Na
Amani Mbwaga 15 Septemba 2017 Mafinga, Tanzania.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa Mhe.Amina Masenza akikagua gwaride la vijana Mujibu wa Sheria Op Tanzania ya Viwanda 2017 katika kikosi cha Jeshi Mafinga JKT. (Picha na Amani Mbwaga) |
Hayo
yamesemwa na Mkuu wa Mkoa Iringa Mhe Amina Juma Masenza wakati wa Kufunga
Mafunzo ya awali ya Kijeshi kwa Vijana wa JKT Mujibu wa Sheria kundi Tanzania
ya Viwanda katika Kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa Mafinga (JKT) kilichopo Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
“Uzoefu unaonesha
kuwa vijana wote wanaopita JKT hufanikiwa katika Maisha yao kutokana na
kuwaandaa vijana kuwa na Uzalendo Uadilifu Ukakamavu, Utii, Uhodari, Uaminifu
na kwa kujifunza shughuli mbalimbali za uzalishaji mali” alisema Mhe Masenza.
Pamoja na kwamba JKT
halitoi ajira kwa vijana lakini mafunzo haya waliyoyapata ni sawa na ajira,
kwani wamejifunza, Kilimo Ufugaji, utunzaji wa mazingira na shughuli nyingine
za mikono, hizo ni fursa za ajira zitakazowafanya waweze kujitegemea katika
hali yoyote.
Aidha Mhe Masenza
alitoa wito kwa vijana wahitimu kwamba mafunzo ya Kijeshi waliyoyapata
yakaimarishe amani na utulivu wa nchi na jamii kwa ujumla.
Pia amewataka vijana
wakadumishe sifa nzuri ya Mafinga JKT na Jeshi kwa Ujumla.
Naye Mwakilishi wa
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Michael Isamuhyo na Mkurugenzi wa ustawi wa Jamii JKT
Kaimu Kanali AS Kagombola alisema mafunzo hayo ya Jeshi la Kujenga Taifa yamelenga kuwaanda vijana wa Kitanzania kuwa
na moyo wa Uzalendo, Kupenda kazi za Mikono Kujituma, Kuilinda, Kuitetea na
Kuifia nchi yao.
Aidha katika
kutekeleza majukumu makuu ya JKT Uzalishaji Mali, Mafunzo ya awali ya Kijeshi
na Malezi kwa vijana ikiwemo stadi za maisha na stadi za kazi kuwa kielelezo
cha kutosha kwa jamii.
Pamoja na majukumu
yote hayo JKT imeendelea kuboresha miundombinu ya Vikosi mbalimbali vya Jeshi
ili kuweza kuongeza idadi kubwa ya Vijana kujiunga na Mafunzo hayo muhimu kwa
Taifa
Kwa upande wake Mkuu
wa Kikosi cha Mafinga JKT Luteni Kanali Hamisi Maiga aliwataka vijana
kutoyumbishwa na watu wasiolitakia mema taifa letu bali wazingatie kiapo chao
cha Utii, Uhodari na Uaminifu
“Fanyeni mambo yenye
tija kwa taifa na yasiyo na tija achaneni nayo” alisema Luteni Kanali Hamisi
Maiga
Waasisi wa Taifa
letu waliona umuhimu wa vijana wa kitanzania kupata mafunzo na kutoa malezi kwa
lengo la kutetea na kulilinda taifa ili kuendana na mila na desturi na
utamaduni wa Taifa letu .
JKT ilipewa jukumu
la malezi kwa vijana kwa lengo la kuondoa
makovu yaliyoachwa na wakoloni ambayo yalianza kuenezwa kwa vijana
wasomi kwa wakati huo.
Kabla ya kuanzishwa
chombo hiki vijana wale wasomi walijengewa kasumba ya wao kuwa bora kuliko
vijana wengine waliopata elimu ya
kiwango cha chini, hali hii ilipelekea mgawanyiko wa matabaka ya kielimu.
Kwa kuona umuhimu
huo JKT Ilianzishwa rasmi na kuanza kutoa Mafunzo ya vijana wasomi na wasiosoma
bila kubaguana, baadae JKT iliongezewa jukumu la uzalishaji mali na Ulinzi.
