Mahafali ya Ufungaji wa Mafunzo ya Awali ya Kijeshi Oparesheni Magufuli Kujitolea Mafinga JKT, Tarehe 28 Juni, 2017.
Vijana wa Mafinga JKT Wakitoka nje ya Uwanja mara baada ya kumaliza Gwaride la Kuhitimu Mafunzo yao ya awali ya Kijeshi Tarehe 28 Juni 2017 |
Na Amani Mbwaga
Mafinga, Tanzania.
Jeshi
la kujenga Taifa JKT limejipanga kidete kuongeza idadi ya vijana wa Tanzania
kujiunga na Mafunzo ya awali ya kijeshi, baada ya kufufua Vikosi na Makambi ya
awali ya Jeshi hilo.
Hayo
yamesemwa na Mwakilishi wa Mkuu wa JKT Luteni Kanali AS Kagombola ambaye ni Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii JKT,
alipokuwa akitoa salamu kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo Meja Jenerali Michael
Isamuhyo, wakati wa kufunga mafunzo ya awali ya kijeshi ya Kundi Magufuli
katika Kikosi cha Mafinga JKT, Kilichopo wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Mkuu
wa JKT amempongeza Mh Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe
Magufuli kwa kuona umuhimu wa vijana na
kufufua vikosi hivyo vya JKT.
Tarehe 15 Machi 1967
Kikosi cha Mafinga JKT Kilifunguliwa rasmi kikiwa na vijana wachache ambao
walijiunga kufanya shughuli za kujenga Taifa.
Baadhi ya sababu za
kuanzishwa kwa JKT ni Kubadili fikra za Vijana wa nchi hii kutoka ile hali ya
ukoloni ya kutegemea nchi nyingine ili kuleta Maendeleo, Kuwafunza Vijana
Kujenga Mshikamano na umoja wa kitaifa ili kulinda uhuru wa Taifa lao.
Pia ni kuwaunganisha
vijana bila kujali itikadi zao, kujifunza uzalendo na stadi za maisha ili
waweze kujiajiri na kujitegemea mara wamalizapo mkataba wao wa kujitolea kwa
miaka miwili.
Luteni
Kanali Kagombola alisema, “katika kutambua hilo Serikali imerejesha Makambi
Matano (05) yaliyokuwa yamesitishwa kufanya mafunzo, ili kuongeza zaidi uwezo wa Kuchukua Idadi
kubwa ya Vijana” Makambi yaliyofunguliwa ni 826 KJ Mpwapwa Dodoma, 839 KJ
Makuyuni Arusha, 845 KJ Itaka Songwe, 846 KJ Luwa Rukwa, 847 Milundikwa Rukwa,
wakati huohuo Makuyuni Arusha tayari imeshaanza kuchukua vijana na sasa wanaendelea
na mafunzo.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe Jamhuri David William ambaye alikuwa
Mgeni Rasmi na Kufunga Mafunzo hayo amewataka vijana kufanya kazi kwa bidii,
Uhodari,Uadilifu na Weledi wa hali ya
juu mara wapatapo nafasi za ajira katika vyombo vya ulinzi na usalama.
“Aidha
kwa wale watakaomaliza mkataba wao wa JKT na kurudi nyumbani nawataka mkawe
raia wema na kamwe msijiingize katika mambo ya uhalifu na ujambazi, bali
mkashirikiane na jamii kwa yale mazuri mliyojifunza hapa Jeshini ili kuilinda
nchi yetu na kuleta maendeleo kwa Taifa letu” alisema Mhe Jamhuri William.
Naye
Mkuu wa Kikosi cha Mafinga JKT Luteni
Kanali Hamis Maiga aliwashukuru wahitimu wa kundi la Magufuli Kujitolea kwa
kuwa na nidhamu kubwa wakati wote wa Mafunzo yao ya miezi sita.
Alisema
Kikosi Kimepata vijana waadilifu wenye nidhamu na Ubunifu wa hali ya juu, kwani
wametuachia Mashine ya Kusaga Nafaka na kupaki unga, Bwawa kubwa la Ufugaji wa
Samaki na mengine mengi.
Wito
wake kwa vijana hawa wa JKT ni kutunza kiapo walichoapa cha Uhodari, Utii na
Uaminifu, kwa lengo la kubadilisha changamoto zilizopo katika jamii na
kuzibadili kuwa fursa.
Serikali ilirejesha
Mafunzo ya JKT Kwa vijana wa Kujitolea mwaka 2001 baada ya kusitiswa mwaka
1994.
Oparesheni katika
Mafunzo ya JKT zilizowahi kupita Toka 2001 ni:
Oparesheni Mkapa 2001
Oparesheni Mkapa 2001
Ø Miaka
40 ya JKT 2002
Ø Utandawazi 2004
Ø Jiajiri 2005
Ø Kasi
Mpya 2006
Ø Maisha
Bora 2007
Ø Uadilifu 2008
Ø Kilimo
Kwanza 2009
Ø Uzalendo 2010
Ø Miaka
50 ya Uhuru 2011
Ø Sensa 2012
Ø Miaka
50 ya JKT 2013
Ø Miaka
50 ya Muungano 2014
Ø OP
Kikwete 2015
Ø OP
Magufuli 2016-
Hadi Sasa.
HABARI KATIKA PICHA.
Kamanda Kikosi wa Kikosi cha Jeshi Mafinga Luteni Kanali Hamis Maiga akitoa wito kwa vijana waliomaliza mafunzo ya awali ya Kijeshi, Kundi la OP Magufuli Kujitolea.
|
BrassBand ya Mafinga JKT Ikitulia wakati wa Ukaguzi wa Mgeni Rasmi Mkuu wa wilaya ya Mufindi wakati wa Mahafali ya Kumaliza Mafunzo ya awali ya Kijeshi Kikosini Hapo.
|
Kikundi cha Sarakasi cha Mafinga JKT |
Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Katikati akiwa katika Picha Ya Pamoja na Wakuu mbalimbali wa vikosi vya Jeshi waliosimama nyuma. |
Mgeni Rasmi akiwa katika picha ya Pamoja na Kamati Tendaji ya Kikosi cha Jeshi Mafinga |
Mgeni Ramsi akiwa Katika Picha Ya Pamoja Viongozi wa Serikali ya Vijana Op Magufuli |
Bwawa la Ufugaji wa Samaki la Kikosi cha Jeshi Mafinga Unaosimamiwa na Vijana wa Kujitolea Mafinga JKT |
Vijana wa JKT Mafinga (SM) Oparesheni Magufuli wakilisha Samaki Chakula |
Kijana wa JKT (SM) Oparesheni Magufuli akiwapa elimu ya Ufugaji wa Samaki Wazalendo wa Mujibu waSheria waliomaliza Kidato cha Sita Mwaka Huu. |
Jengo la Kiwanda Kidogo cha Kusaga nafaka na Kupaki Unga Bora Cha Mafinga JKT. |
Kwa Mawasiliano Zaidi.
Mob: + 255 656 632 566
:+ 255 765 058 711
Twiter:@amanmbwaga
Whatsapp: 0656632 566
No comments:
Post a Comment