Wednesday, July 17, 2013

POLISI ASIMULIA JINSI WANAJJESHI WA TANZANIA WALIVYOUAWA KIKATILI HUKO DARFUL...!!

Tuesday, July 16, 2013 | 10:42 PM

Dar es Salaam. Wakati Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), likiwa bado halijatangaza rasmi majina ya wapiganaji wake waliofariki huko Sudan, askari polisi aliyeko huko ameeleza chanzo na mazingira ya tukio hilo. 
Wapiganaji saba na wengine 14 walijeruhiwa Jumamosi iliyopita.

Gazeti hili limepata majina ya askari hao waliofariki kutoka vyanzo tofauti lakini limeshindwa kuwataja leo kwa kuwa JWTZ kupitia kwa msemaji wake, Kanali Kapambala Mgawe limesisitiza kuwa haliwezi kutangaza majina hayo hadi litakapowasiliana na jamaa za askari waliofariki.

Tukio lilivyotokea

Akizungumza kwa sharti la kutotajwa jina, askari polisi huyo anayefanya kazi katika Mji wa Nyala uliopo Darfur, alisema mauaji hayo yalitokea wakati askari hao walipokuwa wakifuatilia magari yao yaliyokuwa yameporwa na kundi mojawapo la waasi.

Usalama katika Mji wa Nyala ambao ndiyo mkubwa zaidi katika eneo la Darfur, umekuwa mdogo katika siku za hivi karibuni. “Wale wanajeshi walikuwa doria ya kawaida, ila kama wiki moja iliyopita waasi walivamia tena doria ya wanajeshi wetu na kupora magari manne bila kuua mtu.

Siku ya mauaji hayo wanajeshi wetu wakiwa tena katika doria waliyaona yale magari yaliyoporwa kwa mbali yamepaki, waliyafuatilia, walipokaribia kumbe ulikuwa mtego, wakashambuliwa,” alisema askari huyo na kuongeza: “Mauaji hayo yametokea takriban kilometa 70 kutoka katika kambi niliyopo mimi, lakini wote tupo eneo la kusini na hiyo kambi ya Korabeche inaongozwa na jeshi letu.”

Tofauti na chanzo chetu cha habari huko Darfur, Kanali Mgawe alisema wanajeshi hao walishambuliwa walipokuwa kwenye msafara wa kusindikiza walinzi wa amani.

Makundi yanayopambana

Askari huyo aliyeko Darfur alisema: “Makundi yanayopambana huku yapo mengi ila makubwa yapo kama matano. Kuna moja linaitwa Jeshi la Ukombozi la Watu wa Sudan (SPLA), ambalo limegawanyika katika makundi mawili pia kuna mengine kama JEM, Janjaweed na mengineyo.”

Akizungumzia mshtuko walioupata baada ya mauaji hayo, askari huyo alisema wafanyakazi wote wanaohusika na ulinzi wa amani wamepatwa na ganzi... “Huku kwa kweli hali imekuwa chungu, tangu askari hao wauawe hali haitabiriki kabisa, tupo nje hapa (hospitali walimohifadhiwa), tunasubiri uhakika.”
“Hawa jamaa (waasi), wamesheheni silaha na wana vifaa vya kisasa kiasi kwamba hata ndugu zetu walizidiwa kutokana na wenzao kuwa na silaha nzito, nikija Tanzania nitakuonyesha picha za


Source: Gumzo la jiji.


Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/07/polisi-asimulia-jinsi-wanajjeshi-wa.html#ixzz2ZItxi4gp

No comments:

Post a Comment