
Mh Tindu Lissu akiwahutubia Wananchi. |
Wananchi wa Mji wa Namanyere Wakisikiliza hotuba ya Mwenyekiti wa CHADEMA. |
Aman E Mbwaga mmiliki wa blog hii akipata picha ya pamoja na HELCOPTA iliyowaleta viongozi wa CHADEMA. |
Rubani wa ndege akihaiki usalama wa viongozi wa chadema wakati wakiingia kwenye ndege tayari kwa safari ya kuelekea mjini sumbawanga kwa ajili ya mkutano mwingine . |
Tuesday, August 20, 2013
MTAWA WA KANISA KATORIKI AVAMIWA NA KUJERUHIWA HUKO ZANZIBAR..... Tuesday, August 20, 2013 | 9:46 AM
Tukio hilo lilitokea juzi saa 11 jioni, jirani na maeneo ya Kanisa la Kigango cha Mtakatifu Thesia Beit –el-rus, katika nyumba wanazoishi watawa wa kanisa hilo.
Akizungumza na MTANZANIA jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini na Magharibi, Mkadam Khamis Mkadam, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mtu huyo aliyepigwa ni mwanamke ambaye ni mtumishi wa Kanisa Katoliki la Bububu, Zanzibar.
Kamanda Mkadam, alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni ugomvi uliosababishwa na tuhuma za mbwa wa mtawa huyo kuwa amekula kuku wa kijana huyo, ambapo baada ya majibizano kijana huyo alipata jazba, hali iliyosababisha kumpiga ngumi mtawa huyo.
Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kutokea tukio hilo, mtawa huyo alikwenda kufungua jalada la malalamiko katika Kituo kidogo cha Polisi cha Beit-el-rus, kuhusu kupigwa kwake na kijana huyo.
“Tupo tunaendelea na uchunguzi juu ya tukio hili, kwani ni ugomvi wa mitaani unaweza kuleta athari kubwa zaidi, lazima tufanye kazi hii kwa umakini zaidi,” alisema Kamanda Mkadam.
Hata hivyo alisema kuwa Jeshi la Polisi linamshikilia kijana huyo kwa ajili ya mahojiano zaidi, ili kujua sababu za kushambuliwa kwa mtawa huyo ambapo mpaka sasa yupo mikononi mwa polisi.
Alisema baada ya kesi hiyo kufikishwa polisi, wazazi wa kijana huyo walifanya juhudi za kuzungumza na mtawa Irene ili kuweza kufikia maridhiano na kijana huyo na pindi wakishindwa kuelewana, shauri lao litafikishwa mahakamani.
Hata hivyo kutokana na makubaliano hayo, mtawa huyo alikubali kumsamehe kijana huyo, huku polisi ikisema kutokana na sababu za kisheria na usalama, kijana huyo hataachiwa na jalada la kesi limepelekwa katika Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Zanzibar, ili atoe ushauri kuhusu sakata hilo.
source Gumzo ajiji.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/mtawa-wa-kanisa-katoriki-avamiwa-na.html#ixzz2cUdlFY1P
Monday, August 5, 2013
ROBERT MUGABE NDANI YA IKULU YA ZIMBABWE KWA MARA YA SABA....
Monday, August 5, 2013 | 10:32 AM
Baada ya kutangazwa kuwa mshindi wa kinyan’ganyiro cha Urais wa Zimbabwe, Rais Robert Mugabe (89), amefikisha mihula saba ndani ya Ikulu ya nchi hiyo.
Mugabe juzi alishinda tena kiti cha urais. Matokeo rasmi yalionyesha kuwa aliibuka na ushindi wa asilimia 61 wa kura dhidi ya mpinzani wake, aliyekuwa Waziri Mkuu, Morgan Tsvangirai ambaye alipata asilimia 34.
Chama cha Zanu-PF kinachoongozwa na Mugabe na kile cha MDC cha Tsvangirai, viliunda Serikali ya Muungano mwaka 2008.
