Wednesday, October 30, 2013

Tanzania: Tunaweza kujitoa A. Mashariki


Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete
Serikali ya Tanzania imesema inatafakari ushiriki wake ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na inaweza kujitoa ndani ya Jumuiya hiyo iwapo itaendelea kutengwa katika baadhi ya vikao.
Aidha imesema Tanzania haitambui vikao vinavyofanywa na nchi tatu zilizopo ndani ya Jumuiya hiyo ambazo zimekuwa zikizitenga Tanzania na Burundi.
Katika mikutano iliyofanyika hivi karibuni Tanzania na Burundi hazikualikwa kwenye vikao hivyo.Waziri anayehusika na masuala ya Afrika Mashariki wa Tanzania Samwel Sitta ameliambia Bunge la Tanzania kuwa makubaliano ya vikao hivyo vinavyofanywa na nchi za Kenya, Rwanda na Uganda yatatekelezwa na nchi hizo zinazofanya vikao hivyo kwa sababu vinafanyika nje ya utaratibu wa mkataba wa jumuiya hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri Sitta mikutano ya wakuu wa nchi za Rwanda, Kenya na Uganda ambayo ilianza kwa kuitenga Tanzania ilifanyika Entebbe nchini Uganda mwezi Juni mwaka huu na kufuatiwa na mkutano wa pili uliofanyika Agosti mwaka huu huko Mombasa nchini Kenya ambapo nchi hizo tatu bila kuishirikisha Tanzania walizungumzia uanzishaji wa himaya moja ya forodha.
Mambo mengine waliyozungumza wakuu hao ilikuwa uanzishaji wa visa moja ya utalii kwa nchi zao na matumizi ya vitambulisho vya uraia ambavyo vitatumika kama hati za kusafiria miongoni mwa nchi hizo.
Aidha Waziri Sitta amesema ndani ya mikutano hiyo pia walizungumzia kuanzisha mchakato wa kuanzisha shirikisho la nchi hizo.
Tayari Tanzania imeanza mazungumzo na nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kuangalia ni kwa namna gani zitaanzisha ushirikiano nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kama zinavyofanya nchi za Rwanda, Uganda na Kenya.

source bbc swahili

BREAKING NEWZ...!! TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI WA POLISI KWA WAHITIMU WA VYUO VIKUU NA UFUNDI....TAZAMA MAJINA HAPA




Jeshi la Polisi Tanzania linawaita kwenye usaili wahitimu walioorodheshwa hapa chini wa vyuo vya Elimu ya Juu na  vya Ufundi  Stadi. 
 
