Saturday, July 20, 2013

MIILI YA WANAJESHI WA JWTZ WALIOAWA HUKO DARFUL KUWASILI NCHINI LEO...!!

UPDATE:

Saturday, July 20, 2013 | 6:32 PM

 
Miili ya askari saba wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliouawa katika shambulio la kushtukiza katika jimbo la Darfur, nchini Sudan, inatarajiwa kuwasili leo mchana kwa ndege maalum.

“Miili ya askari wetu sasa itawasili saa 9 alasiri leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere (Terminal 1 Airwing), kisha itapelekwa moja kwa moja katika Hospitali ya Rufaa ya Jeshi Lugalo kuhifadhiwa,” ilisema taarifa hiyo ya jeshi jana Jijini Dar es Salaam.

Taarifa hiyo ilisema heshima ya mwisho ya kuwaaga wapiganaji hao, itafanyika Jumatatu saa 3:00 asubuhi katika Viwanja vya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga jijini Dar es Salaam.


Wanajeshi hao waliuawa katika shambulizi la kushtukiza toka katika kundi mojawapo la waasi katika jimbo la Darfur, na kusababisha askari wengine 14 kujeruhiwa.
Tukio hilo lilitokea wakati wanajeshi hao wakiwasindikiza waangalizi wa amani kutoka Khor Abeche kwenda Darfur umbali wa kilometa 20 wa Makao Makuu ya kikosi hicho.

Wakati shambulizo hilo linatokea, Tanzania ilikuwa na wanajeshi 36 katika msafara huo wakiwa ni miongoni mwa askari wa wanaolinda amani kwenye kikosi cha Umoja wa Mataifa (UN) jimboni Darfur nchini Sudan.

Kwa mujibu wa taarifa za awali, miili hiyo ilikuwa itolewe heshima za mwisho katika Hospitali ya Kijeshi la Lugalo, lakini ratiba ilibadilishwa baada ya kuonekana kuwa msiba huo ni wa kitaifa na wananchi wengi wangependa kushuhudia tukio hilo.
Aidha, kutokana na eneo hilo la jeshi kuwa nyeti na kuepuka usumbufu wa watu kuuliza vitambulisho, ilionekana ni muhimu watu wengi wakashiriki.

Taarifa zilieleza kuwa wanajeshi wote watafunga vitambaa vyeusi kwenye mikono yao kama ishara ya kuomboleza msiba huo mzito ulioukumba taifa.

source gumzo la jiji.


Read more: http://talkbongo.blogspot.com/2013/07/update-miili-ya-wanajeshi-wa-jwtz.html#ixzz2ZcQ5hqRJ

No comments:

Post a Comment