Tuesday, July 4, 2017

Hizi ndizo Sauti (3) zinachangia kuleta mafanikio

Mafanikio unayoyahitaji kesho msingi wake mkubwa huanzia leo. Ukitaka kufanikiwa inawezeketana kabisa tena mara moja ndani ya sekunde kadhaa tu. Tupo baadhi yetu huwa tunajikatisha wenyewe  tamaa wenyewe kwa kujisema wenyewe baadhi ya maneneo kama vile hivi nitaweza kweli? Maneno kama hayo yanakufanya uzidi kujiona wewe mnyonge na huwezi kusonga mbele siku zote. Kuna mwalimu wangu mmoja wa dini aliwahi kuniambia mdomo huumba kwa kile unachokisema ndicho kitakachokutokea, acha kujisemea maneno yenye kukutasha tamaa bali jinenee maneno ya ushindi siku zote.

Mara nyingi umekuwa ukisika zaidi kuliko kusikiza. Tofauti kubwa iliyopo kati ya kusikia na kusikiliza ni kama ifuatavyo, Kusikia ni kusikiliza kitu kwa juu juu tu bila kutilia umakini kwa kile unachokisikiliza mfano unasikia gari inatoa mgurumo, mtu atasikia sauti hii ile  lakini hata sikiliza. Ila kusikiliza ni kuwa makini kwa kile ambacho unasikiliza na kukielewa mfano mtu  akiamua kweli kusikiliza taarifa ya habari atakuwa makini na kuilewa na kinyume chake inawezekana pia.

Zifutazo ndizo sauti tatu zinazochangia mtu aweze kufanikiwa;

1. Sauti za watu tofauti tofauti.
Hizi ni zile aina na sauti ambazo umekuwa ukisikiliza kutoka kwa watu mbalimbali ambao wanakuzungua.. Hizi ni sauti za watu zenye kukutia moyo ili uweze kuongeza juhudi kwa jambo unalolitaka ili uweze kufanikiwa. Wapo baadhi ya watu utawasikia wanasema ukijitahidi kufanya vitu Fulani mfano katika masomo, biashara, kilimo na vitu vingine vingi utaweza kufanikiwa . Sauti hizi mtu huambiwa ili kumuongezea hamasa kwa kila jambo analofanya ili aweze kutimiza ndoto zako. Sauti hizi unaweza kusikia kutoka kwa watu waliofanikiwa hata wasiofanikiwa pia. Sauti hizi unaweza ukasikia katika semina na sehemu zinginezo.  Swali la kujiuliza  ni kwamba mafanikio yako yameletwa kwa njia hii au yataletwa kwa njia hii ya kuwasikiliza watu?

2.Sauti za historia mabalimbali.
Ni aina nyingine za sauti ambayo inachangia kwa kiwango Fulani mtu aweze kufani. Sauti hizi za histori ni zile sauti ambazo tunasikia kutoka kwa watu mbalimbali ambao bado wanaishi au hatupo nao tena kwa  kusikia historia kwa baadhi ya mambo ambayo waliyafanya na bado wanayafnaya  ili waweze kufanikiwa zaidi. Sauti hizi za historia tunazisikia kutoka kwa matajiri wakubwa kama vile wakina bill gate, ahmed backera na wengineo wengi. Sauti na historia zao zinatufanya tuone ni jinsi gani walianza na leo hii wameweza kufanikiwa na kuwa matajiri wakubwa. Historia zao zinatufanya tujione na sisi tunaweza na siku moja tutakuwa au tutakuwa zaidi ya wao.

3. Isikilize sauti yako.
Hii ndiyo sauti kubwa kuliko sauti zote.  Sauti hii ni nyembamba sana ambayo ipo ndani ya moyo wa mtu . Watu wachache ambao wanaitambua sauti hii, Sauti hii humfanya mtu yeyote aweze kufanikiwa mara moja endapo utaamua kusikiza sauti yake.  Endapo utaamua kujitambua na kusikiza sauti hii ndio siku ambayo umaskini utakuwa umeupiga teka. Ngoja niendelee kukupa madini juu ya sauti hii, Kila mtu amekuwa na sauti hii nyembembe lakini anashindwa kuitumia hii ni kutoka na mfumo wa maisha ya kwamba huwezi kufanya kitu chochote mpaka  mtu Fulani aamue juu ya maisha yako.