Usaili utafanyika kuanzia tarehe 11/11/2003 hadi tarehe 15/11/2013 saa mbili asubuhi hadi saa kumi jioni kila siku kwa taaluma na maeneo yafuatayo;
  •  Fani za Menejimenti  ya Rasilimali Watu, Utawala, Uchumi, Usimamizi wa Sheria na Utekelezaji(BaLe), Ualimu, Sosholojia, Saikolojia na Ushauri Nasihi, Sheria, Takwimu, Lugha, Uhusiano wa Kimataifa, Uandishi wa habari na Mawasiliano ya Umma, Maendeleo ya Jamii, Ukutubi na Utunzaji Kumbukumbu. Usaili  wa fani hizi  utafanyika katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam(DPA) kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam .
  • Fani ya Udereva ,Ufundi rangi za magari(spray and Painting /Panel Beating ), Ufundi wa matengenezo ya Magari Makubwa(Auto-Mechanics-Heavy Duty) na Ufundi wa Matengenezo ya Umeme wa Magari(Auto Elecrical ). Usaili wa  fani hizi utafanyika Kikosi cha Polisi Ufundi kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
  • Fani za Kompyuta. Usaili wao utafanyika nyuma ya kikosi cha Ufundi yaani  TEHAMA KEKO chini.
  • Fani ya Uhandisi Mitambo(Mechanical Engineering ). Usaili wao utafanyika Kikosi cha Polisi Anga kilichopo Uwanja wa Ndege JK Nyerere DSM.
  • Waataalam wa masuala ya Afya/Wauguzi usaili wao utafanyika katika kikosi cha afya kilichopo kando kando ya barabara ya Kilwa Kurasini Dar es salaam.
  • Orodha  ya majina inapatikana  pia katika Gazeti la habari Leo la tarehe  04/11/2013.
   Muhimu: 
  1. (i)Mwombaji afike kwenyeakiwa na nakala  halisi  pamoja na kivuli cha  vyeti vyote vya masomo/Taaluma [Academic Transcript (s)/Certificate(s)]yaani  kidato cha nne, sita ,Chuo na cheti cha kuzaliwa.Hati ya kiapo cha kuzaliwa haitakubalika. 
  1. (ii)Mwombaji aliyeitwa kwenye usaili atalipia gharamaupimaji afya  shilingi elfu kumi(10,000), usafiri, chakula na malazi kwa muda wote wa zoezi la usaili.
 (iii)Kwa kuwa  muda ni mchache  anaekuja kwa usaili ajiandae baada ya usaili atakaechaguliwa  atapelekwa katika Chuo cha Taaluma ya Polisi Moshi siku nne baada ya usaili kwisha yaani tarehe 19/11/2013.
 Orodha ni kama ifuatavyo;

BOFYA HAPO CHINI UDOWNLOAD MAJINA
-http://www.policeforce.go.tz


Read more: http://www.vitukovyamtaanews.com/2013/10/breaking-newz-tangazo-la-kuitwa-kwenye.html#ixzz2jETtQs1P

UN:Makali ya waasi wa M23 yamekwisha



Jeshi la serikali lineonekana hapa likiingia katika mji wa Rumangabo baada ya kuwafurusha waasi
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa katika Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo, ameambia baraza la usalama la Umoja huo kuwa makali ya kundi la waasi la M23 kama tisho la kijeshi yamekwisha
Martin Kobler alisema kuwa kundi hilo limeondoka katika maeneo yao ya kivita mashariki kwa DRC, na kwamba sasa wako katika eneo dogo karibu na mpaka wa Rwanda.
Eneo lengine la tano lililokuwa ngome ya waasi hao liliweza kudhibitiwa na jeshi la serikali siku ya Jumatatu.
Waasi hao wanasema kuwa wameondoka katika maeneo yao ya vita kwa muda.
Aidha bwana Kobler aliambia baraza al usalama kupitia kwa njia ya Skype kuwa kwa sasa ni kama kundi ilo limefika mwisho wake.
Aliongeza kwamba waasi wameondoka katika ngome yao moja kuu ya mlima Hehu karibu na mpaka wa Rwanda.
Baada ya mkutano huo, balozi wa Ufaransa Gerard Araud alisema anatumai kutakuwa na mazungumzo sasa kati ya waasi hao na serikali.
Alisema: ‘‘Bwana Kobler ametuarifu kuwa wanashuhudia mwisho wa kundi la M23 kama tisho la kijeshi. Kwa hivyo naona kama ni hatua nzuri na kwamba hata kulikuwa na makubaliano kuwa sasa tushinikize mazungumzo kuanza tena mjini Kampala.’’
Mazungumzo ya amani kati ya serikali na waasi wa M23, mjini Kampala, yalisitishwa wiki jana.
Hali hata hivyo hali ilikuwa imetulia Mashariki mwa DRC kwa muda wa wiki moja.
Watu walionekana wakishangilia wakati wanajeshi walipoingia mji wa Rumangabo ambao ulikuwa umetekwa na waasi hao
Na sasa serikali inadhibiti hali mjini humo, kwa mujibu wa gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini, Julien Paluku.
‘‘Tumekuwa na mikutano miwili ili kujadili tutakavyoimarisha hali ya wananchi...na tutatangaza kuanza tena kutolewa kwa huduma za serikali katika muda wa masaa 24,’’ alisema Paluku.
Mji wa Rumangabo – ulio umbali wa kilomita 50 Kaskazini mwa Goma, mji rasmi wa Mashariki mwa DRC, ulikuwa na kambi tatu kubwa za kijeshi nchini humo kabla ya kutekwa na waasi wa M23 mwaka jana.
Hapana shaka kuwa majeshi ya serikali yamefikia hatua kubwa na kupata ushindi mkubwa dhidi ya waasi,

