Sunday, May 18, 2014

CLOUDS FM SPORT XTRA BONANZA LAFANA SANA LEO JIJINI MWANZA.

Mashindano ya Bonanza la CLOUDS FM Lijulikanalo kama SPORTS XTRA BONANZA Limefanyika na kufana sana leo jijini Mwanza Ktk Viwanja vya RAILA ODINGA Ndani ya CHUO KIKUU CHA MT.AGUSTINO JIJINI MWANZA.
Clouds Fm Team ( The Dream Team at RAILA GROUND SAUT-MWANZA) With AMAN MBWAGA.

Clouds fm Team

SHAFIII DAUDA Akitoa maelekezo Kwenye Timu yake wakati wa michuano ya Bonanza


Aman E. Mbwaga Meneja Uhusiano wa Umma Na Masoko akiwa na Mbwiga Wa Mbwiguke wa CLOUDS FM

Amani Mbwaga Akiwa na Henry Joseph Mchezaji wa Timu ya Taifa Tanzania.

Baadhi ya Wanafunzi wa SAUT Waliohudhuria Bonanza hilo.

AMAN MBWAGA With SHAFII DAUDA

AMAN MBWAGA With ALEX LUAMBANO


Optatus Mazwile With Alex Luambano


Kushoto SHAFII DAUDA Katikati HALFANI NGASSA
( Baba yake na Mrisho Ngasa Mchezaji wa YOUNG AFRICANS ) Na Kulia  Ni Mbwiga










AMBULANCE YA JESHI LOA WANANCHI NALO LILIKUWEPO KUSINDIKIZA BONANZA HILO



Timu Ya NMB Mwanza  na a kulia mwishoni ni Meneja wa NMB kanda ya Ziwa Mara baada ya kutinga Fainali.


Timu ya CHUO SAUT iliyonyakuwa Ubingwa wa Sport xtra Bonanza kwa Mikwaju ya Penati mara baada ya kutoka Sare ya bila kufungana







Shafiiii Dauda







Wanafunzi  wakishanglia Ushindi 


Rev FR. Maziku SPORTS COORDINATOR SAUT. Kwa niaba ya chuo Akiwashukuru CLOUDS fm na Makampuni mengine Yaliyoshiriki.

Hapa akifanya Mahojiano na Clouds TV

Meneja wa NMB akitoa Hotuba Fupi kabla ya kukabidhi Makombe kwa washindi

Meneja Msoko Kanda ya Ziwa nae akitoa Machache.

Meneja Masoko wa Vodacom Nae Akitoa Machache

DAUDA Akimtambulisha Waziri wa Michezo SAUT. Bwana Peter Bega


Captain Wa Timu Ya NMB Wakikabidhiwa kombe la Mshindi wa Pili



Kushoto Rais wa Wanafunzi SAUT katikati ni Calvin Captain Timu ya Chuo Akipokea Zawadi ya Kombe la Mshindi wa Bonanza la Sports Xtra 2014/2015


Timu ya SAUT ikisheherekea Ushindi
Shafiii Dauda Akihitimisha na Kuwashukuru wadau wote wa soka na Clouds fm Walioonesha Ushirikiano Mkubwa ktk Mashindano hayo.