Ni watu wangapi leo wanafanya kazi kutokana na kusikiliza sauti za watu wengine kuliko kuzisikiliza sauti zao? Usinipe jibu. Ni watu wangapi leo hii wanajilaumu kwa kufanya kazi kwa ambazo hawazipendi hii ni kutokana walisikiza sauti za watu wengine? Ukichunguza kwa makini utagundua ni wachache mno wanaofanya kazi kwa upendo. Lakini ndugu msomaji wa makala haya kiukweli  sijui nikueleza vipi ili ujue sauti yako ndio ushindi wako ? lakini tambua ya kuwa  siku ambayo utaamua kuisikilza sauti nyembamba  ambavyo inatoka moyoni mwako ndio siku ambayo utafanikiwa. Tukumbuke  Bahati huja kwa waliojitayarisha
Chanzo Muungwana Blog

Umeipata hii ya Ajira kumwagwa?


SERIKALI inatarajia kutoa vibali 3,000 vya ajira katika sekta ya afya, zikihusisha madaktari na wauguzi kwa ajili ya vituo vya afya vya kata ili kuboresha sekta hiyo, imeelezwa hapa jana.

Pia serikali imetangaza kuwa itatoa vibali vya ajira za maofisa hesabu 535 kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati nchini ili kushughulikia ipasavyo ukusanyaji wa mapato.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk. Laurean Ndumbaro, ndiye aliyetangaza neema hiyo kwa wasomi wanaosubiri ajira serikalini wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha waganga wakuu wa mikoa na wilaya kuhusu maadili na uwajibikaji mahali pa kazi.

Alisema vibali vya ajira hizo vitatolewa wiki ijayo huku akiwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa kuzingatia sheria kanuni na taratibu ili kujenga utumishi wa umma wenye uadilifu.

"Naomba wanaoharibu wasihamishwe na kupelekwa maeneo mengine, wakifanya hivyo watakuwa wanaharibu utumishi wa umma, ufumbuzi ni kuchukua hatua palepale alipo," alisema Dk. Ndumbaro.

Aliongeza kuwa sekta zinatakiwa kujenga utamaduni wa kuwapongeza watumishi wa umma wanaofanya vizuri kwenye maeneo yao ya kazi ili wajitume zaidi na kuhamasisha wengine.

Katika kikao kazi hicho, Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara ambaye pia aliwahi kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Eliakim Maswi, alisema vituo vingi vya afya vimefungwa kutokana na watumishi kuwa na vyeti vya kughushi hivyo vingi havina watumishi.

Alisema uhakiki wa vyeti feki bado haujamalizika, lakini akasisitiza kuwa ni muhimu kwa sasa serikali kutoa vibali vya ajira mpya kwa kuwa watumishi waliobainika kuwa na vyeti vya kughushi ni wengi hivyo kuna haja ya kuziba pengo hilo.

Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Mpoki Ulisubisya alisema serikali itaendelea kuajiri watumishi katika sekta ya afya.

Katika ufafanuzi kuhusu ajira mpya zitakazotolewa wiki ijayo, Dk. Ulisubisya alisema kila mkoa utapata mgawo wa wataalamu hao watakaoungana na madaktari 258 ambao walisailiwa kwa ajili ya kwenda kufanya kazi Kenya, lakini baadaye wakaajiriwa nchini.

Katika mwaka huu wa fedha, serikali imeahidi kutoa vibali vya ajira za moja kwa moja 52,436 katika sekta zake mbalimbali.