Juzi, Tume ya Uchaguzi Zimbabwe (ZEC), ilimtangaza Mugabe kuwa mshindi katika uchaguzi wa Rais uliofanyika Jumatano iliyopita.
Zanu-PF pia kilipata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa wabunge baada ya kujinyakulia viti 137 kati ya 210.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa hali inaweza kuwa tete hasa baada ya matokeo hayo ambayo yalipingwa na Tsvangirai na chama chake cha MDC.
Tsvangirai alisema Chama cha MDC kitaisusia Serikali ya Mugabe na kupinga matokeo ya uchaguzi mahakamani. Wasimamizi wa uchaguzi kutoka Umoja wa Afrika wamesema uchaguzi huo ulikuwa huru na wa haki.
Aidha, Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC), ilimtaka Tsvangirai akubali matokeo ya uchaguzi.
Wasiwasi
Malalamiko yanayotolewa sasa na wapinzani kuhusu uchaguzi huo yanazidisha uwezekano wa kuibuka machafuko kama yaliyotokea 2008.
Mwaka huo, Tsvangirai aliongoza katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa Rais na Zanu-PF kilipinga ushindi huo. Ghasia na machafuko vilitokea na kusababisha kuuawa kwa mamia ya wafuasi wa Tsvangirai.
Umwagaji damu uliotokana na uchaguzi huo ulimfanya Tsvangirai ajitoe kushiriki katika duru ya pili ya uchaguzi na hivyo kutoa mwanya kwa Mugabe kutangazwa kuwa mshindi wa duru hiyo kirahisi.
Umwagaji damu uliotokana na uchaguzi huo ulimfanya Tsvangirai ajitoe kushiriki katika duru ya pili ya uchaguzi na hivyo kutoa mwanya kwa Mugabe kutangazwa kuwa mshindi wa duru hiyo kirahisi.
Hata hivyo, shinikizo la kimataifa lililofuata, lilimlazimu Mugabe kuunda Serikali ya umoja wa kitaifa kwa kuishirikisha MDC.
Tayari wananchi wa Zimbabwe katika Mji Mkuu wa Harare wanaamini kwamba wanapaswa kuheshimu matokeo ya uchaguzi na kujiepusha na kuibuka kwa machafuko.
SOURCE: Gumzo la jiji
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/robert-mugabe-ndani-ya-ikulu-ya.html#ixzz2b5c0mOjU
Supporters of Zimbabwe opposition MDC allege attacks
Members of Zimbabwe's opposition MDC party say they have been attacked by followers of President Robert Mugabe.
The allegations come a day after official results from Wednesday's poll gave Mr Mugabe a seventh term in office and his Zanu-PF party three-quarters of the seats in parliament.
Eleven people in Harare and 20 from Mashonaland Central province say they were attacked by known Zanu-PF supporters after the results were announced,
The MDC has called the poll fraudulent.
Its leader, Prime Minister Morgan Tsvangirai, 61, has vowed to take legal action to contest the results.
He has also said his Movement for Democratic Change (MDC) would no longer work with Mr Mugabe's Zanu-PF party and would boycott government institutions.
The two parties have been in a coalition since 2009, after the last election sparked widespread violence.
The 11 people who claimed they were attacked in a township in the capital Harare sought refuge at the MDC party headquarters on Sunday, the BBC's Brian Hungwe reports from Harare.
Both they and those from Mashonaland Central province, north of the capital, allege that they were attacked by Zanu-PF supporters who went door-to-door ordering MDC supporters and their families to pack their bags and leave.
An MDC spokesman, Douglas Mwonzora, said the attacks were well planned. But a spokesman for Zanu PF, Psychology Maziwisa, denied his party was attacking opponents.
The MDC warns that it may not be able to control its angry supporters if the reports of attacks continue, our correspondent reports.
The party has appealed to the Southern African grouping, Sadc, to intervene to prevent the situation getting out of control, he adds.
Some in the MDC have called for a campaign of civil disobedience to isolate Zanu-PF.