Tuesday, October 29, 2013

Sir Alex Ferguson awapa moyo Man U

Ferguson alistaafu baada ya kuiongoza klabu kwa miaka 27
Aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesema kuwa wachezaji wa Man U wanaweza kubadili mwanzo wao mbaya kwenye ligi ya Premier, licha ya kuwa pointi nane nyuma ya timu inayoongoza ligi hiyo kwa sasa Arsenal.
Ushindi mara mbili wa timu hiyo katika mechi mbili zilizopita , ina maana kuwa upande wa David Moyes wameweza kujikomboa kutokana na matokeo mabaya zaidi ya Man U katika mwanzo wa ligi hiyo, kuwahi kushuhudiwa katika miaka 24 ya klabu hiyo.
Ferguson, mwenye umri wa miaka 71, alisema sio mara ya kwanza kwa klabu hiyo kuwa na mwanzo mbaya wa msimu. Imetokea mara nyingi.
"Man U ndio klabu pekee kuwahi kutoka nyuma kwa pointi na hatimaye kushinda ligi,'' alisema Ferguson
Ferguson, aliyesalia kuwa mmoja wa wakurugenzi wa klabu hiyo , alistaafu kutoka katika wadhifa wa meneja mkuu wa klabu mwishoni mwa msimu baada ya kushinda mataji 38 katika usimamizi wake wa miaka 27.
Naye menaja mpya Moyes anakumwba na wakati mgumu upande wa mashabiki baada ya kuanza vibaya msimu.
source: bbc swahili

Arsenal nje ya kombe la Capital One


Juan Mata wa Chelsea akisherekea bao dhidi ya Arsenal
Katika mashindano ya Capital one huko uingereza Arsenal ambao wako kileleni mwa ligi kuu ya uingereza waligaragazwa bila huruma na Chelsea kwa mabao mawili kwa bila. Lakini Chlesea walipokuwa wakiwatesa the Arsenal nyumbani kwao Manchester United waliwachapa Norwich kwa mabao manne kwa bila.
Hii inafanya Man u Kushinda mara sita mfulululizo, bila shaka na kumpa Moyes matumaini ya kufanya vizuri katika ligii ya Uingereza halikadhalika kombe hilo la Capital one.
Na katika kile kinachonekana kuwa wanasoka wa afrika wameshuka katika chati ni kiungo wa kati Yaya Toure pekee kutoka Ivory Coast ambaye yumo katika orodha ya wachezaji 23 walioteuliwa kuwaniwa tuzo ya mchezaji bora wa Fifa mwaka huo.
Kwa sasa wachezaji nyota wa zamani kama Didier Drogba, Samuel Eto'o na Michael Essien wanaonekana kufifia.
Na Yaya Toure yuko nchini Kenya katika juhudi za kupiga vita biashara haramu ya pembe za ndovu.
Toure saa ni balozi wa shirika la mazingira duniani UNEP. Mchezaji huyo mshidi mara mbili barani Afrika alifurahi katika hotuba yake kukubali wadhifa huo mpya.

source bbc swahili.