Aprili 19, kufuatia Mahakama ya Kenya kutoondoa pingamizi lililofunguliwa dhidi ya ajira za madaktari kutoka nchini walioombwa huko, Rais John Magufuli aliamua wataalamu 258 waliokuwa wamejitokeza kuchangamkia fursa hiyo waajiriwe na serikali.

Madaktari hao ndiyo waliokidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya kati ya 496 waliokuwa wameomba.

Machi 18, ujumbe wa serikali ya Kenya ukiongozwa na Waziri wa Afya nchini humo, Dk. Cleopa Mailu ulikutana na Rais Magufuli na kuomba kuajiri kwa mkataba madaktari 500 ili kupunguza uhaba wa wataalamu hao wa afya uliotokana na mgomo nchini humo.

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Muhammad Kambi alipapata kusema idadi ya madaktari wanaohitajika nchini ni 3,510 na katika idadi hiyo, mahitaji zaidi yapo kwenye hospitali za wilaya kunakokosekana madaktari 832, za rufani (460), vituo vya afya (816), Bugando (152) na Hospitali ya Taifa Muhimbili madaktari 235.

Nyingine ni KCMC (143), hospitali za rufani za mikoa (460), madaktari 111 katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Hospitali ya Ocean Road (57), Mirembe (37), CCBRT (26) na Rufani Mbeya (106).

Mei 3, Waziri Kivuli wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Godwin Mollel aliliambia Bunge kuwa uwiano kati ya madaktari na wagonjwa nchini kwa sasa si mzuri.

Akinukuu ripoti ya Madaktari Wenza wa Afrika (Africa Cuamm) ya mwaka jana, Dk. Mollel alisema asilimia 74 ya madaktari wanaishi mjini na daktari mmoja anahudumia wagonjwa 78,880 kwa maeneo ya vijijini, kinyume cha maelekezo ya Shirika la Afya Duniani (WHO) linalotaka daktari mmoja ahudumie wagonjwa elfu moja (1:1,000).

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa Oktoba 2016, Tanzania ina upungufu wa asilimia 58.1 ya madaktari bingwa, wauguzi wa sekta ya umma II kwa asilimia 54.4, wataalamu wa miale kwa asilimia 50.8 na maofisa kliniki kwa asilimia 50.

Pia kuna upungufu wa madaktari wasaidizi na madaktari wasaidizi wa meno kwa asilimia 46.2, wafamasia kwa asilimia 49.9, mabwana afya kwa asilimia 45.7, mafundi sanifu wa maabara kwa asilimia 41.5, maofisa kliniki wasaidizi kwa asilimia 40.7 na madaktari kwa asilimia 37.3.

Wakati serikali ikishindwa kuajiri madaktari, Makamu wa Rais wa Chama cha Madaktari Tanzania (MAT), Dk. Obadia Nyongela, aliiambia Nipashe mwishoni mwa mwaka jana kuwa kuna madaktari 1,700 mtaani ambao wana sifa, lakini hawajaajiriwa.

"Kama mwaka huu (2016) utaisha bila vibali vya ajira kutoka, maana yake mpaka mwakani (2017) kutakuwa na madaktari 2,866 wasio na ajira licha ya kuwapo kwa upungufu wa wataalamu hao," alisema Dk. Nyongela.

Chanzo Muungwana Blog.

Saturday, July 1, 2017

PUBLIC RELATIONS & MARKETING MANAGER'S: JKT Kuongeza Idadi ya Vijana Vikosini.

PUBLIC RELATIONS & MARKETING MANAGER'S: JKT Kuongeza Idadi ya Vijana Vikosini.: Mahafali ya Ufungaji wa Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Oparesheni Magufuli Kujitolea Mafinga JKT, Tarehe 28 Juni, 2017 .                      ...

JKT Kuongeza Idadi ya Vijana Vikosini.