'Profound congratulations'
Mr Mugabe, 89, won 61% of the vote in the presidential poll, against Prime Minister Morgan Tsvangirai's 34%.
Results from the parliamentary election also handed the MDC a defeat. It won just 49 seats compared with Zanu-PF's 158.
Continue reading the main story
Zimbabwe's election
- Robert Mugabe wins landslide in presidential election with 61% of vote
- Mr Mugabe's Zanu-PF wins three-quarters of seats in parliamentary election
- Morgan Tsvangirai fails to get elected president for a third time, calls election a "sham"
- Voting passes off peacefully, but local observers claim "irregularities" resulted in one million being unable to vote
- African Union and South Africa urge all sides to accept the results
The US and UK have expressed concern at the poll results amid the opposition's claims of electoral fraud.
But the Jacob Zuma, president of regional power South Africa, extended his "profound congratulations" to Mr Mugabe and urged all sides to accept the outcome.
On Sunday, MDC party treasurer Roy Bennett told the BBC's Newshour programme that there was a "seething anger simmering across the length and breadth of Zimbabwe... for the fact that they have had their rights stolen."
He condemned Zanu-PF as "a bunch of kleptocratic geriatrics who should have retired long ago".
Asked about possible mistakes that the MDC had made, and about the quality of Mr Tsvangirai's leadership, Mr Bennett hinted that "nobody's indispensable" and that current events "will deal with those who have been exposed as not having the people's interest at heart".
Legal timetable
Monitoring groups disagreed over the conduct of the election.
The most critical account came from the largest group of monitors, the Zimbabwe Election Support Network (ZESN), which had 7,000 workers observing the vote.
The organisation said problems with voter registration had left up to one million people unable to cast their ballots, mostly in urban areas regarded as MDC strongholds.
On Saturday, one of the nine members of the election commission resigned over the way the election was conducted.
Commissioner Mkhululi Nyathi said in his resignation letter: "While throughout the whole process I retained some measure of hope that the integrity of the whole process could be salvaged along the way, this was not to be."
However, the African Union, which had 70 observers, said its initial report suggested the election was "free and credible".
The AU's mission chief Olusegun Obasanjo said there had been "incidents that could have been avoided" and asked Zimbabwe's election authorities to investigate claims that voters had been turned away from polling stations.
The southern African regional bloc, Sadc, with 560 observers, broadly endorsed the election as "free and peaceful", but said it would reserve judgement on the fairness of the process.
Mr Mugabe has had a troubled relationship with the West since launching his programme to seize white-owned land in 2000 - a move widely seen as destroying Zimbabwe's economy.
In contrast, many African leaders still respect him for leading the fight against white minority rule in the 1970s.
Mr Tsvangirai has seven days from the declaration of the results to lodge a legal challenge to the Constitutional Court.
The court then has 14 days to deliver a judgement. If the court upholds the results, Mr Mugabe must be sworn in within 48 hours of the ruling.
If it orders fresh elections, these must be held within 60 days.
Mr Mugabe has governed Zimbabwe since independence from the UK in 1980.
INATISHA!! ASKARI WA KIKE AFARIKI DUNIA KWA KUKANYAGWA NA TAILI KICHWANI... Monday, August 5, 2013 | 9:39 AM
Askari Polisi wa kike mkoani hapa amefariki dunia papo hapo baada ya kukanyagwa na tairi la gari na kupasuka kichwa.
Askari huyo Rehema James (30), alikutwa na umauti juzi wakati akiwa amepanda katika usafiri wa baiskeli maarufu kama daladala eneo la Kambarage mjini Shinyanga.
Watu walioshuhudia tukio hilo waliliambia gazeti hili kuwa, askari huyo alikuwa amepakizwa kwenye baiskeli ndipo gari hilo lilipomgonga na kufariki dunia.
Walisema waliona gari aina ya scania lenye namba za usajili BLQ 546 likimgonga askari huyo na kufariki dunia papo hapo na ubongo wake ukiwa nje huku mwendesha baiskeli akifanikiwa kuruka kutoka kwenye baiskeli hiyo na kukimbia.
Walieleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendesha baiskeli kutaka kulipita gari hilo wakati likikata kona na Rehema alijigonga kwenye tela la gari na kuanguka chini ambapo tairi lilimpitia na kumpasua kichwa.
Utingo wa gari hilo, God Makunga, alisema wakati gari lao likikata kona ghafla alisikia kishindo kikubwa kwenye gari na baada ya kushuka akamkuta mwanamke huyo amekanyangwa na tairi la gari.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Kihenya Kihenya amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Alisema Rehema alikuwa abiria kwenye baiskeli na baadaye akagongwa na gari hilo, na tayari mwili wake umesafirishwa kwenda nyumbani kwao jijini Dar es Salaam kwa mazishi yanayotemewa kufanyika leo.
Alisema chanzo cha ajali hiyo kinachunguzwa na jeshi la polisi linaendelea kumtafuta dereva wa gari hilo kwani alitoroka mara baada ya ajali kutokea na kuacha gari lake eneo la tukio.
Kamanda Kihenya ametoa wito kwa watumiaji wa barabara wakiwamo madereva wa magari na waendesha baiskeli kuwa makini kwa kuzingatia sheria za usalama barabaranisource: gumzo la jiji.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/inatisha-askari-wa-kike-afariki-dunia.html#ixzz2b5N5VLi2
MAJAMBAZI YATEKA KIVUKO NA KUIBA....
Monday, August 5, 2013 | 10:12 AM
Mkuu wa mkoa wa mwanza Evarist Ndikilo
Watu wawili mmoja akiwa na silaha ya kivita wanaosadikiwa kuwa majambazi wamevamia na kuweka chini ya ulinzi ofisi ya mauzo ya tiketi ya kivuko cha Busisi akiwamo ofisa wake na kisha kupora kiasi cha fedha ambacho bado hakijafahamika.
Tukio hilo lilitokea saa 3:15 usiku wa kuamkia jana baada ya watu hao mmoja akiwa na panga na mwingine bunduki aina ya SMG huku akifyatua risasi kadhaa hewani kuwatisha wananchi. Watu hao wanadaiwa kumlazimisha ofisa aliyekuwa anauza tiketi awapatie fedha zote.
Katika tukio hilo ambalo lilidumu kwa takribani dakika 10, mtu mmoja aliyekuwa anakata tiketi alijeruhiwa mguuni baada ya kukaidi amri ya kujisalimisha.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Busisi, Tumani Thomas, alisema hali hiyo ilisabaisha wakazi wa eneo hilo hususani wafanyabiashara walipata hofu kutokana na milio ya risasi.
“Bado kuna utata katika tukio hilo nadhani lengo lao kubwa lilikuwa ni kuvamia feri hizo na kuwapora abiria, kwa bahati zilikuwa ziwani huenda kuna kitu kilichotibua mpango wao huo…majeruhi alikimbizwa Hospiatli teule ya Wilaya ya Sengerema usiku huo na polisi walifika ndani ya muda mfupi,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi, Ernest Mangu, amethibitisha tukio hilo na kusema kwamba alikuwa na taarifa za awali hivyo atatoa ufafanuzi zaidi leo. Tukio hilo limekuja siku mbili toka Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Evarist Ndikilo na Kamanda Mangu kusisitiza kuwa kulikuwa kunaandaliwa mkakati kabambe wa kuimarisha ulinzi na usalama mkoani humo kupitia falsafa ya ulinzi shirikishi.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/08/majambazi-yateka-kivuko-na-kuiba.html#ixzz2b5FwupjN
Thursday, August 1, 2013
WAASI WA M23 MASHARIKI YA KONGO WAPEWA MASAA 48 KUSALIMISHA SILAHA...VINGINEVYO NI BALAA TUPU...!!