Miaka 35 jela kwa njama ya kumuua Mandela


 29 Oktoba, 2013 - Saa 11:51 GMT
Mike du Toit aliongoza kundi la kibaguzi la Boeremag kuwashambulia waafrika weusi na kupanga kumuua Mandela
Kiongozi wa njama ya waliokuwa wanaharakati wa kibaguzi nchini Afrika Kusini kumuua Nelson Mandela na kuwafukuza waafrika weusi kutoka nchini humo, amefungwa jela kwa miaka 35. Hii ni kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo.
Kiongozi huyo aliyekuwa mhadhiri wa huo kikuu Mike du Toit alipatikana na hatia mwaka jana kwa kosa la uhaini, kwa kukiokongoza kikundi hicho katika kupanga njama ya kumuua Mandela. Kesi yake ilisikilizwa kwa miaka 9.
Aliongoza kundi la wapiganaji wa Boeremag, wabaguzi wakuu wa kizungu nchini humo.
Mnamo mwaka 2002 wapiganaji hao walijaribu kuipindua serikali iliyokuwa inaongozwa na chama tawala cha ANC.
Wanachama wengine 20 wa Boeremag waliopatikana na hatia kwa kosa la uhaini, walihukumiwa jela kwa kati ya miaka mitano na 35 katika mahakama moja mjini Pretoria.
Mnamo mwezi Julai mwaka 2012 du Toit alipatikana na hatia ya mashambulizi ya mabomu katika mtaa wa mabanda wa Soweto mjini Johannesburg mwaka 2002.
Alikuwa mtu wa kwanza kuwahi kupatikana na hatia ya kosa la uhaini nchini Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa kibaguzi mwaka 1994.
Wadadisi wanasema kuwa huku swala la ubaguzi likiendelea kuwa changamoto nchini Afrika Kusini makundi yenye itikadi kali za kibaguzi kama Boeremag, hayana ushawishi mkubwa

SOURCE bbc swahili.

Wednesday, October 23, 2013

Majina ya vyuo 9 vilivyofutwa na Serikali kwa kukosa sifa

.

Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi  imevifuta vyuo ambavyo havina sifa ikiwamo kukosa usajili wa Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na kufundishwa na walimu wasio na sifa.  Vyuo vilivyotangazwa kufutwa ni:-

1.Media and Values Training Institute(Dar es Salaam)

2.Information Technology Training Center(Dar es Salaam)

3.Dar es Salaam School of Hair Design (Dar es Salaam)

4.Morogoro School of Medical Sciences (Morogoro)

5.Media and Research Center

6.Vision Hotel and Tourism College

7.East Africa College of Hospitality and Tourism

8.The Africa Institute of Business Management

9.Aspiration Training Center


Naibu Waziri wa Wizara husika , Philip Mulugo, alitangaza hatua hiyo wakati alipokutana na Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, katika ofisi ndogo za Bunge jijini Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Profesa Sifuni Mchome, alisema Serikali ilishatangaza kuwa vyuo visivyo na sifa vifungwe lakini tatizo likawa ni jinsi ya kuwatafutia wanafunzi waliopo vyuo vingine

SOURCE WAVUTI.







Friday, October 18, 2013

JE UMEMALIZA CHUO CHA SAUT-MWANZA?PATA TAARIFA ZOTE ZA GHARAMA YA MAHAFALI NA MAHITAJI MENGINE HAPA

KARIBU KATIKA KONGAMANO KUBWA LA AFYA NA MAHUSIANO LITAKALOFANYIKA KATIKA CHUO CHA SAUT: JUMAMOSI HII




Jumamosi tar.19/10/2013 kutakuwa "KONGAMANO KUBWA LA AFYA NA MAHUSIANO" litakalofanyika katika Chuo Kikuu Cha St.Augustine, ukumbi wa M13 kuanzia saa tatu (03) asubuhi hadi saa saba (07) mchana. 
Mgeni Rasmi ni Waziri wa Afya Mh.Husein Mwinyi,mgeni Maalumu ni Mh.James Mbatia (Mbunge na Mwenyekiti wa asasi ya Utu-Mtanzania)

Kongamano hili lilikuwa liende sambamba na uzinduzi wa Kitabu kiitwacho “TUMAINI LANGU, ELIMU YANGU”kilichoandikwa na Godlisen Malisa aliyekuwa rais wa chuo mwaka 2012-2013. 