Mahafali ya Ufungaji wa Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Oparesheni Magufuli Kujitolea Mafinga JKT, Tarehe 28 Juni, 2017.                                                                                                                                       
Vijana wa Mafinga JKT Wakitoka nje ya Uwanja mara baada ya kumaliza Gwaride la Kuhitimu Mafunzo yao ya awali ya Kijeshi Tarehe 28 Juni 2017


Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Mufindi Jamhuri David William Akipokea Salamu ya Heshima Kutoka kwa Gwaride lililoandaliwa na Vijana wa Mafinga JKT Oparesheni Magufuli Kujitolea wakati wa Kuhitimu Mafunzo yao ya awali ya Kijeshi.
Na Amani Mbwaga                                                   
Mafinga, Tanzania.
Jeshi la kujenga Taifa JKT limejipanga kidete kuongeza idadi ya vijana wa Tanzania kujiunga na Mafunzo ya awali ya kijeshi, baada ya kufufua Vikosi na Makambi ya awali ya Jeshi hilo.

Hayo yamesemwa na Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Luteni Kanali AS Kagombola ambaye  ni Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii JKT, alipokuwa akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo Meja Jenerali Michael Isamuhyo, wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi ya Kundi Magufuli katika Kikosi cha Mafinga JKT, Kilichopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.

Mkuu wa JKT amempongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kwa kuona umuhimu wa vijana na  kufufua vikosi hivyo vya JKT.

Tarehe 15 Machi 1967 Kikosi cha Mafinga JKT Kilifunguliwa rasmi kikiwa na vijana wachache ambao walijiunga kufanya shughuli za kujenga Taifa.
Baadhi ya sababu za kuanzishwa kwa JKT ni Kubadili fikra za Vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya ukoloni ya kutegemea nchi nyingine ili kuleta Maendeleo, Kuwafunza Vijana Kujenga Mshikamano na umoja wa kitaifa ili kulinda uhuru wa Taifa lao.

Pia ni kuwaunganisha vijana bila kujali itikadi zao, kujifunza uzalendo na stadi za maisha ili waweze kujiajiri na kujitegemea mara wamalizapo mkataba wao wa kujitolea kwa miaka miwili.

Luteni Kanali Kagombola alisema, “katika kutambua hilo Serikali imerejesha Makambi Matano (05) yaliyokuwa yamesitishwa kufanya mafunzo,  ili kuongeza zaidi uwezo wa Kuchukua Idadi kubwa ya Vijana” Makambi yaliyofunguliwa ni 826 KJ Mpwapwa Dodoma, 839 KJ Makuyuni Arusha, 845 KJ Itaka Songwe, 846 KJ Luwa Rukwa, 847 Milundikwa Rukwa, wakati huohuo Makuyuni Arusha tayari imeshaanza kuchukua vijana na sasa wanaendelea na mafunzo.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe Jamhuri David William ambaye alikuwa Mgeni Rasmi na Kufunga Mafunzo hayo amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii, Uhodari,Uadilifu  na Weledi wa hali ya juu mara wapatapo nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama.

“Aidha kwa wale watakaomaliza mkataba wao wa JKT na kurudi nyumbani nawataka mkawe raia wema na kamwe msijiingize katika mambo ya uhalifu na ujambazi, bali mkashirikiane na jamii kwa yale mazuri mliyojifunza hapa Jeshini ili kuilinda nchi yetu na kuleta maendeleo kwa Taifa letu” alisema Mhe Jamhuri William.

Naye Mkuu wa Kikosi cha Mafinga JKT  Luteni Kanali Hamis Maiga aliwashukuru wahitimu wa kundi la Magufuli Kujitolea kwa kuwa na nidhamu kubwa wakati wote wa Mafunzo yao ya miezi sita.

Alisema Kikosi Kimepata vijana waadilifu wenye nidhamu na Ubunifu wa hali ya juu, kwani wametuachia Mashine ya Kusaga Nafaka na kupaki unga, Bwawa kubwa la Ufugaji wa Samaki  na mengine mengi.