Na Mwandishi Maalum, NY, Marekani -- Misheni ya Kutuliza Amani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) imetangaza kwamba kwa mara ya kwanza itaanza kuitumia Brigedi Maalum ( Force Intervention Brigade) katika kudhibiti eneo maalum la usalama (security zone) kuzunguka mji wa Goma ulioko Mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na imewapa saa 48 waasi kusalimisha silaha zao.
Taarifa iliyotolewa na MONUSCO na kusambazwa na Idara ya Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa jana jumanne, inaeleza kwamba watu binafsi katika eneo la Kivu ya Magharibi ambalo linajumisha Goma na Sake na ambao hawahusiki na vyombo vya usalama watapewa saa 48 kuanzia saa kumi jana kwa saa za Goma (Jumanne) kuzisalimisha silaha zao katika Misheni hiyo na kujiunga na mchakato wa DDR/RR unaoratibu upokonyaji, usambaratishaji, urejeshwaji makwao, kuwaunganisha na jamii na kuwapatia makazi.
Baada ya saa kumi jioni ya Alhamisi, Agosti Mosi. Taarifa hiyo inasema. Wale wote ambao watakuwa hawajasalimisha silaha zao watachukuliwa kama tishio kwa usalama wa wananchi na MONUSCO itachukua hatua zote muhimu kuwapokonya silaha hizo ikiwa ni pamoja na kutumia nguvu kama ilivyoainishwa katika Mamlaka na sheria za ushiriki za MONUSCO.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo zaidi ya wananchi milioni moja wanaishi katika eneo dogo la Goma na Sake na kando kando ya barabara ambayo inawaunganisha na kambi ya wakimbizi ya Mugungu ambayo ni makazi ya muda ya watu karibu 70, 000 ambao wameyakimbia makazi yao kutokana na mapigano.
Kwa mujibu wa MONUSCO, tangu kati kati ya mwezi Mei eneo hilo limeshuhudia mapigano ya mara kwa mara kutoka kwa kundi la M23 dhidi ya majeshi ya Serikali ya FARDC ikiwa ni jaribio la wazi la kutaka kusonga mbele kuelekea Goma na Sake.
“Katika mashambulizi hayo, likiwamo la hivi karibuni la Julai 14, M23 walitumia kiholela silaha zao za moto zikiwamo silaha nzito ambazo zimesababisha wananchi kujeruhiwa” .
Taarifa hiyo imeongeza kwamba kundi hilo la M23 katika mashambulizi hayo limelenga pia Vituo vya Umoja wa Mataifa.
Aidha taarifa hiyo inabainisha kwamba eneo hilo maalum la usalama ( security zone) litasaidia kudhibiti tishio la moja kwa moja mbali na eneo la nje ya Goma na pengine eneo hilo linaweza kupanuliwa na kurudiwa sehemu nyingine kutakako hitajika.
Tamko hilo la kutoa saa 48 kwa waasi kusalimisha silaha zao linafuatia kuwasili katika eneo la Goma kwa Kamanda Mkuu wa MONUSCO, Luteni Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz, ambaye alitangaza kwamba Misheni ya MONUSCO itaunga mkono jeshi la Serikali (FARDC) katika kuanzisha eneo la usalama kuzunguma eneo la Goma na vitongoji vyake.
Taarifa hiyo inamkariri Kamanda Mkuu wa MONUSCO akiyapongeza majeshi ya serikali kwa kazi nzuri iliyofanya wiki iliyopita ya kuwadhibiti M23. Ingawa anasema eneo la Goma na Sake bado limo katika mazingira magumu sana na kwamba ni wajibu wa wahusika wote kuhakikisha wahalifu wote hawaendelei kuhatarisha raia wa eneo hilo.
Kwa mwaka uliopitia , kundi la M23 pamoja na makundi mengine yenye silaha yamekuwa yakipambana mara kwa mara na majeshi ya serikali katika Mashariki ya Kongo, huku makundi hayo yenye silaha mwezi Novemba mwaka jana yakiikalia Goma kwa muda.