Kongamano hili nimeandaliwa mahususi kutoa nafasi kwa vijana wasomi kujadili kuhusu afya zao, mahusiano yao, na hatari ya maambukizi ya VVU kwa wasomi wetu.

Kongamano litajumuisha uwasilishaji wa mada zilizofanyiwa utafiti wa kina juu ya MAHUSIANO HATARISHI yanayoweza kupelekea maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa vijana wasomi.

Karibu uje ukutane na Waziri mwenye dhamana ya Afya uweze kuuliza mambo yote muhimu kuhusu wizara yake.

Karibu ukutane na mwanaharakati James Mbatia, akuelimishe na kukufundisha umuhimu wa Elimu yako na namna ya kuepuka maambukizi hatarishi. Karibu utoe maoni, uulize maswali, uchangie hoja etc.

Kongamano litajumuisha wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali vya kanda ya ziwa ikiwemo CBE, IJA, DIT, TIA, OPEN University, Chuo cha waalimu Butimba, Chuo Kikuu cha Sayansi ya Afya Bugando, Chuo cha Uuguzi Bukumbi, Chuo cha Uvuvi Nyegezi, Chuo Kikuu Kishiriki cha Mt.Meru Mwanza campus, nk.

Kwanini vijana wengi wasomi wanajiiingiza katika Mahusiano hatarishi? Ni kweli kuchelewa kwa “boom” kunachangia mabinti wasomi kujiuza? Je ni kweli WATOTO WA MAMA SALMA wapo vyuoni? Je haiwezekani kuwa na mpenzi mmoja kuanzia First year hadi third year? Etc.

Hayo na mengine mengi utayapata ukihudhuria Kongamano hili la kwanza na la aina yake kuwahi kufanyika nchini hasa kanda hii ya ziwa.

Mada zitawasilishwa na wahadhiri kutoka chuo kikuu cha SAayansi ya Tiba Bugando na Chuo Kikuu SAUT.

Pia kongamano hili litafungua rasmi mashindano ya uandishi wa Insha juu ya sababu za wasomi wa vyuo vya elimu ya juu kujiingiza katika mahusiano hatarishi na suluhisho lake. Mshindi katika uandishi wa Insha atazawadiwa Sh.200,000/= Taslimu.

Burudani zitakuwepo za kusisimua na tragicomedy za kuelimisha pia zitakuwepo.

Vyombo mbalimbali vya habari vitakuwepo, ikiwa ni pamoja na ITV, StarTv, na magazeti mbalimbali. Radio SAUT Fm watarusha kongamano hilo na baadae litarudiwa kwenye vipindi vya usiku, kwa wale watakaoshindwa kusikiliza mchana.

Shukrani za dhati ziende kwa Uongozi wa Chuo cha SAUT, Radio SAUT Fm, Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), Asasi ya Utu Mtanzania, Shirika la Pensheni kwa watumishi wa Serikali za Mitaa (LAPF), Moil Petroleum, AprilMey Entertainment, Wizara ya Afya na Mazingira SAUTSO na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine wamefanikisha kuandaa kongamono hili.

Shukrani pia zikufikie wewe utakayesoma hapa na kuhamasisha wenzio kushiriki. Fikisha taarifa hizi kwa watu wengi kadri uwezavyo. Pia Jitahidi sana kuwahi ili usikose nafasi.! Ukipata ujumbe huu wajulishe wenzio

source nyanja.