Wito wake kwa vijana hawa wa JKT ni kutunza kiapo walichoapa cha Uhodari, Utii na Uaminifu, kwa lengo la kubadilisha changamoto zilizopo katika jamii na kuzibadili kuwa fursa.

Serikali ilirejesha Mafunzo ya JKT Kwa vijana wa Kujitolea mwaka 2001 baada ya kusitiswa mwaka 1994.
Oparesheni katika Mafunzo ya JKT zilizowahi kupita Toka 2001 ni:

Oparesheni Mkapa             2001
Ø Miaka 40 ya JKT                 2002
Ø Utandawazi                          2004
Ø Jiajiri                                    2005
Ø Kasi Mpya                             2006
Ø Maisha Bora                          2007
Ø Uadilifu                                  2008
Ø Kilimo Kwanza                      2009
Ø Uzalendo                                2010
Ø Miaka 50 ya Uhuru                2011
Ø Sensa                                      2012
Ø Miaka 50 ya JKT                    2013
Ø Miaka 50 ya Muungano          2014
Ø OP Kikwete                             2015
Ø OP Magufuli                            2016- Hadi Sasa.



                                      HABARI KATIKA PICHA.

Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Jamhuri David William akitoa hotuba  kwa Hadhira iliyohudhuria Mahafali ya Kuhitimu Mafunzo ya Awali Ya Kijeshi Katika Kikosi cha Jeshi  Mafinga
Mwakilishi wa  Mkuu a JKT Luteni Kanali AS Kagombola ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii JKT akijiandaa kutoa Salamu za Mkuu wa JKT

Kamanda  Kikosi wa Kikosi cha Jeshi Mafinga Luteni Kanali Hamis Maiga akitoa wito kwa vijana waliomaliza mafunzo ya awali ya Kijeshi, Kundi la OP Magufuli Kujitolea.
Kamanda Kikosi Luteni Kanali Hamis Maiga akimtambulisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Prof:Riziki Shemdowe
Paredi Kamanda Kapteni  Bakari Namgugu Akimshukuru Mgeni Rasmi Mara baada ya Kumaliza Ukaguzi wa Gadi za Maonesho ya kwata ya Mwendo wa Pole Na Haraka, katika Mahafali ya Vijana  JKT Oparesheni Magufuli Kijitolea Katika Kikosi cha Jeshi Mafinga.











BrassBand ya Mafinga JKT Ikitulia wakati wa Ukaguzi wa Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Mufindi wakati wa Mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya awali ya Kijeshi Kikosini Hapo.

Gwaride likitoka nje ya Uwanja.


Baadhi ya Ndugu , Jamaa, Marafiki na Wananchi wa Mkoa wa Iringa Wakifuatilia Kwa Makini Sherehe  Za Kumaliza Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Katika Kikosi Jeshi Mafinga.

Kikundi cha Singe


Kikundi cha Sarakasi cha Mafinga JKT








Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Katikati akiwa katika Picha Ya Pamoja na Wakuu   mbalimbali wa vikosi vya Jeshi waliosimama nyuma.
Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya Pamoja na Kamati Tendaji ya Kikosi cha Jeshi Mafinga




Mgeni Ramsi akiwa Katika Picha Ya Pamoja Viongozi wa Serikali ya Vijana Op Magufuli


Bwawa la Ufugaji wa Samaki la Kikosi cha Jeshi Mafinga Unaosimamiwa na Vijana wa Kujitolea  Mafinga JKT

Vijana wa JKT Mafinga (SM) Oparesheni Magufuli wakilisha Samaki Chakula

Kijana wa JKT (SM) Oparesheni Magufuli akiwapa elimu ya Ufugaji wa Samaki Wazalendo wa Mujibu waSheria waliomaliza Kidato cha Sita Mwaka Huu.


Jengo la Kiwanda Kidogo cha Kusaga nafaka na Kupaki Unga Bora Cha Mafinga JKT.

Kwa Mawasiliano Zaidi.
Mob: + 255 656 632 566
           :+  255 765 058 711
Twiter:@amanmbwaga