Aidha mapingano ya hivi karibuni ambayo safari hii yalihusisha pia kundi jingine la wanagambo wenye silaha lenye asili yake nchini Uganda, yamesababisha zaidi ya wananchi 100,000 kuyakimbia makazi yao na hivyo kuongeza mgogoro wa kibinadamu katika eneo hilo linalohusisha watu wengine 2.6 milioni ambao wameyakimbia makazi yao huku wengine 6.4 milioni wakihitaji chakula na huduma za dharura.
Wakati huo huo, Kaimu Mkuu wa MONUSCO Bw. Moustapha Soumare katika taarifa yake ametoa wito kwa pande zote kutafuta suluhu ya kisiasa kwa matatizo ya DRC kupitia Mpango Mpana wa Kisiasa wa Umoja wa Mataifa kuhusu amani, usalama na ushirikiano wa maendeleo katika DRC na eneo la Maziwa Makuu uliopitisha mwezi wa Februari na viongozi 11 wa Afrika na Taasisi nne za Kikanda na Kimataifa.
Aidha akasema katika kipindi hiki ambacho suluhu la kisiasa linatafutwa MONUSCO itatumia nguvu iliyonayo kuwalinda wananchi dhidi ya hatari zitokanazo na makundi ya waasi.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/07/waasi-wa-m23-mashariki-ya-kongo-wapewa.html#ixzz2ahTcr0jo
MUGABE KUNG'ATUKA AKISHINDWA UCHAGUZI...
Wednesday, July 31, 2013 | 9:03 PM
Rais Robert Mugabe
Raia wa Zimbabwe wanapiga kura katika uchaguzi wa Urais unaotajwa kuwa na ushindani mkali huku kukiwa na madai ya udanganyifu. Rais Robert Mugabe wa miaka 89 amesema atang’atuka ikiwa yeye na chama chake cha Zanu-PF watashindwa.
Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai na chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) wamelalamikia Zanu-PF kwa kuhitilafiana na utaratibu wa uchaguzi ili kunyakua ushindi, lakini chama tawala kimekanusha madai hayo.Shughuli za kampeini zimekua ghasia zozote huku kukiwa na visa vichache sana vya kuwatisha wapiga kura.
Vyama vya Zanu-PF na MDC viliunda serikali ya muungano mwaka wa 2008 baada ya muafaka wa kumaliza ghasia za baada ya uchaguzi kufuatia matokeo ya Urais yaliyozua utata. Bw. Tsvangirai alishinda awamu ya kwanza, lakini akajiondoa kwa raundi ya pili akilalamikia mashambulizi yaliyolenga wafuasi wake.
Serikali ya Zimbabwe imewapiga marufuku waangalizi wa magharibi kuchunguza uchaguzi wa leo. Hata hivyo Muungano wa Afrika (AU), Kanda ya Kusini mwa Afrika (SADC) na makundi ya kijamii nchini Zimbabwe yamekubaliwa kufuatilia jinsi uchaguzi utakavyoendeshwa.
Watu milioni 6.4 wamejiandikisha kupiga kura hii, na maelfu walijitokeza kwenye kampeini za uchaguzi. Matokeo yanatarajiwa kutolewa kwa siku tano zijazo. Mwandishi wa BBC aliyeko Harare amesema kuna foleni ndefu katika vituo vya kupigia kura ikiwa siku ya mapumzoko kuhakikisha raia wanapata nafasi ya kuamua serikali mpya.
Mshindi wa moja kwa moja sharti apate asili mia 50 ya kura zote kutangazwa Rais. Ikiwa hakuna mgombea atapata kura hizo, raundi ya pili imepangwa kufanyika Septemba 11. Uchaguzi huu ndio wa kwanza kufanyika Zimbabwe chini ya katiba mpya iliyopitishwa mnamo mwezi Machi mwaka huu.
source Gumzo la jiji.
Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/07/mugabe-kungatuka-akishindwa-uchaguzi.html#ixzz2ahS31eDj
Subscribe to:
Posts (Atom)