JKT ilianzishwa
Julai 10, 1963 katika uwanja wa ndani wa michezo wa Taifa (Indoor Stadium)
majira ya saa kumi na moja jioni, ambapo vijana 11 kutoka wilaya 11 wakiwa
makatibu wa vijana TYL walijiunga kwa mafunzo katika kambi ya JKT Mgulani
jijini Dar es salaam
Sanjari na hilo
Mwaka 1964 ilitungwa Sheria ya JKT (The National Service Act) ambayo ilimpa
madaraka Mkurugenzi wa JKT Kuandikisha Vijana wa Kujitolea Kujiunga na Jeshi la
Kujenga Taifa.
Sheria hiyo ilifanyiwa
marekebisho mwaka 1966 na 1967 ili kuwawezesha vijana waliokuwa wakihitimu
elimu ya Sekondari ya Kidato cha nne na Sita Kujiunga JKT Kwa mujibu wa Sheria.
Mafunzo haya ya JKT
kwa vijana wa Kujitolea na Mujibu wa sheria yaliendelea kwa ufanisi mpaka mwaka
1994, serikali ilipositisha kwa sababu mbalimbali za Kiuchumi.
Kusitishwa kwake,
watafiti walisema kuwa jamii ilishuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili na
uwajibikaji usiozingatia nidhamu, hasa kada ya vijana.
Mmomonyoko huo
ulizusha malalamiko ya makundi mbalimbali ya jamii yakitaka kurejeshwa kwa
taasisi hiyo, hali iiyowezeshwa na Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais na
Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Benjamini William
Mkapa, Kuyahuisha Mwaka 2001 kwa Vijana wa Kujitolea .
Mnamo machi 26 mwaka
2013, Serikali ya Awamu ya nne chini ya Amiri Jeshi Mkuu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alizindua upya mpango wa Mafunzo ya JKT kwa
vijana wa Mujibu wa Sheria.
Hadi sasa katika
Serikali hii ya awamu ya tano ya Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli imeendelea kutoa mafunzo hayo
ya vijana wa mujibu wa Sheria na Kujitolea kwa Kiwango cha hali ya juu hii
inatokana na kurejeshwa kwa baadhi ya Makambi ya JKT yakiwemo ya Makuyuni,
Mpwapwa, Itaka, Milundikwa, na Luwa.
Baadhi ya ndugu, jamaaa na wananchi wa mji wa Mafinga wakifuatilia kwa makini Paredi ya Vijana wa JKT Mafinga |
Kijana wa JKT Mujibu wa Sheria Service Man Mshindi wa Kwata akipokea zawadi |
Kijana wa JKT Service Girl Mshindi wa Usafi akipokea zawadi |
Paredi Ikitoka nje ya Uwanja |
Kikundi cha Kwaya ya Vijana Wa JKT Mujibu wa Sheria 2017 |
Kikundi cha Ngoma cha Mafinga JKT |
Kikundi cha Sarakasi cha Mafinga JKT |
Kikundi cha Singe cha Vijana Mujibu wa Sheria OP Tanzania ya Viwanda Mfinga JKT 2017 |
Kikundi cha Kareti Op Tanzania ya Viwanda Mujibu wa Sheria 2017 |
Vijana wa JKT Mafinga wakionesha uwezo wao Mkubwa wa Kareti |
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Juma Masenza akimshukuru Afisa Habari na Uhusiano wa Mafinga JKT Koplo Elias Mbega mara baada ya Kukabidhiwa zawadi iliyoandaliwa na Ofisi ya Habari na Uhusiano Mafinga JKT (Picha na Amani Mbwaga)
Kijana wa wa Kikundi cha Sanaa Mafinga JKT Service Man Paul Kwayu akimkabidhi Mkuu wa Kikosi Luteni Kanali Hamis Maiga CD ya Kwaya ya Kikosi Mafinga JKT. |
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Juma Masenza akihutubia Hadhara iliyojitokeza katika Mahafali ya Vijana wa Mujibu wa Sheria Op Tanzania ya Viwanda 2017 |
Mwakilishi wa Mkuu wa JKT na Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii JKT Kaimu Kanali AS Kagombola kitoa Salamu za Mkuu wa JKT |
Kamanda Mkuu wa Kikosi cha Mafinga JKT Luteni Kanali Hamis Maiga akiwaasa Vijana wa JKT |
Mgeni rasmi akiwa katika Picha ya Pamoja na aadhin ya Maofisa na askari wa Kikosi cha Jeshi Mafinga |
Mkuu wa Mkoa akia katika Picha ya Pamoja na viongozi wa Vijana OP Tanzania ya Viwanda 2017 (Picha zote na Amani Mbwaga)
Kwa mawasiliano zaidi Wasiliana nasi:
Mob 0765058711
0656632566
Email:prof.mbwaga@gmail.com