Tuesday, October 15, 2013

JESHI LA NIGERIA LIMEWAUWA WAPIGANAJI 150

Jeshi la Nigeria lawaua wapiganaji 150

Wanajeshi 9 wangali hawajulikani waliko baada ya makabiliano makali kuzuka kati ya wapiganaji na wanajeshi hao mjini Borno
Jeshi la Nigeria, linasema kuwa limewaua wapiganaji 150 wa kundi la wapiganaji wa kiisilamu la Boko Haram wakati wa msako dhidi yao wiki jana.
Makabiliano yalitokea wakati jeshi lilipokuwa linafanya msako dhidi ya wapiganaji hao katika jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa nchi.
Wanajeshi wengine wa serikali wanasemekana kutojulikana waliko. Aidha jeshi lilisema pia liliweza kumuua kamanda wa wapiganaji hao Abba Goroma.Katika taarifa yake, jeshi lilisema kuwa takriban wanajeshi 16, walifariki wakati walipofanya shambulizi la kwanza dhidi ya kambi ya wanajeshi hao ambako walipata silaha nzito
Mwandishi wa BBC nchini Nigeria anasema kuwa, jeshi kwa kawaida huongeza chumvi idadi ya wapiganaji waliouawa kwa lengo la kuonyesha kuwa wanajeshi waliouawa kwenye mapigano walikuwa wachache.
Boko Haram ilianza harakati zake mwaka 2009 katika jimbo la Borno ambalo hadi sasa liko chini ya sheria ya hali ya hatari.

SOURCE BBC Swahili

Thursday, October 10, 2013

Fedha za Mrisho Ngassa zakamatwa






UNAZIKUMBUKA zile Sh45 milioni ambazo, Mrisho Ngassa alipeleka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ili kuilipa Simba? Zimezua utata.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imeingilia kati malipo ya Sh 45 milioni ambazo Mrisho Ngassa aliilipa Simba na kulitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuzuia kwa muda mpaka zilipiwe kodi.
Hata hivyo, tayari TFF imeilipa Simba Sh 40 milioni, huku ikibakiza Sh5 milioni wakati bado inasubiri maelekezo kamili ya TRA.
Ngassa alipeleka hundi ya Sh45 milioni kwa TFF ili wailipe Simba wiki iliyopita baada ya kuamriwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji kufanya hivyo kutokana na kusaini mkataba wa klabu mbili.
Hata hivyo, Simba imelipwa Sh 40 milioni tu, huku TFF ikishikilia hundi ya Sh5 milioni mpaka itakapopata maelekezo kamili ya TRA.
Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah, aliithibitishia Mwanaspoti jana Jumatano kuwa wamepewa maagizo na TRA kuwa wasiilipe Simba fedha hizo mpaka zikatwe Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT),
Osiah alisema alishaandikia hundi ili kulipa fedha hizo, lakini kutokana na maagizo hayo ya TRA, wamelipa Sh 40 milioni huku kiasi kilichobaki wakisubiri maagizo mengine ya TRA.
Alisema alikuwa amepanga kuandika barua TRA ili kupata ufafanuzi kwani anachojua ni kuwa Simba haijasajiliwa katika malipo ya VAT na klabu pekee iliyosajiliwa kwa mfumo huo Tanzania Bara ni Yanga. Mchezaji huyo amecheza klabu zote kubwa nchini ambazo ni Simba, Yanga na Azam
“Katika barua nataka kupata ufafanuzi kwa sababu sisi (TFF) si mawakala wa TRA kwa Simba, sisi ni mawakala wa TRA kwenye mapato ya milangoni ya timu zote, naona tayari Simba wamelipwa Sh 40 milioni kiasi kilichobaki tunasubiri kupata maelekezo ya TRA,” alisema.
Katika hatua nyingine, Osiah alifafanua kuwa alikuwa amepata barua ya Simba iliyoandikwa na Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Evodius Mtawala, ikiagiza kuwa fedha hizo si za Simba ila anapaswa kulipwa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspoppe.
“Simba wamesema fedha hizo alipwe Hanspoppe. Hata hivyo tulikuwa tumeshawalipa Simba,” alisema.