Saturday, June 8, 2013

REV. DR CHARLES KITIMA VICE CHANCELLOR AWAAGA WANAFUNZI WA SAUT JANA. KTK VIWANJA VYA RIOLA ODINGA

SSPRA KWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA WANAFUNZI YA CHUO KIKUU CHA MT.AUGUSTINO WAANDAA SHEREHE YA KUMUAGA PADRI DOKTA CHARLES KITIMA JANA KATIKA UWANJA WA RAILA ODINGA.

Aliyekuwa Makamu Mkuu wa Chuo cha Mt.Augustino Mwanza(SAUT) Mh.Padri Dokta Charles Kitima leo amewaaga wanafunzi na jumuiya yote ya mtakatifu augustino katika kiwanja cha raila odinga na kumkaribisha Makamu Mkuu Mpya Padri Pius Mgeni kuwa ndiye makamu mkuu wa chuo kwa sasa.

Akizungumza katika sherehe hiyo ya kumuaga padri charles kitima awewataka wasomi wote wa vyuo vikuu na viongozi wote kuiga mfumo wa hayati Mwalimu J.K Nyerere ambao aliutumia katika kuiongoza Tanganyika na kuwa mstari wa mbele katika kutetea rasimali za wazawa ambazo utoroshwa kwenda nje kwa njia za panya.

Aidha,Amewataka vijana kuendelea kusoma kazi mbalimbali ambazo Hayati Mwalimu JK Nyerere katika uhai wake aliwahi kuziandika kwa ajili ya watanzania,kama marejeo ya kuondokana na matatizo yanayoikabili la tanzania kwa sasa.

 Katika sherehe hiyo ya kumuaga iliendana sambamba na kikizinduua kitabu kipya kilichoandikwa na Boniphace Pesambili Mgeta ambaye ni mwanafunzi katika shahada ya mwasiliano ya umma(Bachelor of Arts in Mass Communications) katika chuo kikuu cha Mtakatifu Augustino Mwanza.Pia amempongeza boniphace kwa kuandika hicho kitabu na kutaka aendeleze weledi katika kuandika kazi ambazo zinatetea haki za watanzania.

Padri charles kitima ametoa zawadi ya kwa wanafunzi wote wa chuo kikuu cha mtakatifu augustino kwa kuwanunulia nakala 300 ya vitabu vilivyoandikwa na Bw. Boniphace Mgeta

Kitabu hicho kimeandikwa kufuatia tafiti mbalimbali zilizofanywa na wanafunzi wailosoma katika chuo hicho katika kafuta suluhisho la matatizo mbalimbali ambayo yanawakabiri watanzania kwa sasa.

Zoezi hilo la uzinduzi wa kitabu lilisindikizwa na wakuu wa idara mbalimbali,Idara ya mawasiliano ya umma,Mkuu wa Idara ya sheria,na Mkuu wa idara ya Mahusiano ya jamii na matangazo.

       




 























                       

























   

Monday, June 3, 2013

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA KAMPENI YA USAFI JIJINI MWANZA

MKUU WA MKOA WA MWANZA AFUNGUA KAMPENI YA USAFI JIJINI MWANZA

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh.Evarist Ndikiro amefungua rasmi kampeni ya kuweka jiji la Mwanza katika hali ya usafi akishirikiana kwa ukaribu kabisa na Meya wa jiji la Mwanza Mh.Stanslaus Mabula, kampeni hii imeandaliwa na Halmashauri ya jiji la Mwanza ikishirikiana kwa ukaribu kabisa na chuo kikuu cha mtakatifu Agustino (SAUT) kilichopo jijini hapa.Kampeni hii inalengo la kutoa elimu na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kuliweka jiji la Mwanza katika hali ya usafi, kampeni hii imekuwa na kauli mbiu hii 

          "Pamoja Tuliweke Jiji letu safi"

Mkuu wa mkoa wa mwanza MH.Evarist Ndikiro akiwa na baadhi ya viongozi wengine wa jiji la Mwanza katika kuzindua kampeni ya usafi leo katika jiji la mwanza.
Wa pili kutoka kushoto ni Meya wa jiji la Mwanza Stanslaus  Mabula pamoja na mkuu wa mkoa wa Mwanza Evarist Ndikiro katika kampeni ya usafi.
Mkuu wa mkoa wa mwanza mh.Evaristi Ndikiro akifanya usafi wa jiji la mwanza leo.
Wa pili kutoka kushoto ni meya wa jiji la mwanza na kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa mwanza Mh.Ndikiro wakifanya usafi
Mkuu wa mkoa wa mwanza akipewa  mfagio
Mkuu wa mkoa wa Mwanza akishika mfangio kama ishara ya kushirikiana na wakazi wa jiji la mwanza katika suala nzima la usafi.
Baadhi ya wanachama wa SSPRA kutoka chuo cha SAUT wakishiriki katika kufanya usafi pia.
hawa ni baadhi wa wakazi wa jiji la mwanza wakiwa katika zoezi la usafi ililofunguliwa leo na mkuu wa mkoa wa mwanza MH.Evarist Ndikiro 
    Baadhi ya wanachama wa sspra wakifanya usafi.


Kutoka kushoto ni rasi wa chuo cha mtakatifu augustino Mh. Dovakmwene Mscheshi akifanya usafi pamoja na wakazi wa jiji la mwanza.
 Wakazi wa jiji la mwanza wakifanya usafi
 Wakazi wa jiji la mwanza wakifanya zoezi la usafi leo
Mwenyekiti wa media and publications Mussa Mbilinyi akishiriki leo katika suala nzima la usafi wa jiji.