Timu ya SHERIA MWAKA WA NNE Imeingia Fanali FAWASCO- SAUT. mara baada ya Bonanza

Timu ya Masscommunication Fawasco -SAUT

Monday, May 12, 2014

Masharti ya Boko Haram kuhusu wasichana


Wasichana ambao kundi la Boko Haram liliwateka nyara
Kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekahu amesema kuwa atawaachilia huru wasichana waliotekwa nyara iwapo tu wapiganaji wa kundi hilo wanaozuiliwa na serikali ya Nigeria wataachiliwa huru.
Katika kanda mpya iliyotolewa na kundi hilo, kiongozi huyo, amesema kuwa wasichana hao waliweza kusilimu katika kipindi cha wiki nne zilizopita tangu watekwe nyara.
Walitekwa nyara kutoka katika shule yao mjini Chibok, Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyoKanda hiyo inaonyesha zaidi ya wanawake miamoja wakiwa wamevalia hijabu na kuswali. Abubaka Shekau anasema kuwa wanawake hao ni wasichana waliotekwa nyara na kundi hilo.
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekahu
Rais wa Ufaransa amejitolea kuwa mwenyeji wa mkutano utakaotafuta njia za kupambana na Boko Haram.
Wakati huohuo Waziri wa mambo ya ndani nchini Nigeria amesema serikali haitakubali masharti ya kundi la Boko Haram kwamba kwanza liwaachilie wapiganaji wake kabla ya wasichana zaidi ya miambili waliotekwa nyara waachiliwe.
Waziri Abba Moro amsema ni jambo la kipuuzi sana kwa kundi la kigaidi kujaribu kuweka masharti kama hayo.
Mwandishi wa BBC mjini Maiduguri John Simpson anasema kuwa masharti yaliyotolea na kundi hilo ni ishara kuwa liko tayari kufikia makubaliano na serikali
Wasichana watatu kati ya waliooyeshwa na kuongea katika kanda hiyo walikuwa wanavalia hijabu. Mmoja alisema kuwa amesilimu wakati mwingine akisema yeye tayari ni Muisilamu.

Wednesday, May 7, 2014

Mvua ya Samaki Sri Lanka


Samaki waliotoka mtoni kutokana na upepo mkali
Wakaazi wa kijiji kimoja Magharibi mwa Sri Lanka wamesema kuwa wameshangazwa na pia kufurahishwa na tukio la 'kunyeshewa' na mvua ya Samaki wadogo.
Samaki hawa ambao walikuwa katika hali nzuri ya kuweza kulika wanaaminika kuwa walibebwa kutoka kwa mto kwa upepo mkali.

Hili si tukio la kwanza la aina hii kuwahi kutokea Sri Lanka- mwaka wa 2012, kulitokea kisa cha mvua ya viumbe vya baharini vijulikanavyo kama 'Kamba' ambavyo huliwaWanakijiji hao wa wilaya ya Chilaw walisema kuwa walisikia kitu kizito kikianguka na wakapata samaki wengi wenye uzani wa kilo hamsini .
Wanasayansi wamesema kuwa mvua ya Samaki hutokea wakati ambapo upepo mkali unazinga juu ya maji ya kina kifupi na hivyo kusababisha mzunguko wa maji unaovuta karibu kila kitu kilicho ndani ya maji ikiwa ni pamoja na samaki na hata Vyura.
Wakazi wanasema sio mara ya kwanza kwa mvua ya Samaki kuwanyeshea
Viumbe hawa wa majini wanaweza wakasafirishwa kwa masafa marefu kwa kushikiliwa na mawingu hata baada ya ule mzunguko wa maji kuisha.
Wanakijiji wanasema kuwa mvua hiyo ya Samaki ilinyesha Jumatatu huku viumbe wale wakianguka kwenye mashamba, barabara na paa za kijiji hicho.
Baadhi ya samaki hao wenye urefu wa kati ya sentimita tano na nane, walikuwa bado wako hai na walitiwa kwenye ndoo za maji na wanakijiji waliowatumia kama kitoweo badaye.
Hii ni mara ya tatu kwa tukio kama hili kufanyika Sri Lanka, ingawa katika eneo tofauti.
Kando na ile mvua ya ‘Prawn’ya mwaka wa 2012 kusini mwa Sri Lanka, mvua ya kimondo (meteors) nyekundu na manjano ilinyesha mwaka huo huo,tukio ambalo bado linachunguzwa na wanasayansi wa Marekani na Uingereza.
Samaki wamadhamana kuu Sri Lanka.
Chanzo: Bbc